Waziri Selemani Jafo ashauri kuanzishwa kwa wiki ya nyungu katika kupambana na Corona

Waziri Selemani Jafo ashauri kuanzishwa kwa wiki ya nyungu katika kupambana na Corona

Kujifukiza hakuna maana watu wote watapona!,kumbuka hili gonjwa halina dawa sidhani kama wewe mwenzangu lilikupata unaweza tulia tu bila kujaribu namna yoyote!,malaria inadawa tena hizo za kizungu lkn watu bado wanakufa kwa malaria tena wakiwa kwenye dozi...unapuuzia kujifukiza kwasababu hujaumwa!
Hii serikali ni washirikina kabisa. Hakuna tena ubishi

Wamemdanganya Ndasa masikini badala ya kuwahi hospital yeye kakomaa kujifukiza. Matokeo yake mnayajua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumeambiwa tutumie wiki inayokuja kwa kila mmoja wetu kujifukiza (Nyungu) mara tatu kwa siku.

Hata kama hiyo ni tiba, hivi ni kweli utajifukizia hata kama huumwi? Viongozi wa Tanzania acheni masihara na utani kwenye maisha ya watanzania.

Wapatieni Madaktari na wauguzi vifaa vya kujikinga, Huo mnaofanya ni uzembe unaomaliza maisha ya watanzania, Daktari anasomeshwa kwa gharama kubwa na wapo wachache, mnashindwa kuwapatia PPE za elfu 70 tu, mnaona heri wafe?

Wakifa hao na ninyi mtasaidiwa na nani? Hebu kuweni serious, mnachojua ni kukamata na kufungulia kesi wasio na hatia.

Tunataka Magufuli urudi ukaongoze mapambano ila ubadilike....Usipobadilika Taifa litaendelea kuangamia.
 
field marshall1,
Acheni upumbavu, laughing stock ya nchi gani duniani ambayo haiangaiki na Corona?, hivi mnaangaliaga yanayoendelea duniani?, Kuna nchi ina muda wa kuicheka nchi nyingine nyakati hizi?,., Huu ugonjwa unaonyesha baadhi ya watu walivyo shallow minded.

Corona haina dawa, Indonesia raisi wao mwezi March aliwatangazia mchanganyiko wa mchaichai na majani mengine yanaing'oa Corona, Madagascar wana dawa yao wanayoiamini, bongo watu wanajifukiza Kuna watu wamepona na kuachiwa Mloganzila kwa kujifukiza na ushahidi upo.

Hiyo yote na kote duniani ni kujaribu. Kama huamini kujifukiza kaa kimya subiri WHO wakipata dawa wakutangazie. Ila mnaboa kukaa mnaongea upumbavu eti laughing stock, ya nani ambaye hajaathirika??..
 
USA taifa kubwa mnakowasabikia, walipendekeza watu wanywe klorokwin
Kwa kupotosha ujambo. Ni trump ndio alisema.. lakin wataalam wao walikataa. Ni hoax tu na hwakuitumia hiyo dawa sababu mamlaka husika walikataa.
( kwa mfumo wa utawala wao.. mamkaka za kiserikal zinaweza kumgomea rais kwenye jambo fulani.)

Lakin wanalifanyia uchunguzi hilo suala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Watanzania tunaweza kufanya lolote lile litakalo tupa imani ya kuishi maisha marefu. Hata kama ni la uongo au kufikirika.

Mbona watanzania kibao tu na wengine picha zao zipo humu mpaka leo, walienda mpaka Loliondo kunywa kikombe cha babu miaka ile huku wakiwa hata hawajui wanaumwa nini.
 
field marshall1,

Wewe inaonekana una ufinyu wa kufikiri, hakuna Nchi inayocheka wenzie kipindi hichi cha Corona, watu wanafukuzia kwa kutumia dawa za asili na wanapona, we endelea kukalia mitandaoni ili mradi uonekane unachangia kwa vitu usivyohelewa.

Nasikitika kuona watanzania wengi wana ufinyu wa kifikra, wamekalia utandawazi wanasahau mila na desturi za kitanzania.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa Watanzania tunaweza kufanya lolote lile litakalo tupa imani ya kuishi maisha marefu. Hata kama ni la uongo au kufikirika.

Mbona watanzania kibao tu na wengine picha zao zipo humu mpaka leo, walienda mpaka Loliondo kunywa kikombe cha babu miaka ile huku wakiwa hata hawajui wanaumwa nini.
Taja mmoja aliyeenda Loliondo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Please be patient.
We have been warning people about MATAGA's mindset and Lumumba sycophants but kept ignoring our alert. So now you are reaping what you deserve.
 
Wakuuu, kulitokea promo kubwa sana juu ya maombi, wale wachungaji wa kilokole wakajiona mabonge ya watu, wakaonekana masupa star.

Lakini cha ajabu naona kama wameanza kusalitiwa na sasa ngoma inaenda kwenye waganga wa kienyeji.

Naona leo wameanza kuibuka na majani kila aina daaah Tanzania tumepatikana kwakweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kupotosha ujambo. Ni trump ndio alisema.. lakin wataalam wao walikataa. Ni hoax tu na hwakuitumia hiyo dawa sababu mamlaka husika walikataa.
( kwa mfumo wa utawala wao.. mamkaka za kiserikal zinaweza kumgomea rais kwenye jambo fulani.)

Lakin wanalifanyia uchunguzi hilo suala.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uhakika na unachoandika?
 
Mkuu samahani, wewe ukiamua kuchuma majani ya muarobaini hapo au alovera ukanywa hapo tayari utakuwa ni mganga!!?
 
Afrika tunawekeza kwenye nyungu![emoji2211][emoji2211][emoji2211] Taifa ambalo haliwekezi kwenye tafiti, sayansi na technologia ni Taifa mfu
 
Afrika tunawekeza kwenye nyungu![emoji2211][emoji2211][emoji2211] Taifa ambalo haliwekezi kwenye tafiti, sayansi na technologia ni Taifa mfu
Siku mkiona akina Pompeo wameshuka kuja kuchukua nyungu sijui mtasemaje!?
 
Back
Top Bottom