Kwa pesa wanazopewa na serikali ya muungano lazima wafanye maendeleo hayo.
Lancet laboratory ni matapeli hamna kitu., rafiki yangu alikuwa anaumwa akaandikiwa achukue vipimo lancet pale kinondoni. Tulipofika wakampima wakamwambiaa majibu baada ya wiki kwani vipimo vinaenda Africa Kusini. Baada ya muda akaandikiwa achukue vipimo vingine, Kwa sababu alikuwa mkoani alitaka kujua gharama na pia kufanya appointment ili akija aje na asikae muda mrefu. Nilipoenda Lancet walinipa gharama na majibu yatachukua wiki Moja Kwa sababu vipimo vitapelekwa south Africa. Baadae nikasema nipitie TMJ niulizie gharama za vipimo. Nilipofika TMJ walinipa gharama ambazo ni za chini na kunieleza majibu nitapata baada ya dakika 45.Nilishangaa na nikawauliza mbona Lancet Bei Yao ni hii na wanaochukua wiki Moja, yule daktari alicheka na kuniambia Lancet Huwa wanaleta vipimo kwao Ile vipimo kwenda Africa Kusini ni mbwembwe tu.