Mkuu hicho chakula anakula mwanao au mwalimu? education is so expensive, kubali kugharamia jamani
Huu uendeshaji wa shule kwa miaka hii imekuwa mgumu sana, walimu tunapata shida sana maana wazazi wamekuwa wajuaji sana ,sasa hebu fikiria mtu ameambiwa achangie ili mwanae ale lakini anakuja kulialia huku mitandaoni,unataka sisi walimu tutoe chakula chetu kuwalisha watoto wenu?
Sasa unadhani kilo kumi atakula Mara ngapi au siku ngapi?,ukifanya mahesabu ya haraka haraka mwanao hizo kilo kumi atakula zikizidi ni siku 40,sasa shida iko wapi? Tatizo watu wamekuwa wajuaji na hawataki kuheshimu taaluma za watu,wewe mwalimu umemuamini na kimkabidhi mwanao sasa unashindwa nini kumkabidhi mchele kilo kumi ili mwanao ale na apate elimu bora?
Pia mkuu tambua kuwa sasa mtoto atakuwa anatoka kwako saa 12 na kurudi nyumbani saa 11-12/jioni sasa unadhani mwanao atakula nini kwa muda wote huu ,maana hapa inahitajika taktibani Milo miwili aipate akiwa shuleni,sasa kwa hizo kilo kumi nadhani hazitoshi,ningekuwa Mimi mkuu wa shule ningeagiza gunia zima la mchele
Shule ninayofundisha Mimi mtoto hupaswa kuchanga debe Moja la mahindi ambalo ni takribani kilo 20, na mtoto kwa mwaka mzima huchanga debe mbili za mahindi,sh elfu 10,000 na kilo kumi kwa nusu mhula,wala sijaona shida yoyote kwa wazazi,maana chakula wala watoto wao
Jamani acheni kutupa stress sisi walimu,hatuna shida na Michele yenu,ila naomba mtuamini,maana mawazo yenu ni kwamba chakula hicho kitaliwa na walimu,si kweli.
Sent from my TECNO KB7j using
JamiiForums mobile app