Waziri Nape atembelea Multichoice, awarudishia DSTV 'local channels' baada ya marekebisho ya kanuni

Waziri pia afuatilie na kuondoa ukiritimba wa DSTV kuonesha michezo ya EPL ili local company nayo iweze kuonyesha mpira.Azam kwa sasa ina watazamaji wa kutosha kupata kibali cha kuonesha EPL ...
 
Umechanganya mkuu,

Dstv ndio ilikataa kuonesha hizo chanel bure yani bila malipo, baada ya selikali kuja na sheria kwamba visimbusi vyote lazima vioneshe chanel za ndani bila malipo.

Ndipo azam, startimes na wengine wakakubali ila dstv wao waligoma na wakaamua kufuta chanel zenyewe kwenye kisimbusi chao.
Siyo kweli unachosema Ni mabadiliko ya Kanuni namba 16 ya miundombinu ya utangazaji kidigitali ndiyo iliwabana DSTV ndiyo maana leo baada ya Waziri kutangaza mabadiliko ya Kanuni hyo wafanyakazi was Multichoice walishangilia Sana kwa vigelegele mpaka Nape mwenyewe akawanyamazisha ili aendelee kuongea
 
Waziri wa habari, Nape Nnauye ametangaza kurejeshwa kwa 'Free local channels' kwenye king'amuzi cha DSTV alipofika ofisi za Multichoice Tanzania akiyataja kama maagizo ya Rais Samia kurekebisha kanuni na Sheria.

Agosti 12, 2018 DSTV ililazimika kuondoa chaneli za FTA baada ya mamlaka ya mawasiliano nchini kuipiga mkwara wa uwezekano wa kuifutia leseni endapo itaendelea kwani ilikuwa hairuhusiwi kulipia chaneli hizo zinazopaswa kuwa bure.

Uamuzi huu pia iliwadhuru wote waliokuwa wanaendesha ving'amuzi kwa mfumo wa 'DHT' ambao iliwajumuisha pia Azam na Zuku ambao wenyewe waliamua kufata masharti na baadae kuruhusiwa.

Waziri wa mawasiliano wa wakati huo, Dkt. Mwakyembe akitoa sababu za kuzuia, alisema leseni ya kampuni hizo tatu ilikuwa na maudhui ya kulipia(Pay TV) hata kwa chaneli za FTA na pesa ikiisha zinazimwa kama luku. Pia alisema miundombinu yao ya urushaji matangazo haiko nchini.

Mwakyembe alisema waandaji wa maudhui(TV Stations) wana uhuru wa kuchagua TV zao ziwe za umma au kulipia na wakichagua za umma mapato yao yanatokana na matangazo ya biashara pekee bila kumtoza mteja kitu ambacho alisema DSTV walikiuka.

Pia, soma=> Waziri Mwakyembe: Azam, Zuku na DSTV walirusha maudhui ya ndani kinyume na leseni zao! Lazima warejeshe fedha zote walizowatoza Wananchi

View attachment 2102845View attachment 2102846View attachment 2102847
Barua inasainiwa na waziri au KM wa Wizara
 
Waziri pia afuatilie na kuondoa ukiritimba wa DSTV kuonesha michezo ya EPL ili local company nayo iweze kuonyesha mpira.Azam kwa sasa ina watazamaji wa kutosha kupata kibali cha kuonesha EPL ...
Swala la DSTV kuonyesha EPL siyo ukiritimba ...
Ishu Ni kwamba matangazo ya EPL yanauzwa Ghali Sana

Na kwa bara la Africa Ni DSTV na beIN sports Pekee ndiyo wamepewa idhini ya Kurusha Matangazo ya EPL na kila mmoja Ana mipaka yake beIN Sports Ni afrika kaskazini na Super sports Ni Sub Sahara Africa

Kampuni nyingine Kama Azam na Startimes Wkionesha basi Ni Baadhi ya Mechi ndogo ndogo Tena Siyo bure ....lazima walipie na wapate kibali maalum

Azam ilibidi wanyamaze kwa Maana walishindwa kufikia Vigezo na Masharti

Kwa hyo hapo serikali haihusiki kabisa

Tatizo Helaaa
 
Siyo kweli unachosema Ni mabadiliko ya Kanuni namba 16 ya miundombinu ya utangazaji kidigitali ndiyo iliwabana DSTV ndiyo maana leo baada ya Waziri kutangaza mabadiliko ya Kanuni hyo wafanyakazi was Multichoice walishangilia Sana kwa vigelegele mpaka Nape mwenyewe akawanyamazisha ili aendelee kuongea
Kanuni hiyo ilikuwa inasemaje?

