Waziri Nassor Mazrui: Hospitali zote za Zanzibar kupewa Sekta Binafsi waziendeshe

Waziri Nassor Mazrui: Hospitali zote za Zanzibar kupewa Sekta Binafsi waziendeshe

Mtu binafsi anatafuta faida so lazima apige kazi kweli kweli hakuna uzembe. So as much as sikubaliani nayo ila ukweli usemwe private sector wako serious kwenye kazi kuliko serikalini.

Angalia tu ATCL linganisha na Precision, au TTCL na Vodacom, au TRA na Deloitte, ama Azania na Marian!!

Let's be serious serikali inabidi ibadili mfumo wa jinsi inaendesha taasisi ikiwezekana mishahara isitoke hazina Bali kwenye taasisi husika Ili Kila mtu alipwe kutokana na anachozalisha not otherwise
Ndicho tunataka na kwenye bandari sio upuuzi unaoendelea Sasa hivi
 
Ubepari wa ktz upoje? Wa kutoa bandari au mali za umma bure? Wawekezaji kuwahonga wabunge wetu ili wakapitishe mambo yao? Haya mambo ya viongozi wetu ukiyafuatilia kwa karibu! Unaweza kumkufuru Mungu! Ukaomba heri ungezaliwa kunguni au chawa huko afghanistan Ukanyonye mataliban damu kuliko kujinasibu eti mi mtanzania! Aibu kiwango cha blue rays
Nani anapewa Bure? Pesa zitakuwa haziingii Serikalini? Wacha upumbavu wewe jitu jizi na dokozi ,komesha yenu ni sekta binafsi
 
Hizo hospital zote zinategemea madaktari wa MNH na hata case nyingi wanazipeleka MNH
Sasa Hujiulizi why Wakiwa huko private wanatoa Huduma makini kuliko foleni ya MNH?

Agakhan haitegemei madaktari wa huko Muhimbili, Serikali ipunguze vigezo vya watu kutoka Nje wale wenye utaalamu adhimu waje.
 
Ni kwa namna gani huyo mtu binafsi ataboresha huduma wakati wewe mwenyewe huna standards za kupimia huo ufanisi unafananaje.

Taasisi ya afya iwe ya serikali au private ufanisi wa management ni kwenye kusimamia miongozo ya utoaji wa huduma za afya ni sehemu ya policies zao na practice za kila siku.

Kuna external supervising body ambayo inaweza vamia ghafla na kufanya services auditing kuangalia how the institution complies with regulations. Na yale aliyokuwa akiyafanya ‘Dorothy Gwajima’ sema nchi zingine hasa zilizoendelea kitu kile kile kinafanywa na ‘health regulator’ halafu anaandika uzembe uliokuta nao huko katika kutokufuata mifumo.

Subiri sasa hiyo report ya regulator ikishatoka halafu kituo chenye uzembe huyo wizara au halmashauri au uongozi wa hospitali itakoma kwa lawama watakazopewa na wanasiasa, media na stakeholders wa sector.

Sasa huko serikalini ata ukienda website ya wizara ya afya uwezi kukuta health services policies, regulations na kwanza ata bunge huwa alijadili health policies. God knows ata hao wanafunzi wa health management wanaandika vipi essay/zao wakati crucial material kwenye website ya wizara na wala sijui zinapatikana wapi.

Ni upuuzi tu kwenye sera za afya kinachoendelea Tanzania; hiyo sector sio ya ubunifu ni highly regulated. Bado kuna kanuni za utendaji kazi ambazo proffesional bodies husika zinatakiwa iziweke kwenye website zao na hospital management izitumie kama supervision delivery.

Kwenye afya hakuna ubunifu ni hierarchical system from UN, Government policies (regulations), policy implementation at service level and supervision at work floor. Uwezi kuongoza afya kama hujui hata hizo regulations zenyewe kwenda hospitali wakati uwezi ata kufanya service audit ni ujinga tu.

Kufanya privatisation wakati serikali aina hata policies wala vigezo vya kupima ubora wa huduma na hakuna external auditor ni ujinga.

Mna mtaalamu wa hayo mambo aliebobea ‘Dorothy Gwajima’ mtumieni ata kwa ushauri kuliko haya mambo yenu ya kijinga kijinga.
 
Hizo chini ndio module zote za health and social care management; hiyo ni ya diploma but trust me it cover more than ambacho utafundishwa kwenye degree course or masters degree.

Shida yenyewe ata ukiwapa watanzania awawezi kuandikia report hizo info, kutumia kutungia policy za serikali or even understand how to implement those measures at work place. Lakini as far as health and social care management kwa UK hizo ndio module zote nothing more only that kuna mambo machache yanabadilika kutokana na sheria/policy mpya/professional standard of intervention practice.

Ndio maana tunaposema Dorothy Gwajima anajua kwa sababu kama unaelewa hayo mambo sio siri anajua kwenye afya not so much social services alipowekwa.
 
Attachments

Saizi maeneo yote yamefikiwa na hospital za Umma , Serikali ikomeshe kutumia Kodi zetu hovyo
Iambie serikali iache kulipa ruzuku, hospitali za kanisa zipandishe gharama zitoze kama hospitali za wafanyabishara binafsi.
Bugando iwe na gharama kama Agha Khan tuone kama wauza nyanya watatibiwa. Hivi unajua kuna wilaya Tanzania hii hazina hospitali za serikali? Sasa kanisa lipandishe gharama uone wauza majeneza watavyopiga hela
 
Sasa Hujiulizi why Wakiwa huko private wanatoa Huduma makini kuliko foleni ya MNH?

