Themagufulianz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2017
- 4,548
- 1,993
Hivi Majaliwa anajua idadi ya watu duniani ni around 8b? anamaanisha zaidi ya 50% walifuatilia? Au alimaanisha 39milioni?
Hivi population ya dunia ni ngapi mpaka leo maana huenda ni wachache tu ambao hawakuona.
Nimeshtuka balaa ....
Kwanini mkuu maana ana taarifa nyingi sana huenda ni kweli.
Waziri mkuu wa Tanzania ametoa taarifa hiyo huko Zanzibar katika hadhara ya kuaga mwili wa JPM Leo, hii ni miongoni mwa rekodi kubwa kabisa kutokea hapa Africa, R.I.P Magufuli.
Event kubwa(Category ya mazishi) duniani iliyovunja rekodi ni ya Michael jackson(Memorial Service) ,ilikuwa na viewers bilioni 2.
Kumbe wamezidi hatawale wanao fuatilia kombe la dunia world Cup. KWELI JPM NI BABA wa Africa.
Kama bado Mnamwamini majaliwa shauri yenu.
Sababu ni kuwa ni uongo mtupu, na hakuna mtu wa kumfatilia hata hapo Kenya watu walikuwa busy na mambo yao.
Mmmhh uongo wa kiwango cha SGR ,yaani amevunja mara nne rekodi ya Mohamad Ali alifatiliwa na idadi ya watu bilioni 1.
Duh! So nusu dunia ilikuwa ikifuatilia tukio la jana la kuagwa rais wetu mpendwa..tukumbuke dunia inakadiriwa kuwa na watu bilion saba na pointi kadhaa
inashangaza kuona bado zama za kupika namba zinaendelea ..sijui wanafanya hivyo ili wamfurahishe nani.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2019, Inakisiwa watu 7.674 billion wanaishi Duniani. Ndiposa tuseme 50% ya Wakazi wa Dunia walifuatilia shughuli ya Jana.Akiwa anatoa maelezo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu amesema kwa taarifa walizonazo jana wakati wa shughuli za kumuaga Hayati JPM watu waliofuatilia tukio hilo duniani ni 3.9 bilioni kama siyo 4 bilioni.
Na hivyo amevishushukuru sana vyombo vya habari kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja.
“Tunavishukuru vyombo vya habari vimekuwa na sisi toka siku ya kwanza kuwahabarisha Watanzania, hata tukio hili mnalirusha duniani kote. Mpaka jana jioni tunazo taarifa watu waliofuatilia tukio la kuaga kitaifa jana Dodoma ni zaidi ya watu bilioni 3.9” - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Kama Jana walikanusha maduka kufungwa kwa nguvu Kariakoo na Dodoma, bado mnawaamini hawa waliosema Magufuli ni mzima tarehe 15/3 ghafla wakatangaza kifo chake 17/3 utadhani kafa kwa ajali!
Huyu waziri si ndio alituambia rais yupo ofisini achapakazi?
Siamini Kama itv karibia NUSU Dunia nzima ifuatilie.mabeberu na propaganda sijui habari inakaaje Hapa Ila UN wamesema Kuna msiba.
Inawezekana ni wale waliopiga kura za kwenye mabegi.
Sawa wewe mwenye mawazo ya kizalendo endelea kutumia majani ya michongoma,changanya shubiri pia,weka na majani ya migomba na nyanya chungu ndani yake,usisahau pia kuweka mavi ya mbuzi na ng'ombe kikombe kimoja Bw Mzalendo,unywe mara tatu kwa siku,ujifukize pia dakika 40 upone corona[emoji1787][emoji1787]Una fikra za kitumwa,umeharibiwa na Mbeligiji!!
Dunia ina watu BILIONI 7.
Kati ya hao BILIONI 6 hawaijui kabisa Tanzania wala Magufuli.
Hao Bilioni 1 wanaobakia kuna vichaa, watoto, watu wa vijijini wasio na tv wala umeme, wanafunzi ambao muda huo walikuwa darasani n.k
NAMBA HAZIDANGANYI.