Na kwa nini azam na wengine walikuwa wanarusha hizo chanel bure ila dstv pekee ndio ilikuwa hairushi?
 
Waziri pia afuatilie na kuondoa ukiritimba wa DSTV kuonesha michezo ya EPL ili local company nayo iweze kuonyesha mpira.Azam kwa sasa ina watazamaji wa kutosha kupata kibali cha kuonesha EPL ...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hicho unachokisema hakihusiani kabisa na wizara ya habari ya tz
 
Kanuni hiyo ilikuwa inasemaje?

Na kwa nini azam na wengine walikuwa wanarusha hizo chanel bure ila dstv pekee ndio ilikuwa hairushi?
Sijui kinasemaje ila Kwa maelezo ya Waziri Nape Mwenyewe Ni Dhahiri Kwamba serikali ndyo ilikuwa Kikwazo..

Na yeye amekiri hivyo..Sasa wewe unachopinga Ni Nini?

Karudie kutazama alichokisema nape Ndiyo Utajua Hujui
 
Waziri pia afuatilie na kuondoa ukiritimba wa DSTV kuonesha michezo ya EPL ili local company nayo iweze kuonyesha mpira.Azam kwa sasa ina watazamaji wa kutosha kupata kibali cha kuonesha EPL ...
Kuonyesha EPL Azam haijiamulii tu..Dstv wana leseni ya kuonyesha EPL huku sub saharan na mpunga waliotoa sio wa kitoto aisee

Sasa Azam hawezi kupewa tu kirahisi aonyeshe mechi zote 360 kwa TZ pekee.
 
Unajua Nini mkuu
Watu wanaona Supersports waona Vifurushi ghalisana wanafikiri labda Ni Ukiritimba...

Bila kufahamu Ligi Ghali zaidi duniani na yenye Masharti magumu Sana kiutangazaji Ni Epl

Kwa mfano Kwa Marekani kituo ambacho kimepewa Idhini ya Kurusha EPL ni NBC sports na Wanalipa US$ 2 bn

Yaani hata Utajiri wote wa Mo Dewji haufikii hiyo hela.
 
Unajua Nini mkuu
Watu wanaona Supersports waona Vifurushi ghalisana wanafikiri labda Ni Ukiritimba...

Bill kufahamu Ligi Ghali zaidi duniani na yenye Masharti magumu Sana kiutangazaji Ni Epl

Kwa mfano Kwa Marekani kituo ambacho kimepewa Idhini ya Kurusha EPL ni NBC sports na Wanalipa US$ 2 bn

Yaani hata Utajiri wote wa Mo Dewji haufikii hiyo hela.
Sio mchezo..

Azam bado sana kuweza kuonyesha EPL in full..
 
Umechanganya mkuu,

Dstv ndio ilikataa kuonesha hizo chanel bure yani bila malipo, baada ya selikali kuja na sheria kwamba visimbusi vyote lazima vioneshe chanel za ndani bila malipo.

Ndipo azam, startimes na wengine wakakubali ila dstv wao waligoma na wakaamua kufuta chanel zenyewe kwenye kisimbusi chao.
Kwa taarifa ya leo hao nani kasalim amri kati ya serikali na DSTV?! I mean DSTV kamkubalia serikali kuonesha hizo local channels bure au serikali kamkubalia DSTV kuonesha hizo local channels kwa kulipia?! Maana naona kila mtu anaongea yake watu wanakwepa kufafanua point ya msingi, otherwise maagizo ya NAPE hayajaeleweka
 
Halafu mtu anazungumzia kwa Tanzania tu aiseeeeh atafirisika, we bara zima la Africa wamegawana beIN Sports na DSTV halafu mtu anakuja kusema AZAM arushe EPL mechi zote kwa Tz tu?![emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ndo ninachojiuliza na mm...itakua sio fair kwa wengine kwa kweli.
Hapo Kuna mambo mawili, siasa iliyotumika kumuondoa DStv kwenye soko la ndani ndio hiyo hiyo imemrudisha kwenye soko la ndani.

