View attachment 2308131
Mhe. Waziri Mkuu amefafanua Vizuri Sana, Dhima ya Mhe Rais Samia Juu ya Sakata la nyongeza ya mshahara.
"78% YA WATUMISHI WAMEPOKEA NYONGEZA YA 23% YA MSHAHARA" Tukiwa bado katika kizungumkuti Juu ya Sakata la hivi karibuni kuhusu nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa Umma, leo tarehe 29th mwezi July, Mhe Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania amefafanua wazi juu ya nyongeza hii ya asilimia 23%.
"Asilimia 75 - 78 ya watumishi wote wa Umma ndiyo wanaofaidika na hii asilimia 23 ya nyongeza ya mshahara, hata Mawaziri wetu na wao wanaongezewa asilimia 0.7" - Kassim Majaliwa - Waziri Mkuu
Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi mzuri sana kuhusu mambo ya nyongeza ya 23.3% ya mishahara. Kama 78% ya wafanyakazi wote wamepata increment ya 23.3% then huyu anayelalamika ni nani?
"Ukiangalia mshahara kama wa Waziri wamepata 0.7%, sasa nani amepata hiyo ni yule mwenye kipato kikubwa, ujumbe wa msingi ni kwamba asilimia 23 iliyotamkwa haijalipa watu wote,"- Waziri Mkuu
"Hao wanaosema kwamba tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye hii asilimia 22, huku ndiyo utawakuta Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha,"- Waziri Mkuu
Hakika Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ana nia ya dhati, na wafanyakazi wote aliwaambia ataendelea kuboresha maslahi ya watumishi. Hivyo tuendelee kuumunga mkono.