msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 929
- 1,764
Mheshimiwa Rais alisema mawaziri wakileta vitu ambavyo havieleweki tuwakosoe. Kwa misingi hiyo naomba nitumie jukwaa hili kumkosoa waziri ummy mwalimu.
Jana kwenye press conference na waandishi wa habari waziri ummy alionyesha masikitiko makubwa juu ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea. Ummy alitolea mfano wakurugenzi wa halmashauri ya kilindi, same na uvinza kwamba anatamani angeitisha mkutano wa hadhara ili wananchi wawazomee kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.
Ni sahihi dada ummy kukemea tabia hiyo hata mimi nakupongeza kwa sababu tabia ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea inachochea uzembe na ucheleweshaji wa maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.
Lakini itakumbukwa ni takribani wiki ya tatu sasa tangu mheshimiwa Rais aagize wizara ya tamisemi chini ya ummy mwalimu kuajiri haraka walimu 6000 kwaajili ya replacement ila tangu agizo hilo litolewe, waziri Ummy hajatokeza mahali popote kutolea ufafanuzi wa ajira hizo na kinachoendelea.
Je kitendo hicho cha kupuuzia agizo hilo la mheshimiwa Rais, dada ummy huoni kwamba na wewe ni sehemu ya watendaji wanaofanya kazi kwa mazoea..?