Waziri Ummy acha kuwasakama wakurugenzi wako. Hata wewe unafanya kazi kwa mazoea

Waziri Ummy nenda taratibu dada kutumbuatumbua tu eti kisa madiwani wamemlalamikia mkurugenzi au watu fulani tu wamekupa taarifa kuwa kuna ubadhirifu siyo sahihi hata kidogo.Kabla ya kuchukua uamuzi wa kutumbua jiridhishe kwanza kwa kufanya uchunguzi na najua Serikali ina vyombo vingi vinavyoweza kufanikisha hili ili haki itendeke.Watanzania huwa hatutakiani mema, mtu anaweza tengenezewa zengwe tu atolewe kisa amezuia ulaji wa watu.
 
Mheshimiwa Rais alisema mawaziri wakileta vitu ambavyo havieleweki tuwakosoe. Kwa misingi hiyo naomba nitumie jukwaa hili kumkosoa waziri ummy mwalimu.

Jana kwenye press conference na waandishi wa habari waziri ummy alionyesha masikitiko makubwa juu ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea. Ummy alitolea mfano wakurugenzi wa halmashauri ya kilindi, same na uvinza kwamba anatamani angeitisha mkutano wa hadhara ili wananchi wawazomee kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Ni sahihi dada ummy kukemea tabia hiyo hata mimi nakupongeza kwa sababu tabia ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea inachochea uzembe na ucheleweshaji wa maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Lakini itakumbukwa ni takribani wiki ya tatu sasa tangu mheshimiwa Rais aagize wizara ya tamisemi chini ya ummy mwalimu kuajiri haraka walimu 6000 kwaajili ya replacement ila tangu agizo hilo litolewe, waziri Ummy hajatokeza mahali popote kutolea ufafanuzi wa ajira hizo na kinachoendelea.

Je kitendo hicho cha kupuuzia agizo hilo la mheshimiwa Rais, dada ummy huoni kwamba na wewe ni sehemu ya watendaji wanaofanya kazi kwa mazoea..?
Hilo la kuhusu ajira utakuwa una mpa lawama tu ambazo sio zake!!ungekuwa unajua utaratibu wa kuajiri usingesema hivyo, labda kama una fanya makusudi tu, wizara ya utumishi ndio inayotoa kibali kwa wizara nyingine kuweza kuajiri, sasa kama utumishi hawajampa go ahead huo mchakato ataunza vipi?haya mambo sio rahisi kama tunavyofikiria jamani!!
 
Acha awasakame tu! Hawa ndiyo wanachangia maafa ya Demokrasia wakati wa Uchaguzi wa Wabunge kwa kutangaza wagombea wa CCM.
 
Kalewa sifa na upande mwingine akitaka kuonesha Mh Jaffo hajafanya kazi ya maana.

Wenye akili watajiuliza kwa nini aliondolewa Afya? Ajue kumboa Jaffo anajiboa yeye na aliye mwamini kumuweka hapo.
Kwenye Afya yeye ndiye mwanzo wa kudorora kwa MSD aliyokuwa anaisimamia. Aliendekeza kulala kingono na BWANAKUNU aliyekuwa Mkurugenzi wa MSD. Huku wakigawana rushwa za tenda ya madawa kutoka Bahari Pharmacy.

BWANAKUNU yuko Segerea akisubiri hatma yake ya kutakatisha fedha, ni ajabu Ummy Mwalimu anahamishwa Wizara tu

Zahanati, hospitali hakuna dawa nayo MSD kama imefirisika maana hawana cha kupeleka vituoni
 
Acha awasakame tu! Hawa ndiyo wanachangia maafa ya Demokrasia wakati wa Uchaguzi wa Wabunge kwa kutangaza wagombea wa CCM.
Sasa ulitaka watangazwe wagombea wa chama gani kama vyama vyote vya upinzani ni mahututi ICU ? Hata 2025 mtapigwa tu na uanaharakati wenu uchwara.
 
Hujakosea mkuu..Huu ni mwaka wa saba sasa nasota mtaani na ramani bado haisomeki
Mambo yatakaa sawa tu mzee muhim uzima, Mimi mwenyewe udsm toka 2016 mpk sasa bila bila nikaamua kuivua degree nikaingia kitaa, huku mambo ni fire mpk najiuliza nilichelewa wap
 
Mkurugenzi wa jiji la TANGA sijui ni mchawi kiasi gani,madudu yaliyopo hapa ni balaa lakini kila kiongozi mkubwa anapokuja eti haoni tatizo duh!!
Mfumo mkuu, ameshiriki kwa kiwango kikubwa kumbeba Ummy toka alipokuwa mbunge vitu maalum, Mkurugenzi na meya aliyepita wamepiga pesa katika miradi yote na zimempiga tafu sana Ummy kwenye kampeni ya uchafuzi 2020. Hivyo hawezi kuguswa.
 