Waliona hawana namna ya kumuondoa DStv ili waingie kumiliki soko la ndani wakapitia Waziri mwakyembe kutengeneza kanuni zilizombana DStv kuonyesha channel za ndani ili Azam na wengine wadogo Kama Sahara media na continental pamoja na startimes waweze kucapitalize kwenye local channels.

Sasa DStv nae ametumia njia hiyohiyo kuondoa hizo kanuni kupitia njia ya Su
Umechanganya mkuu,

Dstv ndio ilikataa kuonesha hizo chanel bure yani bila malipo, baada ya selikali kuja na sheria kwamba visimbusi vyote lazima vioneshe chanel za ndani bila malipo.

Ndipo azam, startimes na wengine wakakubali ila dstv wao waligoma na wakaamua kufuta chanel zenyewe kwenye kisimbusi chao.
Sure
 
Halafu mtu anazungumzia kwa Tanzania tu aiseeeeh atafirisika, we bara zima la Africa wamegawana beIN Sports na DSTV halafu mtu anakuja kusema AZAM arushe EPL mechi zote kwa Tz tu?![emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Wanadhani ni rahisi kama kurusha mechi za kombe la mapinduzi.
 
Halafu mtu anazungumzia kwa Tanzania tu aiseeeeh atafirisika, we bara zima la Africa wamegawana beIN Sports na DSTV halafu mtu anakuja kusema AZAM arushe EPL mechi zote kwa Tz tu?![emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Kweli Mkuu EPL Ghali Sana Aisee
Yaani Afrika nzima Ni DSTV na beIN Sports Tena Hapo beIN Sports siyo kampuni ya Kiafrika Bali ni kampuni ya Quatar kwa hyo anahudumia Ukanda wa Nchi za Afrika kaskazini na Middle East Yote

Kwa hiyo ukiongelea Kampuni ya Kiafrika inayo mudu Kuonesha EPL Ni DSTV Pekee..

Huko Nigeria' Algeria' Misri Ni nchi tajiri Sana kuliko Tanzania lakini kwa EPL wamenyoosha Mikono Juu...sembuse Azam?

Azam Kuonesha EPL Full Table wajipange Sana siyo kitoto..

DSTV wanaume.
 
Kwa taarifa ya leo hao nani kasalim amri kati ya serikali na DSTV?! I mean DSTV kamkubalia serikali kuonesha hizo local channels bure au serikali kamkubalia DSTV kuonesha hizo local channels kwa kulipia?! Maana naona kila mtu anaongea yake watu wanakwepa kufafanua point ya msingi, otherwise maagizo ya NAPE hayajaeleweka
Dstv ndio kasalimu amri
 
Hili jambo bado lina utata sana yani Dstv aoneshe Clouds Tv ,TBC1, Channel Ten na EAtv bure kabisa hata kama mtu hana kifurushi?

Maana mwanzo DStv alikuwa anazionesha lakini kifurushi kikiisha nazo zinakata....

Hata washindani wake walilamikia sio DStv kuonesha bure bali ni kuonesha hizo channel either bure au kwa kifurushi walikataa kwakuwa leseni yake haihusu hizo channel....

Kama Nape anamaanisha hizo channel tutaziona bila kufurushi basi sidhani kama wakina Azam na wengine watakubali kwani wao wameingia gharama kubwa sana na ving'amuzi vyao vitakosa soko...:

Kauli ya Nape bado haiweleweki lakini tusubiri nini kitakuwa kati ya kuona channel bila kifurushi au kuona channel kwa kifurushi.....
 
Back
Top Bottom