Waziri Ummy acha kuwasakama wakurugenzi wako. Hata wewe unafanya kazi kwa mazoea

Waziri Ummy acha kuwasakama wakurugenzi wako. Hata wewe unafanya kazi kwa mazoea

Kalewa sifa na upande mwingine akitaka kuonesha Mh Jaffo hajafanya kazi ya maana.

Wenye akili watajiuliza kwa nini aliondolewa Afya? Ajue kumbomoa Jaffo anajibomoa yeye na aliye mwamini kumuweka hapo.
 
Mkurugenzi wa jiji la TANGA sijui ni mchawi kiasi gani,madudu yaliyopo hapa ni balaa lakini kila kiongozi mkubwa anapokuja eti haoni tatizo duh!!
 
Tunamuomba asimfuatilie tu mkurugenzi wetu wa Same, DED wa Same anajitahidi sana kuifanya same iwe ya kisasa.
 
The right attitude na mipango kuyabadili organisation culture aliyoanza nayo Ummy Mwalimu akifanikiwa ata kwa 80% nadhani ataacha alama kubwa hapo.

Hila kwa jinsi anavyopenda kuchekacheka I don’t think people will take her serious.
 
Mkurugenzi wa jiji la TANGA sijui ni mchawi kiasi gani,madudu yaliyopo hapa ni balaa lakini kila kiongozi mkubwa anapokuja eti haoni tatizo duh!!
Hayo madudu yaainishe hapa viongozi wayaone bila hivyo tutaona kama una chuki binafsi tu na huyo mkurugenzi
 
Mheshimiwa Rais alisema mawaziri wakileta vitu ambavyo havieleweki tuwakosoe. Kwa misingi hiyo naomba nitumie jukwaa hili kumkosoa waziri ummy mwalimu.

Jana kwenye press conference na waandishi wa habari waziri ummy alionyesha masikitiko makubwa juu ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea. Ummy alitolea mfano wakurugenzi wa halmashauri ya kilindi, same na uvinza kwamba anatamani angeitisha mkutano wa hadhara ili wananchi wawazomee kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Ni sahihi dada ummy kukemea tabia hiyo hata mimi nakupongeza kwa sababu tabia ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea inachochea uzembe na ucheleweshaji wa maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

Lakini itakumbukwa ni takribani wiki ya tatu sasa tangu mheshimiwa Rais aagize wizara ya tamisemi chini ya ummy mwalimu kuajiri haraka walimu 6000 kwaajili ya replacement ila tangu agizo hilo litolewe, waziri Ummy hajatokeza mahali popote kutolea ufafanuzi wa ajira hizo na kinachoendelea.

Je kitendo hicho cha kupuuzia agizo hilo la mheshimiwa Rais, dada ummy huoni kwamba na wewe ni sehemu ya watendaji wanaofanya kazi kwa mazoea..?
Tanzania ina mkurugenzi moja tu wa Halmashauri, spora liana, wengine Kimeo na hawajui wafanyalo ,na hawana uwezo wa kukusanya mapato ,serikali iwafanyie utafiti kwanza kabla hawajateuluwa tena
 
Ummy yuko So primitive. Wakati bungeni wanakiri uchumi umedoda na biashara za Watu zimekufa YEYE anataka wakurugenzi wakusanye kodi Kama zamani. Huyu mama amekua roboti kabisa
 
Wawe waangalifu na hawa Wakurugenzi wasije mwaga mboga kwani wana siri kubwa ya kilichotokea uchaguzi wa 2020. Nahisi ndio maana wanakiburi kila kona waliko.🤣🤣🤣
 
Rais hawezi kukurupuka katika jambo kama hilo. Tatizo ni ummy na katibu wake ndio wanachelewesha mchakato kwa sababu wanazozijua wenyewe
Labda hawana pesa ya kuwalipa kutokana na ufinyu wa bajeti...au wanaangalia sehemu zenye uhitaji na bajeti ikianzwa kutekelezwa watu waanze kuajiliwa.. nadhani ni process.
 
Nchi yetu sote,,,, Viongozi wanapwaya sana kwenye nafasi zao
 
Mama Ummy ni kiongozi mzuri, ila inabidi abadili Approach ya kutumia mamlaka yake kuwajibisha na kuatatua matatizo sugu.

Ila kiukweli wizara ya tamisemi ni ngumu sana, watumishi wa umma wameshindikana kwa kufanya kazi kwa mazoea huku huduma mbovu.
 
Back
Top Bottom