Agakhan haitegemei madaktari wa huko Muhimbili, Serikali ipunguze vigezo vya watu kutoka Nje wale wenye utaalamu adhimu waje.
Ukute hujawahi enda Agakhan

Kaulize Clinic za Jumapili na Jumamosi Paeditrician ni wa hospital gani

Nenda Endoscopy uone Dr anatokea wapi
 
Ukute hujawahi enda Agakhan

Kaulize Clinic za Jumapili na Jumamosi Paeditrician ni wa hospital gani

Nenda Endoscopy uone Dr anatokea wapi
Sawa ndio mwanzo wa sekta binafsi ya afya kukua kwa India sekta binafsi ni kubwa zaidi ya umma na hapa kwetu bado sekta ya umma ni kubwa kwa level zile za juu nq ndio maana bado huduma zipo chini siku sekta binafsi ya afya kwa level ya juu ikikuwa ikafikia 85% basi watu watasahau kwenda India.
 
Iambie serikali iache kulipa ruzuku, hospitali za kanisa zipandishe gharama zitoze kama hospitali za wafanyabishara binafsi.
Bugando iwe na gharama kama Agha Khan tuone kama wauza nyanya watatibiwa. Hivi unajua kuna wilaya Tanzania hii hazina hospitali za serikali? Sasa kanisa lipandishe gharama uone wauza majeneza watavyopiga hela
Haya majaa ilimu yao yakuunga sana. Hawajui kuna bidhaa lazima serikali igharamie . Wanaamini bepari ana huruma
 
Bora zazibar huku serikali analipa kila mwaka zaid ya 40bn shilling hasipitali za kanisa wakati hizo hela zinatosha kijenga hospiatli za umma kibaya zaidi huo mkataba hauna kikomo.
Huu mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na KANISA ni jipu linalosubiri kupasuka.

Unazipa taasisi za Kanisa upendeleo wa waziwazi katika biashara zao za huduma ya afya dhidi ya wafanyabiashara wengine wanaotoa huduma kama hizo.

Upendeleo huu wa kibiashara ni kinyume cha katiba ya nchi inayosema kuwa serikali haitoendesha nchi kwa upendeleo.

Ndiyo maana hata huduma ndogo tu kama catering serikali inapaswa itangaze tenda ili watoa huduma mbalimbali wajitokeze na mchakato fair ufanywe, Licha ya kuwa mtoa huduma akipika chakula wanakula watu wote hii haiondoi ukweli kuwa fairness kwenye kumpata inatakiwa.

Hoja kuwa hospitali za kanisa zinahudumia wote haina mashiko. Hata hao watoa huduma wengine nao wanahudumia wote.
 
Zanzibar idadi ya Hospital ni sawa na za Wilaya ya Kisarawe. Hakuna la maana.
 
Akiongea na Wandishi wa habari Waziri wa Afya Nassor Mazirui (ACT wazalendo) amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ipo kwenye mchakato wa kubinafsisha Hospitali zote za Zanzibar ile ziweze kuendeshwa na watu binafsi kuleta tija.

Ikumbukwe tayari mpango huu umeshaanza kutekelezwa hasa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, ambapo huduma zote za Maabara na Vipimo vya Mionzi na Ultrasound tayari zinasimamiwa na makampuni binafsi.

Taarifa zisizo rasmi zinaonesha Lancent Labartories Ltd ndio wanaosimamia mpango huo kwa sasa. Tangu Dr. Ali Hussein Mwinyi aingie madarakani amefanya mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali kisiwani humo.

Katika Sekta ya Afya amefanikiwa kujenga hospitali kubwa za rufaa za mikoa za kisasa na kuajiri idadi kubwa ya madaktari na watoa huduma wa idara mbalimbali. Idadi hiyo inakadiriwa kuwa kiwango kikubwa kuliko awamu zilizopita.

Hata hivyo Dr. Hussein Mwinyi anapongezwa kwa usimamizi mzuri wa rasilimali za umma na hivyo kuungwa mkono na Wananchi wengi.

Safi sana.

Sisi Watawala kwanini tuteseke akili yakhee.

Tunabinafsisha kila kitu isipokuwa ofisi na Madaraka yetu.

Kazi yetu,inabaki kuletewa pesa tu, kufanya teuzi, kutembelea mataifa mbalimbali na Kula bata tu.
 
Huu mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na KANISA ni jipu linalosubiri kupasuka.

Unazipa taasisi za Kanisa upendeleo wa waziwazi katika biashara zao za huduma ya afya dhidi ya wafanyabiashara wengine wanaotoa huduma kama hizo.

Upendeleo huu wa kibiashara ni kinyume cha katiba ya nchi inayosema kuwa serikali haitoendesha nchi kwa upendeleo.

Ndiyo maana hata huduma ndogo tu kama catering serikali inapaswa itangaze tenda ili watoa huduma mbalimbali wajitokeze na mchakato fair ufanywe, Licha ya kuwa mtoa huduma akipika chakula wanakula watu wote hii haiondoi ukweli kuwa fairness kwenye kumpata inatakiwa.

Hoja kuwa hospitali za kanisa zinahudumia wote haina mashiko. Hata hao watoa huduma wengine nao wanahudumia wote.
Kanisa lirudishiwe shule zake, majengo yake, mkataba wa Afya uvunjwe.
 
Back
Top Bottom