The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Safi sana Serikali,shikilieni hapo hapo..Majitu yana mavitambi ya wizi eti yaongezewe salary..Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa amesema wengi wanaolalamika kupata ongezeko dogo la mishahara ni wale ambao wana mishahara mikubwa. Ametolea mfano wa mawaziri kuwa wako baadhi ambao ongezeko lao ni 0.02%
Amewaomba watumishi kuwaamini viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Amesema wengi waliopata ongezeko kubwa ni wale watumishi waliokuwa wanapata mishahara midogo.
Pia amesema wananchi wanapaswa kushukuru kwa ongezeko hilo ambalo miaka kadhaa iliyopita haikuwepo
Fedha ya nani? Kama huelewi ni wewe na je wewe ni Kati ya watumishi waliongezwa 20,000?Yule aliyekuwepo hakuongeza mishahara lakini miundombinu ilijengwa. Huyu wa sasa haieleweki fedha inaenda wapi
Tulishazoea miaka yote tunapambana lakini kwa nini utangaze ongezeko ambalo halipo...basi wangekaa kimyaa Kila mtu Aone tu Kuna ongezeko Wala hakuna angepiga keleleJambo la msingi wafanyakazi ni kutafuta vyanzo vingine vya mapato nje ya mshahara
Punguza speed ya kujibu, akili huna usisahau hiloFedha ya nani? Kama huelewi ni wewe na je wewe ni Kati ya watumishi waliongezwa 20,000?
Wewe ni kajinga,umepunguziwa Paye kwa 1%,umeongezwa salary,umefutiwa uharamia wa loanboard na bado ukapandishwa daraja ila bado unaongea upumbavu wako...tena yule ni bora kuliko huyu, yule alipunguza PAYE ambayo iliongeza mshahara kiasi cha kutosha, huyu anashauriwa vibaya na walamba asali kina mwigulu, huku danganya toto nyongeza ya shahara huku unaongeza mitozo kila pahala ili mradi tu kumkera mwananchi, ee Mungu eee tumekuachia baba! amua na huu ugomvi
Wewe ndio unachagua Rais? Nenda Kwa wananchi kawambie msichague ccm kwa sababu haijawaongezea watumishi salary uone utakachojibiwa.Kwa majibu kama haya inatosha kusema 2025 wasalimie Ruangwa. Majibu hayana mashiko kabisa na mbaya zaidi Hangaya aliamua kuwapa matarajio makubwa wafanyakazi.
Ni lini na wabunge watalalamika posho ndogo? Ikitokea hii kweli nitaona uzalendo umemkuta mkutwa.
Jibu swali uliloulizwa kama hujui wengine watajibu, no worriesHapo nahitaji kujibu nini? Wewe akili hauna?
Serikali inawezaje kumpangia Mo Dewji au bakhressa jinsi ya kuwalipa wafanyakazi wake?
Sasa tucta ndio watafanya nini? Hoja ya tucta ni hiyo hiyo kwamba kima Cha juu hawajaongesewa salary hivyo waliowaombea 15% ambayo serikali imekataa.Isije ikawa wamekwisha malizana na tucta kwa sababu kauli ya mara ya mwisho kutoka serikalini walisema tucta wameenda kujadiliana... Sasa tucta kabla hawajasema tena kitu leo waziri mkuu amezungumza
Hakuna chochote, serikali imeshaweka msimamo.Leo usiku au kesho kutatengenezwa bonge la tukio Kama uteuzi,utenguaji etc ili tukio hili lifunikwe.
Wataalam wako jikoni wakitengeneza movie la kihindi,'steringi' lazima afie kwny shamba la maua.
Hakuna chochote, serikali imeshaweka msimamo.Leo usiku au kesho kutatengenezwa bonge la tukio Kama uteuzi,utenguaji etc ili tukio hili lifunikwe.
Wataalam wako jikoni wakitengeneza movie la kihindi,'steringi' lazima afie kwny shamba la maua.
