Waziri Mwigulu: Baadhi ya waliopotea wanahusika na uhalifu

Kwa maana yako kukimbia mkono wa sheria ndio wanajitunbukiza kwenye kiroba wenyewe na kujifunga jiwe kubwa na kujitosa baharini au ziwani?
Uneshawahi kusikia dhana ya homicide-Suicide?
 
Huwa mnatia aibu sana mnapojaribu kukimbia hoja kwa style hii ya kujitoa ufahamu.

Ina maana umesahau humu humu jamvini tumewahi kujadili juu ya watu wanaojiteka?
Kwa nini hampendi kusikia ripoti halali kutoka kwa waziri huku mkibaki na hoja za uongo msizokuwa na ushahidi nazo?
 
Ok, nakubaliana nawe lkn vp kuhusu Mh Lissu kushambuliwa kwenye viwanja vya Bunge nalo mnawahitaji ndugu zake wadhibitishe hilo?? Mnapaswa kuwa na kumbukumbu wakati mwingine. Kila kitu tunafahamu ila pakwenda hatufahamu. Hata ninyi kuna siku wakwenu atapotea halafu tuone nanyi mtakwenda kuripoti wapi.
 
ingekuwa na maana kama mh mwigulu angetoa takwimu au idadi ya waharifu wenye kesi mahakamani, au waliofungwa, kutoka kundi la wanaodaiwa kupotea. pungufu ya hapo hoja ya waziri ni butu.
 
ingekuwa na maana kama mh mwigulu angetoa takwimu au idadi ya waharifu wenye kesi mahakamani, au waliofungwa, kutoka kundi la wanaodaiwa kupotea. pungufu ya hapo hoja ya waziri ni butu.
Wewe ndio unakuwa butu kwa kukataa kuelewa neno rahisi la Mwigulu kwamba wapo waliojipoteza baada ya kufanya uhalifu na kuwa kwenye list ya wanted
 
Anasema ni wahalifu yeye ni mahakama? Vere stuppdit!
 
Amejuaje kama "walijipoteza" kwa sababu ya uhalifu wakati hawajakamatwa?

Jamaa za hao waliopotelewa na ndugu zao wanapouliza ndugu yao yuko wapi kwa nini hawaambiwi kwamba ndugu yao huyo ni "wanted" ndio maana labda amekimbia?
 
Aseme nini sasa! Kwasababu hata uongo huishiwa maneno ya "Uongo mpya".
 
Amejuaje kama "walijipoteza" kwa sababu ya uhalifu wakati hawajakamatwa?

Jamaa za hao waliopotelewa na ndugu zao wanapouliza ndugu yao yuko wapi kwa nini hawaambiwi kwamba ndugu yao huyo ni "wanted" ndio maana labda amekimbia?
Umefuatilia na kujua ni ndugu wangapi wameulizia ndugu zao Polisi na wakajibiwa hivyo?
 

TUMEKUWA TUKISHUHUDIA VIOJA KWENYE UTAWALA HUU KUTOKA KWA MAWAZIRI KUSHINDWA KUJIBU MASWALI. HIVI KARIBUNI NIMEMSIKIA MWIGULU NCHEMBA AKIBORONGA BUNGENI. ANASEMA ETI KUNA WATU WALIOTOWEKA AMBAO WANATAFUTWA NA POLISI NA SI KILA HABARI INAWEZA KUTOLEWA KWA WANANCHI.

KWANZA, ZITTO ALIKUWA ANAULIZA SPECIFIC QUESTION FOR A SPECIFIC ANSWER NA ALITAJA MAJINA YA WATU WALIOTOWEKA. JIBU LA WAZIRI HALIKUGUSA HATA KESI MOJA KATI YA WATU ALIOWATAJA ZITTO. BADALA YAKE WAZIRI "ALIJIBU" SWALI IN GENERAL.

HAKUNA MTU ANAYETAKA KUJUA SIRI ZA SERIKALI ILA WATU WANATAKA HAKI ITENDEKE. KWA MFANO, KAMA SERIKALI INAMTUHUMU BEN SAANANE KWA KUVUNJA SHERIA INGESEMA WAZI KWAMBA ANATAFUTWA NA POLISI. NA SIO KITU KIGENI KUSIKIA POLISI WANATOA TANGAZO KWAMBA MTU FULANI ANATAFUTWA KWENYE NCHI KARIBU ZOTE HAPA DUNIANI.
HIKI NI KISINGIZIO KINACHOTUMIWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KUEPUKA LAWAMA KUTOKA KWA WANANCHI. MWIGULU NCHEMBA ANGEWEZA KUSEMA KWAMBA BEN SAANANE ANATAFUTWA KWA TUHUMA KADHA WA KADHA, HUKU SIO KUTOA SIRI ZA SERIKALI.

KAMA NINGEKUWA NI ZITTO KABWE NINGEMBANA WAZIRI KWA SWALI LA NYONGEZA, JE BEN SAANANE ALIKUWA ANATUHUMIWA KWA KOSA LOLOTE?

KAMA NILIVYOTAJA HAPO JUU NI KAWAIDA KWA POLISI DUNIANI KOTE KUTOA MATANGAZO YA WATU WANAOTAFUTWA KWA TUHUMA MBALI MBALI. WATU WANATAKA KUJUA KAMA HAO WATU MAARUFU WALIOTOWEKA WALIKUWA NA TUHUMA ZOZOTE
 
Huyu jamaa ni mpuuzi sana kila kukicha anabadili kauli yake. Kwanza alidai hii miili inayookotwa si ya Watanzania bali ni miili ya watu kutoka nchi za jirani. Sasa tena anakuja na hili la kupotea ni kwamba wanahusika na uhalifu. Atwambie ni kifungu kipi cha sharia za Tanzania ambacho kinaruhusu waliohusika na uhalifu kupotezwa!? Na ni uhalifu upi wa Mtanzania ambao hukumu yake ni kupotezwa na hutolewa na mahakama ipi? Na hizi kesi za hao wahalifu waliopotezwa zilifanywa katika mahakama ipi na hukumu kutolewa lini na jaji/majaji gani?

Huyu jamaa ni mpuuzi sana.

Serikali inatoa majibu mepesi kama watu wote ni wajinga.
 

anaweza kusema chochote ashatuona wajinga.
 

Sijui kama umemuelewa vizuri Mwigulu. Anachosema yeye ni kwamba wakati mwingine watu huwa wanakimbia mafichoni kama wakiwa wamefanya makosa. Sawa nakubali, ninachotaka aseme ni je mtu kama Ben Saanane alikuwa na tuhuma zozote ambazo zingemfanya akimbie? Kama ni mtuhumiwa basi serikali iseme bayana ili ipate ushirikiano wa wananchi kumsaka.
 
 
Kwa maana hiy muhalifu dawa yake kupotea? ?!
Asante mheshimiwa
 
Iko haja ya mliosoma na hawa watu mtwambie uwezo wao darasani ulikuwaje?
Tusijekuwa tunapoteza muda kujadili kauli zake kumbe ndio akili imegotea hapo.

PHD sometimes yaweza kuwa "Pengine Hana Degree"
 

Zitto alimuuliza waziri specifically kwa kumpa majina ya watu. Waziri akatoa majibu ya ujumla bila kutaja hata kesi moja ya majina aliyopewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…