Tatizo ni hizo ajira 6000,ujasikia kipaumbele ni wanaojitolea ,kama hujitolei kaa mbali
 
Mheshimiwa Rais alisema mawaziri wakileta vitu ambavyo havieleweki tuwakosoe. Kwa misingi hiyo naomba nitumie jukwaa hili kumkosoa waziri ummy mwalimu.

Jana kwenye press conference na waandishi wa habari waziri ummy alionyesha masikitiko makubwa juu ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea. Ummy alitolea mfano wakurugenzi wa halmashauri ya kilindi, same na uvinza kwamba anatamani angeitisha mkutano wa hadhara ili wananchi wawazomee kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Ni sahihi dada ummy kukemea tabia hiyo hata mimi nakupongeza kwa sababu tabia ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea inachochea uzembe na ucheleweshaji wa maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Lakini itakumbukwa ni takribani wiki ya tatu sasa tangu mheshimiwa Rais aagize wizara ya tamisemi chini ya ummy mwalimu kuajiri haraka walimu 6000 kwaajili ya replacement ila tangu agizo hilo litolewe, waziri Ummy hajatokeza mahali popote kutolea ufafanuzi wa ajira hizo na kinachoendelea.

Je kitendo hicho cha kupuuzia agizo hilo la mheshimiwa Rais, dada ummy huoni kwamba na wewe ni sehemu ya watendaji wanaofanya kazi kwa mazoea..?
Ajira ni mchakato unahusisha watendaji wengi na wenye tabia ya kama hao aliowafukaza ndio wanachelewesha hizo ajira kwa hio ni jambo la kumpongeza kwani watumishi wa Serikali wamekua hawachukuliani hatua wanapokosea, kwa hatua aliyoichukua ahakikishe anachukua pia hapo wizarani na kwenye halimashauri hasa waalimu wanateseka na kujibiwa vibaya wanapoenda kufuatilia stahiki zao. SULUHISHO Waziri Ummy weka huduma nyingi online kama maddi ya madaraja,nyongeza za mishahara, uhakiki wa wafanya kazi, Utoaji wa malalamiko, ajira, ili kuepuka wafanya kazi kuonana ana kwa ana kwa sababu hapa ndio matatizo yanaanzia. Endelea Kuwajibisha wafanyakazi wazembe na wavivu na MUNGU Akulinde na Kukubariki.
 
Mkuu ,lini tutaaplai wik ya 3 sasa, au ndio mambo ya kujitolea
Sijui ummy ana mpango gani mkuu ndio maana nasema na yeye anafanya kazi kwa mazoea sababu tangu Rais atoe kibali hadi leo tulitegemea watu wawe wanatuma maombi lakini mpaka sasa hamna kinachoendelea
 
Mheshimiwa Rais alisema mawaziri wakileta vitu ambavyo havieleweki tuwakosoe. Kwa misingi hiyo naomba nitumie jukwaa hili kumkosoa waziri ummy mwalimu.

Jana kwenye press conference na waandishi wa habari waziri ummy alionyesha masikitiko makubwa juu ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea. Ummy alitolea mfano wakurugenzi wa halmashauri ya kilindi, same na uvinza kwamba anatamani angeitisha mkutano wa hadhara ili wananchi wawazomee kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Ni sahihi dada ummy kukemea tabia hiyo hata mimi nakupongeza kwa sababu tabia ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea inachochea uzembe na ucheleweshaji wa maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Lakini itakumbukwa ni takribani wiki ya tatu sasa tangu mheshimiwa Rais aagize wizara ya tamisemi chini ya ummy mwalimu kuajiri haraka walimu 6000 kwaajili ya replacement ila tangu agizo hilo litolewe, waziri Ummy hajatokeza mahali popote kutolea ufafanuzi wa ajira hizo na kinachoendelea.

Je kitendo hicho cha kupuuzia agizo hilo la mheshimiwa Rais, dada ummy huoni kwamba na wewe ni sehemu ya watendaji wanaofanya kazi kwa mazoea..?

Mmeguswa eeh???? Maana nyie watu wa hizi halmashauri mnakuwa kama mnafanya kazi kwenye serikali tofauti. Ummy anarekebisha mambo. Mnasahau mpo ili kutumikia wananchi. Sio kujilimbikizia mali kwa kutumia nafasi zenu
 
Back
Top Bottom