Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Habari!
Elimu ya VETA tunaweza kuiita elimu ya kati. Wakufuzi wake ni wahitimu wa elimu za juu. Wapo pia wakufuzi wenye elimu ya kati, nawafahamu.
Bahati mbaya kauli ya Majaliwa haijawataja hao wenye degree anataka waenda VETA ni degree za fani gani, na je, nini hatma ya elimu yao ya degree.
Huko VETA wakasome kozi za mda gani? Kwa lengo gani? Nani atagharamia ada na mahitaji mengine na nini hatma ya elimu yao ya VETA ikiwa hatma ya degree zao haijapatikana?
Mh. Samia usiogope gharama ya kuvunja bunge kwa kumtimua huyo Mh. Majaliwa.
Majaliwa ni jirani yangu huko Lindi ila kwenye mambo ya kitaifa Mimi sina jirani. Timua kabisa ili kuwepo na funzo kwa viongozi wengine waache kuongea kwa misisimko.
NJE YA MADA
Kama kuna mtoto wa Kiongozi mteule wa Rais anasoma VETA mje mnipige ngumi 4 za puani niko hapa TAZARA Dar es salaam nawasubiri.
Achana na watoto wa vichochoroni, nazungumzia mtoto aliyekulia nyumba za bure za viongozi.
yaan una shauriwa jambo la maana na muhimu sana kwa mustakabali wa ustawi wa maisha yako kiuchumi, kisha una beza mawaidha hayo ya maana sana kwa kiburi namna hiyo gentleman? hiyo si sawa hata kidogo,
pale VETA unaweza kupata ujuzi katika fani za ufundi ujenzi, umeme, welding, useremala n.k hata ukiwa na masters ya makaratasi, kama unaona kilimo ni kigumu zaidi, maana huko ndiko zilipo ajira za uhakika na za kutosha kwa waTanzania wote 🐒