Waziri Ndumbaro azindua Jengo la Utalii wa mashamba ya misitu Biharamulo-Chato, atoa maelekezo kwa Sekta ya Utalii nchini

Waziri Ndumbaro azindua Jengo la Utalii wa mashamba ya misitu Biharamulo-Chato, atoa maelekezo kwa Sekta ya Utalii nchini

itaanza watumishi wote lazima wafanye utalii buricha ili wabaki na ajira,next mikutano yote ya mambo ya utalii italazimishwa kufanyika huo,then wafanyabiashara wataambiwa wakafanye utalii kama hujaenda urgency note,Makampuni ya utalii yatapewa target ya kupeleka watalii hata kama hawataki then tutapewa data za watalii waliotembelea Over.
Duh! Kazi iko. Asante kwa post yako mkuu🙏🙏
 
Hivi siku hizi Biharamulo ipo mkoa wa Chato?

Waziri Ndumbalo is a very intelligent man na mwenye msimamo - hakusema Biharamulo-Chato kwa bahati mbaya/slip up, kuna kitu wanakilenga katika harakati za kutangaza utalii - wangesema Biharamulo - Mleba/Karagwe ingewachanganya Watalii walio zoea kusikia kwenye matangazo/media kuhusu: Chato-Burigi, Chato-Lubondo, Chato..., kinacho uzika kiutalii ni neno Chato, hivi sasa icon hiyo imekwisha jengeka na kuzoeleweka Kimataifa - Dk. Ndumbalo angesema Biharamulo bila kuongezea neno Chato, sina shaka potential tourists wangekuwa confused na kuhoji kwani Biharamulo inawezaje kuwa kwenye circuit ya utalii bila ya kuishirikisha wilaya ya Chato.
 
Niliwahi kusema humu kwamba yuko waziri wa mawaziri, ndio anayetoa mwongozo wa cha kufanya, hawa mawaziri wengine wote akiwemo Waziri Mkuu kazi yao ni kujibu maswali bungeni tu.

Haiwezekani mawaziri wote waachane na Dodoma waanze kushadadia Chato, hata kama watanzania ni mabwege zumbukuku, si kwa utopolo huu wanaofanyiwa.
Uzembe wa Nyerere Butiama hatakiwi kurudiwa
 
Wananchi wa Kusini wakiangalia kinachoendelea Chato huku zao lao la korosho likiwa limehujumiwa, na 200b za mfuko wa korosho zikiwa zimeporwa kwenda kununulia ndege, kwa vyovyote watataka rais safari hii atoke kusini ili akapendelee kwao.
Si ulikuwa unampigia chapuo kachero mbobezi na uzushi wako wa korosho?
 
Waziri Ndumbalo is a very intelligent man na mwenye msimamo - hakusema Biharamulo-Chato kwa bahati mbaya/slip up, kuna kitu wanakilenga katika harakati za kutangaza utalii - wangesema Biharamulo - Mleba/Karagwe ingewachanganya Watalii walio zoea kusikia kwenye matangazo/media kuhusu: Chato-Burigi, Chato-Lubondo, Chato..., kinacho uzika kiutalii ni neno Chato, hivi sasa icon hiyo imekwisha jengeka na kuzoeleweka Kimataifa - Dk. Ndumbalo angesema Biharamulo bila kuongezea neno Chato, sina shaka potential tourists wangekuwa confused na kuhoji kwani Biharamulo inawezaje kuwa kwenye circuit ya utalii bila ya kuishirikisha wilaya ya Chato.

Bila shaka mshipa wako wa aibu ulishakatika kitambo sana.
 
Wananchi wa Kusini wakiangalia kinachoendelea Chato huku zao lao la korosho likiwa limehujumiwa, na 200b za mfuko wa korosho zikiwa zimeporwa kwenda kununulia ndege, kwa vyovyote watataka rais safari hii atoke kusini ili akapendelee kwao.
Hazijanunua ndege.zimeenda kuijenga CHATO.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
I once asked hivi hawa wanajua maana na aina za utalii duniani au wanajitungia yao ili mradi kila kitu kiwe Chaito ?
Kwakweli wangenisaidia nini maana ya utalii wa mashamba ya misitu basi ningeshukuru sana!Maana mpaka sasa bado sijaelewa!
 
