Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Magufuli awamu yake yote hakuwa kuboresha maslai ya wafanyakazi, Samia anastahili pongezi sana
 
Kuna kitu sielewi, hii mishahara ya serikali ndio inayotumika sekta binafsi au? na vipi serikali inapanga mishahara ya sekta binafsi au uhusiano uko vipi kati ya serikali na mishahara ya sekta binafsi
 
Kwa hiyo akina sisi wenye mshahara wa 700k ni mkubwa kama wa mawaziri?
Kama una mshahara wa 700K maana yake, Nyongeza yako siyo pungufu ya Tsh 42,000 ( take home ) kwa mwezi ambayo Ni sawa na Tsh Laki 5+ kwa mwaka.
 
Sasa aliekudanganya kuhusu mshahara humjui au unajitoa akili tu.

Fanya kazi acha kumtegemea mke apandishiwe mshahara ili ukakope kupitia mshahara wake.Ujanja ujanja tu
 
Magufuli awamu yake yote hakuwa kuboresha maslai ya wafanyakazi, Samia anastahili pongezi sana
Mama kajitahidi sana, japo hata Magufuli alijitahidi pia kwa maana mfumuko ulikua chini.

Mama tunaenda nae
 
Sasa aliekudanganya kuhusu mshahara humjui au unajitoa akili tu.

Fanya kazi acha kumtegemea mke apandishiwe mshahara ili ukakope kupitia mshahara wake.Ujanja ujanja tu
Tulia ww hujielewi utakuwa unaviela vyakikafara ndomana unabwabwaja ujinga
 
Kuna kitu sielewi, hii mishahara ya serikali ndio inayotumika sekta binafsi au? na vipi serikali inapanga mishahara ya sekta binafsi au uhusiano uko vipi kati ya serikali na mishahara ya sekta binafsi
Huelewi au akili huna? Serikali inapangaje mshahara sekta binafsi?
 
Kama una mshahara wa 700K maana yake, Nyongeza yako siyo pungufu ya Tsh 42,000 ( take home ) kwa mwezi ambayo Ni sawa na Tsh Laki 5+ kwa mwaka.
42 ni gross sio take home. Japo inatosha maana hakuna kazi wanafanya
 
Tatizo wameondoa increment...ambayo huwa inabusti sana salio mara dufu ya hilo ongezeko la elfu kumi na mbili..
Mbona hajazungumzia increments ambayo ipo kisheria na wameiondoa?
Kama serikali ambayo ndio mwajiri mkuu nchini inavunja Sheria wazi wazi na hawa waajiri wengine watafanyeje?
 
Mhe. Waziri Mkuu amefafanua Vizuri Sana, Dhima ya Mhe Rais Samia Juu ya Sakata la nyongeza ya mshahara.

"78% YA WATUMISHI WAMEPOKEA NYONGEZA YA 23% YA MSHAHARA" Tukiwa bado katika kizungumkuti Juu ya Sakata la hivi karibuni kuhusu nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa Umma, leo tarehe 29th mwezi July, Mhe Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania amefafanua wazi juu ya nyongeza hii ya asilimia 23%.

"Asilimia 75 - 78 ya watumishi wote wa Umma ndiyo wanaofaidika na hii asilimia 23 ya nyongeza ya mshahara, hata Mawaziri wetu na wao wanaongezewa asilimia 0.7" - Kassim Majaliwa - Waziri Mkuu

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi mzuri sana kuhusu mambo ya nyongeza ya 23.3% ya mishahara. Kama 78% ya wafanyakazi wote wamepata increment ya 23.3% then huyu anayelalamika ni nani?

"Ukiangalia mshahara kama wa Waziri wamepata 0.7%, sasa nani amepata hiyo ni yule mwenye kipato kikubwa, ujumbe wa msingi ni kwamba asilimia 23 iliyotamkwa haijalipa watu wote,"- Waziri Mkuu

"Hao wanaosema kwamba tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye hii asilimia 22, huku ndiyo utawakuta Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha,"- Waziri Mkuu

Hakika Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ana nia ya dhati, na wafanyakazi wote aliwaambia ataendelea kuboresha maslahi ya watumishi. Hivyo tuendelee kuumunga mkono.
 
Increment kwa kiswahili ni ongezeko, au ulitaka kusemaje?
Uliajiriwa vipi ukiwa mweupe hivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…