Waziri Ummy: Bima ya Afya (NHIF) inakaribia kufa

Waziri Ummy: Bima ya Afya (NHIF) inakaribia kufa

Watumiaji wakubwa wa NHIF ni watumishi wa serikali na mashirika ya umma. Niliwahi kuuliza humu nikajibiwa kwamba wanakatwa 3% ya mshahara kama ada ya uanachama. Maana yake anayepokea milioni moja kwa mwezi atakatwa 30,000 na kwa mwaka 360,000.

Kijana wa miaka 25 anachangia zaidi ya 500,000 kwa mwaka kama si muajiriwa. Mfanyakazi anapata huduma kwa hadi watu sita. Mtu binafsi ni yeye peke yake.

Hawa wanaochangia binafsi wamepunguziwa huduma ambazo wafanyakazi na wategemezi wao wanapata pamoja na kwamba wao wanalipa zaidi ya wafanyakazi.

Hili linahitaji kuangaliwa.
Tatizo wanajilipa hela ndefu sana
Mishahara mikubwa mikubwa
Mfuko lazima ucollapse

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ipo shida katika weledi. Badala ya mfuko kuwekeza kwenye preventive wanalipia kutibu. Wangewekeza kwenye screening ingepunguza idadi ya fedha zinazotokana na matibabu
 
NHIF ina tatizo.... Moja la tatizo ni kutoa huduma sawa kwa kila mtu..

Waweke viwango vya huduma kutokana na mtu achangiavyo
Acha ujinga wako wewe
Unajua jamaa wanavyo lipana mishahara mikubwa mikubwa wewe???posho zao
Sisi huku hospital tunakula bonus kubwa hivi??wao je???

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Haaa si mutusi waziri ila ni udhaifu mkubwa saana kutoka hadharani na kunena hayo aliyoyanena... (ni siri ya ndani ilipaswa wajipambanua na kuja na hoja au mawazo mbadala) so huo umma aliouyangazaia hali ya NHIF ndio ufanye nini sasa..
Kweli serikali haijakopa huko?!
Watumishi wa bima hawana uweledi na ubunifu hilo tatizo nalo.

Serikali Ipeleke ruzuku huko kunusuru mfuko huo sasa...

Badala ya kujenga vituo vya afya kila kata na kujinadi kwamba ndio maendeleo na ili halli havina watumishi wala madawa na vifaa tiba.. hizo pesa na nguvu zingeelekezwa kutoa elimu na kuhimiza life style itakayowafanya watu wajiepushe na hayo magojwa ya NTD makampeni yakaanzia tokea shuleni na ktk jamii....

Otherwise NHIF isilalamike watoe huduma stahiki kwa wanufaika!!
 
Huu ndio ukweli, Kuna mmoja alinisimulia kinachofanyika Muhimbili nikabaki nashangaa tu. Kuna udanganyifu mkubwa usio wa kawaida.
Ndiyo tabia zenu utopolo mataga kupiga dili wizi wizi kila sehem
Kura wizi
Bima wizi
Madini wizi
Uongoz wizi
Ajira wizi
Gas wizi
Kila kitu wizi
Vijana nao wamewaiga wazee
Nao wanaiba
Dawa ni kuwa na Sheria kaliiiii ukidokoa fedha ya Uma unafilisiwa na kwenda gerezan no discussion

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tulianza tunalaumu Wakoloni, tukaja kulaumu Makaburu, baadae tukaona tulaumu Makabaila, halafu tukaanza kulaumu Wanyonyaji na Walowezi, tukaona haifai tuwalaumu Mabepari...

Ninahamu kuona siku tutakayoanza kujilaumu sisi WENYEWE.

Adui yetu ni SISI WENYEWE.
 
Sheria ya Bima ya Afya kwa wote itakuwa suluhisho la changamoto zote zinazojitokeza katika Mfumo wa bima ya Afya.
Tatizo mnajilipa mishahara mikubwa mikubwa posho nene
Kuna zile posho mnatupa huku hospital eti za kuwasaidia kuhudumia wateja wenu
Japo zinatusaidia sana lkn sio haki
Ndiyo maana mfuko una collapse

Wazir amesema mnaenda kufa je nan atawazika????



Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni moja ya mashirika yaliyoanzishwa bila upembuzi yakinifu.
Serikali ijifunze toka serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Benjamin William Mkapa.
Mkapa alianzisha kwa weledi mkubwa TANROADS na TRA ya sasa.
Tunashindwa nini kujifunza na tuna ma PhD yanaozea vichwani mwa kina Mwigulu.
Mkuu hili shirika lilianzishwa wakati wa mzee Ben just like TRA and Tanroad. Jaribu kuangalia kumbukumbu zako.
Nionavyo mimi hii organization inakufa sababu kuu ikiwa ni ‘siasa zetu mbovu’ kama kawaida yetu!
 
NHIF imeanza kutoa huduma mwaka 2001 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu baada ya kufanyika kwa upembuzi yakinifu na wa kitaalam.
Mbona leo mnataka kufa??
Mkuu ebu kuwa serious kidogo
Hapa una wasiliana na wasomi pengine wamekuzidi
Kwa nn unapenda kudanganya??

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sasa Mwigulu naye ni mtu? Yule ni kimeo
Huyu PhD yake mashaka matupu pia nadhani anshida upstairs
Ukimsikiq kwenye press kuhusu gharama za maisha hana ubinifu wowote kama waziri wa fedha

Nilimdharau na nikamshanga alipokwenda na hoja ya lutapa 3Trilioni sijui toka USAIDs kwenda kwa mashirika ya kiraisa ati pesa ziende serikali nao watazisimamia vizuri tekeleza miradi mkakati... hajua sekta binafsi ndio ametoa ajira nyingi kwa watanzania zaidi ya serikali?!

Nchi inapita pagumu saana,
 
Uongozi wa Mfuko uko imara na unayo mikakati thabiti na endelevu ya kuhakikisha Mfuko unazidi kuimarika na kutoa huduma kwa wanachama wake.
Naona una tetea ugali wako
Kwa hiyo wewe na wazir nani muongo??
Usitufanye watoto
Tumesikiliza hotuba ya wazir
Wewe unaleta uongo uongo wako hapa kama ulivo zoea kudanganya

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Dar es Salaam. Wakati mikakati ya kuboresha huduma za afya ikiendelea kuwekwa, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amebainisha dalili za kufa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutokana na kulemewa na madeni ya matibabu ya wanachama wake.

Akifungua mkutano wa siku tano wa kikanda wa kuwajengea uwezo kuhusu ugonjwa wa kipindupindu jijini hapa jana, Waziri Ummy alitaja magonjwa yasiyoambukiza ndiyo sababu kuu ya gharama kubwa.

“Kuongeza uelewa ni jambo la msingi, kwa mfano bima yetu ya afya (NHIF) inakaribia kufa kwa kuwa umeelemewa na ongezeko la madai yanayohusu NCD (magonjwa yasiyoambukiza),” alionya Ummy.

Magonjwa yasiyoambukiza yanajumuisha moyo, saratani, mfumo wa upumuaji na kisukari yanayochangia asilimia 71 ya vifo vinavyotokea duniani ambapo ni sawa na watu milioni 41 kila mwaka.

Akisisitiza kuhusu uelewa wa dalili za magonjwa na jinsi ya kujikinga nayo, Waziri Ummy alisema “fanyeni kuwa jukumu la msingi ili kuzuia kuenea kwa maambukizi, najua tutafanikiwa kupambana na kipindupindu katika nchi zetu.”

Kutokana na hali hiyo, waziri huyo ameiagiza NHIF kuachana na utaratibu iliouanzisha hivi karibuni wa kudhibiti idadi ya wagonjwa wanaohudhuria vituo vya afya.

Katika taarifa yake aliyoitoa hivi karibuni, Waziri Ummy alisema licha ya dhamira njema ya mfuko huo kuondoa uovu unaofanywa na wamiliki wa vituo vya afya, wanapaswa kukaa na wadau kukubaliana njia ya kuchukua.

Hata hivyo, bado NHIF inadai kuna udanganyifu mkubwa unaofanywa na watoa huduma kwenye vipimo kwa magonjwa.

Kamati ya Bunge

Wiki iliyopita, Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) ilisema imebaini matumizi makubwa kwenye gharama za huduma za wanachama wa NHIF, hali inayotishia uhai wa mfuko huo.

Hayo yalibainishwa baada ya kamati hiyo kujadiliana na NHIF kuhusu taarifa za uwekezaji na hesabu za mwaka wa fedha 2020/2021.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma, Jerry Silaa alisema kutokana na hali hiyo, kamati imeishauri NHIF kuandaa mkakati wa kuongeza wanachama zaidi.