Waziri Ndumbalo is a very intelligent man na mwenye msimamo - hakusema Biharamulo-Chato kwa bahati mbaya/slip up, kuna kitu wanakilenga katika harakati za kutangaza utalii - wangesema Biharamulo - Mleba/Karagwe ingewachanganya Watalii walio zoea kusikia kwenye matangazo/media kuhusu: Chato-Burigi, Chato-Lubondo, Chato..., kinacho uzika kiutalii ni neno Chato, hivi sasa icon hiyo imekwisha jengeka na kuzoeleweka Kimataifa - Dk. Ndumbalo angesema Biharamulo bila kuongezea neno Chato, sina shaka potential tourists wangekuwa confused na kuhoji kwani Biharamulo inawezaje kuwa kwenye circuit ya utalii bila ya kuishirikisha wilaya ya Chato.
Daaaah,aibu nimeona mimi kwa comment hiii!😁😁😁😁
 
Sababu kuu ya magufuli kutotaka upinzani bungeni ilikua ni hii,2015-2020 kidogo alikua anaogopa baada ya kelele kua nyingi bungeni wapinzani walisema sana.Sasa akaona dawa kuwakomoa kuwafanyia hila ili wasirudi na yeye atambe leo hakuna hata mbunge atakayehoji haya yanayofanyika na sio kama hawayaoni ila wanaogopa kumgusa M/kiti maana anaweza kukufukuza chama na ubunge ukakoma.

Kwa haya yanayoendelea inawezekana sasa Chadema ikawaruhusu Covid 19 ili wakapige spana bungeni maana uvumilivu utawashinda tu ndugu .Jiwe ameshavuka mstari na wananchi sasa tuliokua tunaona siasa haituhusu tutaona joto ya jiwe 2020-2025 ,maana miradi mingi inayoanzishwa huko chato inajengwa kwa kigezo cha sifa na kumfurahisha mtu na ndo maana inatumika nguvu kubwa sana kutuaminisha kua chato kuna fursa.

Miradi inayolazimishwa kupelekwa chato kwa sasa haina umuhimu wowote zaidi ya hasara labda ipite miaka 30 angalau ndo itaweza jikongoja lakini kwa sasa ni msiba.Rejea ATCL inavyojiendesha kihasara na bila shaka serikali inalazimika kulipa ruzuku kila mara ili lijiendeshe.

Magufuli akiondoka ataiacha nchi kwenye makovu makubwa ya uchumi,chuki,visasi,madeni na ukabila.

Nb;
Nijengeeni chato
Nijengeeni chatoooo
Nijengeeni chatoooooooooooo
 
Pamoja na yote hebu mtupe maelekezo ya kufika chato kwa kutumia usafiri wa mabasi, things nataka kufanya ni opportunity, wakati tunapiga pinga humu ila pesa kwa njia yoyote lazima itafutwe, iwe sehemu usiyoipenda au unayoipenda.
 
Kwakweli wangenisaidia nini maana ya utalii wa mashamba ya misitu basi ningeshukuru sana!Maana mpaka sasa bado sijaelewa!

Mataifa ya Ulaya specifically nchi za Scandinavia, Ujerumani (Black forest),USA na zaidi Canada mbona pamejaa misitu ya mi-pine (misonobari) kama kweli watalii wanaweza kuchoshwa kutembelea misitu ya mi-pine huko Ulaya na Marekani badala yake watalii wakikimbilia kuangalia mi-pine ya Chato-Biharamulo kuliko mi-pine ya Mufindi Iringa mbona hiyo itakuwa ni bahati kubwa na kheri ya kutangaza utalii wa kutembelea misitu yakupandwa kuliko Natural forest.

Dk. Ndumbaro na Wizara ya Utalii wanapaswa kupongezwa kwa ubunifu ulio tukuka - kilicho baki sasa ni kupandikiza samaki wa mapambo mwaloni Chato, baadae ufanyike mpango wa kuanzisha SCUBA diving kwenye ziwa la Burigi, lakini nataka tuelewane hapa kwamba asili mia 75% ya mapato yatumike kuendeleza manispaa ya Bukoba na mji wa Muleba - tuwe wakweli hapa, Burigi kiutamaduni ni sehemu ya Mkoa wa Kagera mnaweza kutaka kupindisha pindisha mambo for some strange reasons lakini ukweli unabaki pale pale, kama mnasema dhahabu inufahishe Mkoa wa Geita,kwa nini Burigi hisinufahishe Mkoa wa Kagera badala yake mnataka ziwa hilo liondolewe Mkoa wa Kagera au lisiwe associated na Mkoa huo!!!

Juzi hapa nilimuona mtalii wa Kitaliano akisema wazungu wako interested kwenye kuangalia masuala ya utamaduni, mambo ya kale na vyakula zaidi kuliko kuangalia wanyama ambao ni rahisi kuwangalia wakiwa makwao kwa kupitia TV channels zinazo onyesha documentary zinazo husu wild life - na mimi naunga mkono maoni ya mtalii - ingekuwa vema kama Wizara ya utalii ingeufanyia kazi ushauri wa mtalii huyo.

Narudia kukumbusha tena kwamba Wizara ya Utalii iweke mkazo vile vile kwenye utalii wa kutembelea vivutio vya masuala ya utamaduni Nchini na sio kwenye wildlife tu.
 
Back
Top Bottom