Mambo mazitk kama yapi? Kauli nyepesi kama ipi?Kweli hii ni Serikali ya kipekee duniani,Prime Minister anaongea kauli nyepesi kwa mambo mazito huku akipigiwa makofi na watu walionuna mioyo.
Hilo ongezeko ni la ajabu kweli.Japokuwa mimi siyo mwanahisabati lakini kutoa na kujumlisha hakunishindi kihivyo.Nimebahatika kuona pay slip moja hapa,Basic 1,820,000/= mwezi June&July Basic salary 1,865,000 na kwa hesabu ya kichwa ongezeko ni =Tshs 45,000;ambayo ni sawa 2.5% na kwenye take home July imeongezeka Tsh 26,000 hivi ambayo ni sawa na 62.4% ya 45,000 aliyoongezewa ikiwa makato ni 23.6%,je huyo mtu naye aishukuru serikali kwa nyongeza aliyoisubiri kwa miaka 5?
Hapo bado hajakutana na tozo za miamala,VAT ya 18% kwa kila manunuzi,kupanda kwa bei za bidhaa na huduma kwa karibia 60% miaka 5 iliyopita.Funga kazi ni pensheni ya mkupuo ya 33.3%.Wafanyakazi wa Tanzania ya Tanganyika asipokufa kwa njaa atakufa kwa stress.
Chadomo waongezeeni salary basi.Sasa hapo watumishi bado mnasubiri tena majibu tofauti kutoka serikalini?huyu Muongo wa taifa ndio ameshafunga hilo suala.
CCM ni laana ya taifa hili
Ongezeko gani halipo? Hujaona formula iliyotumika?Tulishazoea miaka yote tunapambana lakini kwa nini utangaze ongezeko ambalo halipo...basi wangekaa kimyaa Kila mtu Aone tu Kuna ongezeko Wala hakuna angepiga kelele
We jamaa ni mtumishi w umma au unaongea tu tubishane hapa.Increment kwa kiswahili ni ongezeko, au ulitaka kusemaje?
Uliajiriwa vipi ukiwa mweupe hivi?
Increment ni ongezeko la mwaka ambalo mtumishi anapaewa kupata hata kama rais hajaongeza mishahara..Increment kwa kiswahili ni ongezeko, au ulitaka kusemaje?
Uliajiriwa vipi ukiwa mweupe hivi?
Mambo yanazidi kuwa "zig zag" kwa hiyo 78% ya watumishi walikuwa wanakula 300000 ( kima cha chini) maana ndo waliopewa 23%View attachment 2308131
Mhe. Waziri Mkuu amefafanua Vizuri Sana, Dhima ya Mhe Rais Samia Juu ya Sakata la nyongeza ya mshahara.
"78% YA WATUMISHI WAMEPOKEA NYONGEZA YA 23% YA MSHAHARA" Tukiwa bado katika kizungumkuti Juu ya Sakata la hivi karibuni kuhusu nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa Umma, leo tarehe 29th mwezi July, Mhe Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania amefafanua wazi juu ya nyongeza hii ya asilimia 23%.
"Asilimia 75 - 78 ya watumishi wote wa Umma ndiyo wanaofaidika na hii asilimia 23 ya nyongeza ya mshahara, hata Mawaziri wetu na wao wanaongezewa asilimia 0.7" - Kassim Majaliwa - Waziri Mkuu
Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi mzuri sana kuhusu mambo ya nyongeza ya 23.3% ya mishahara. Kama 78% ya wafanyakazi wote wamepata increment ya 23.3% then huyu anayelalamika ni nani?
"Ukiangalia mshahara kama wa Waziri wamepata 0.7%, sasa nani amepata hiyo ni yule mwenye kipato kikubwa, ujumbe wa msingi ni kwamba asilimia 23 iliyotamkwa haijalipa watu wote,"- Waziri Mkuu
"Hao wanaosema kwamba tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye hii asilimia 22, huku ndiyo utawakuta Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha,"- Waziri Mkuu
Hakika Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ana nia ya dhati, na wafanyakazi wote aliwaambia ataendelea kuboresha maslahi ya watumishi. Hivyo tuendelee kuumunga mkono.