Waziri Mwigulu: Sijasema fedha za AZAKI ipewe Serikali

Waziri Mwigulu: Sijasema fedha za AZAKI ipewe Serikali

Kama AZAKI zitakubali kutoa ushirikiano, kwanini serikali isiahidi kusimamia vizuri miradi ikamilike kwa viwango? Sote si tunajenga nyumba moja?

Sioni hata ugumu uko wapi. Labda tunatofautiana uelewa.
Ukweli ni kwamba sio kila kitu AZAKI zinafanya serikali inapenda.

Zipo nyingine kazi ni kuimarisha uwajibikaji, ndio zikifanya kazi yake; wakurugenzi wanaishia kuambiwa sio raia.
 
Kama AZAKI zitakubali kutoa ushirikiano, kwanini serikali isiahidi kusimamia vizuri miradi ikamilike kwa viwango? Sote si tunajenga nyumba moja?

Sioni hata ugumu uko wapi. Labda tunatofautiana uelewa.
Serikali ianze kutoa ushirikiano kwa kufuta kodi kwenye Shughuli za AZAKI na vifaa vinavyoagizwa na AZAKI
 
Na wewe Waziri usikubali hizo fedha wapewe hao Azaki, watazila hakuna kitu cha maana zitafanya.

Hizo pesa ziwe kwenye account maalumu ya serikali kuzimonitor.

Mwendazake hakuwa mjinga kuzuia hizo pesa kuja kinyemela.

Azaki waainishe miradi ya kutumia hizo pesa sio tuu kuja kununua condom na ped eti ndio matumizi ya maendeleo.

Mwisho hao Azaki wawe wanapanga mipango yao Kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya Nchi sio kila mtu anafanya lwake.
Sijui wewe ni darasa la ngapi..? wWacha niishie kucheka tu... [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapana, yuko sahihi. Tazama hata video akiwa anazungumza kwenye kikao, utaona akishauri AZAKI ziende sanjari na Dira ya Taifa, Mipango na Vipaumbele vya Serikali ili kuwe na ushirikiano katika kuleta maendeleo. Hakusema hizo fedha ipewe Serikali.
Kwanini awapangie? au walisaidiana kuziomba huko ubeberuni?
 
Tatizo AZAKI huwa hazishirikishwi kwenye upangaji wa Dira za taifa

Wanakaa maofisa wa Serikali peke yao kutengeneza dira na mpango ya maendeleo

Pili AZAKI aziache wafadhili huwa hawapendi AZAKI kuingiliwa na Serikali ni kama Serikali ikiingilia mambo ya mashirikisho ya vyama vya michezo tumeona Kenya ikipigwa marufuku kushiriki michuano ya kimataifa baada ya Serikali ya Kenya kuingilia mambo ya uongozi wa chama cha mpira kenya

TATU ,AZAKI hupeleka write ups zao kwa wafadhili ikiwemo USAID kwenye maeneo ambayo wanaona kuna ombwe ambalo Serikali huwa Haija li cover.
Hizo azaki sio michezo yenye mashirikisho yao kimataifa. Azaki zinajidai kwamba zinajishughulisha na maendeleo ya jamii. Hayo ni majukumu ya serikali yetu sio serikali ya marekani.

Kama wamarekani wanatusaidia lazima hao wakala wao azaki wafuate mipango iliyowekwa na serikali yetu. Sio fedha inatolewa eti kutetea haki za mashoga.

Kuna mambo mengi ya ovyo tu kuwapoteza watu malengo ya maana ili kwenda na mipango ya kibeberu ya wamarekani.

Kwa hivyo hela hizo kwa azaki kwa kweli lazima zisimamiwe kuona zinafanya nini.
 
Maelezo ya kipuuzi. Azaki za kiraia zina vipaumbele vyake, na siyo laza viwe vipabele vya Serikali.

Mwigulu anataka NGOs ziwe idara za Serikali?
Hata mie nimeshangaa,Mtoaji mwenyewe anajua mission ya NGO.Anajua kupitia madelu zitapanwa zije zinunue uchaguzi
 
Hapana, yuko sahihi. Tazama hata video akiwa anazungumza kwenye kikao, utaona akishauri AZAKI ziende sanjari na Dira ya Taifa, Mipango na Vipaumbele vya Serikali ili kuwe na ushirikiano katika kuleta maendeleo.

Hakusema hizo fedha ipewe Serikali.
Haya ni maandiko yake mwenyewe. Mnapopindisha kauli zao wenyewe ni kwa manufaa ya nani? Acheni ujanja janja
Screenshot_20220328-090438_Twitter.jpg
 
kwenye hizo hela hamna azaki ya haki za binadamu? maana kwa wenzetu haki za binadamu zipo nyingi ila ile ya wale jamaa wa “upinde wa mvua" ndio wanaipambania sana
 
Unamtetea huyo muhuni?
Na ni muhuni kweli. Unakumbuka Arusha aliua watu wasio na hatia kwa bomu pale Soweto? Huyu hashindwi chochote. Baadae akaibukia kwa TB Joshua. Mungu tu asaidie Mwigulu asiende mbele zaidi ya uwaziri. Atakuwa ni janga kuliko JPM. Asikiaye na afahamu!
 
Pamoja na kupora wanyonge akiba zao kupitia tozo holela, bado anatolea udenda pesa za wahisani.......jamaa chenga sana.
 
Hizo azaki sio michezo yenye mashirikisho yao kimataifa. Azaki zinajidai kwamba zinajishughulisha na maendeleo ya jamii. Hayo ni majukumu ya serikali yetu sio serikali ya marekani.

Kuna mambo mengi ya ovyo tu kuwapoteza watu malengo ya maana ili kwenda na mipango ya kibeberu ya wamarekani.

Kwa hivyo hela hizo kwa azaki kwa kweli lazima zisimamiwe kuona zinafanya nini.
1 Kama jukumu la maendeleo ya jamii ni jukumu.la Serikali tu siyo la Marekani kwa nini Serikali huwa inaenda kuomba pesa za misaada maendeleo Marekani?
2.Unataka kusimamia pesa ambayo sio yako .Mtu kaenda kuomba kipawa hata akiila yote au kujenga wewe inayohusu nini.Shukuru tu kuwa kuna pesa wameingia kwenye mzunguko wa pesa nchini
 
Back
Top Bottom