Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,063
- 735
Watu tuache unafiki.
Kifo ni njia ya kila mtu hapa Dunia. Zamu yako ikifika unaondoka na unaacha kila kitu ulicho chuma hapa duniani ikiwa ni pamoja na mwili wako.
Hapa JF tunapiga kelele juu ya Utendaji mbaya na wa kiibilisi wa SISIEMU ambao unaua maelfu ya Watanzania kila siku kwa namna nyingi ambazo chimbuko lake ni umasikini.
Safari za hivi karibuni za mawaziri kuzunguka Tanzania kueneza uongo zime tumia fedha nyingi sana za Taifa ambazo kwa namna moja au nyingine zingesaidia kutatua matatizo ya wanyonge katika kila kona ya Tanzania.
Pamoja na kuzunguka kwao na kujionea umasikini ulivyo tanda viongozi wetu bado wanaendelea kueneza siasa za kiuuaji ambazo ndiyo njia pekee ya kuwafanya wabaki mabadarakani.
Vibaka wakiuawa kwa kuchomwa moto picha zao zinawekwa kwenye magazeti zikionyesha moto ukiwateketeza na wengi tunaona sawa. Vibaka wengi nniliowahi kuwajua mimi pale Dar ni bread earner wa familia zao kwa sababu tu uchumi wa nchi umetiwa sumu na SISIEMU.
Kama kila mtu ataonja mauti na hatakuwa na uwezo wa kwenda na fedha hata zilizoko kwenye mifuko ya nguo zake wakati wa kifo au Mabilioni aliyoyaweka Dubai au Jumba la fahari alilojenga kwa fedha ya wizi au fahari na utukufu alio jikusanyia kwa udharimu hapa duniani.
Inamfaa nini mtu kujilimbikizia mali ya wizi?
Inamfaa nini mtu kuunga mkono udharimu Uonevu udanganyifu na ufisadi?
Inafaa nini mtu kuunga mkono chama cha watu dharimu kama SISIEMU?
Inafaa nini?
Miaka 20 iliyo pita nilifanikiwa kutembelea mikoa mingi ya Tanzania bara na Zanzibar nikajionea umasikini mkubwa uliowazunguka na kuwanga'ang'ania watanzania kama kutandwa na siafu.
Niliugua, Nililia na kutoa machozi mengi na kujiuliza SISIEMU wana fanya nini kuondoa umasikini huu mkuu?
Baada ya kilio hiki kikuu moyo wangu ukawa mgumu kama jiwe juu ya udharimu wa SISIEMU.
Moyo huo wa jiwe ulikomazwa zaidi nilipo pata kuwekwa kitako na mfuasi mmoja msomi wa James Mapalala aliyenieleza juu ya mikutano yao ya siri na juu ya mabadiriko mengi ya kisiasa yanayotarajiwa kutokea na jinsi watu kama Mapalala walivyojitolea muhanga kudai uwepo wa vyama vingi.
Wakati ule nilipigwa butwaa kama Watanzania tulivyo pigwa butwaa na List of Shame.
Leo picha za umasikini wa Watanzania bado ziko akilini mwangu, zaidi uovu wa SISIEMU ni mkuu kuliko ule ulo kuwepo miaka 20 iliyopita. Moyo wangu sasa ni mgumu kama ALMASI.
Pamoja na ukweli kwamba SISIEMU ni Watanzania wenzangu nakiri kwamba vitendo vyao vya kudhurumu utu wetu na kutudharirisha katika nchi yetu vimetusukuma mpaka mwisho wa uvumilivu wetu kiasi kwamba wengine tumejiapisha viapo vingi vya kupambana nao.
Vitendo vyao vinatulazimisha kuwaweka kwenye kundi moja na maadui wa maendeleo ya taifa letu.
Ni vigumu kwangu kuvua shati la machungu ya SISIEMU na kuingiwa Simanzi pale mmoja wao akipatwa maafa.
Huu ndiyo ukweli, tena ukweli unao uma.