“Baada ya kujadiliana tumekuja na maelekezo matatu ikiwamo kuutaka mfuko kuja na mpango wa kuongeza idadi ya wanachama kwa sababu hesabu zake zimeonyesha matumizi ni makubwa kwa maana ya malipo ya huduma za wanachama yanazidi kuongezeka ukilinganisha na mapato wanayokusanya, hii inahatarisha uhai wa mfuko,” alisema Silaa.

Mwenyekiti huyo alisema kamati imeuagiza mfuko kuwa na jitihada za makusudi za kuweka utaratibu mzuri wa kudhibiti matumizi.

Alisema wameutaka kuimarisha mifumo ya Tehama kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma sambamba na kudhibiti mianya ya udanganyifu.

Ushauri kuiokoa NIHF

Akizungumzia na Mwananchi kwa simu jana, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Shedrack Mwaibambe, alisema ili kuunusuru mfuko huo, Serikali inapaswa kupunguza wigo wa NHIF na kuanzisha mifuko mingine miwili ambayo itakayochukua watu kulingana na hali zao.

Dk Mwaibambe alisema kwa hali inavyoendelea ni wazi mfuko huo umeelemewa na idadi kubwa ya watu ambao mchango wao hauendani na huduma zinazotolewa.

Kutokana na hilo, alishauri licha ya NHIF, uanzishwe mifuko mingine itakayohudumia sekta isiyo rasmi na wasio watumishi wa umma.

“Sasa hivi wigo umeongezeka, wanachama ni wengi na ukifuatilia kwa karibu, utagundua wanaotumia zaidi huduma za matibabu ni wazee na watoto ambao matibabu yao ni ghali,” alisema.

Ukiwapo mfuko wa watumishi wa sekta binafsi watakaohudumiwa kwa utaratibu tofauti na wa sekta isiyo rasmi nao ukawahudumie wastaafu, watoto, bodaboda na watu wenye shughuli zisizo rasmi, alisema kutakuwa na ufanisi tofautina ilivyo sasa.

Dk Mwaibambe pia alishauri kuanzishwa kwa mfumo utakaomtambua mhusika anayeenda kutibiwa na kadi ya NHIF.

“Uwepo mfumo wa biometric, inaweza kuwa gharama lakini utasaidia kukabiliana na udanganyifu. Hii ina maana ili mnufaika atibiwe itatakiwa aweke kidole kujithibitisha maana kuna udanganyifu mwingi unafanyika kwenye huu mfuko,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania (Aphta), Dk Egina Makwabe, alisema ili kunusuru mfuko huo lazima Serikali iangalie upya gharama za vifurushi ili kupunguza wengi kutegemea michango ya wachache.

Dk Makwabe pia alisisitiza siasa zisiingizwe kwenye afya badala yake ukweli uwekwe wazi.

“Ukiangalia hivi vifurushi mfano cha watoto ambacho gharama yake ni Sh50,400 kwa mwaka, bado ni kidogo. Tukumbuke katika kundi ambalo linatibiwa zaidi ni watoto sasa kama anatibiwa mara nyingi gharama za matibabu zinakuwa juu, huyu lazima atatumia fedha za wachangiaji wengine, itanyonya mfuko. Nashauri waangalie hivi vifurushi na waweke udhibiti kuhakikisha hakuna udanganyifu. Kingine, Serikali iruhusu uchangiaji gharama kwa baadhi ya huduma zilizo ghali sana,” alisema.

Makwabe alisema mabadiliko ya gharama ni suala ambalo limekuwa likijadiliwa kwa miaka mingi bila kupata mwafaka na NHIF imeendelea kutumia bei za mwaka 2016 licha ya mabadiliko yaliyotokea.

“Suala la bei ni sugu, bei ambazo watoa huduma binafsi tunazozitumia na za serikalini zilitolewa mara ya mwisho mwaka 2016 sasa hivi ni mwaka 2022 ni miaka sita na bei haijawahi kubadilika. Kuna bei zimeshuka na nyingine zimepanda kutokana na maisha yalivyo,” alisema.

Alitolea mfano bei ya dawa ya panado kwamba hununuliwa kati ya Sh35 hadi Sh250 kwa kidonge kutegemea na ilikotoka lakini NHIF itamlipa mtoa huduma ni Sh20. Iwapo mtoa huduma ataitoa dawa hiyo, alisema atafanya hivyo kwa hasara na mwisho wa siku vituo vitadorora kiuchumi na kushindwa kulipa kodi hata mishahara ya wafanyakazi.

Taarifa ya NHIF

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 11 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema wametumia Sh99.09 bilioni mwaka 2021/22 kulipia magonjwa yasiyoambukiza.

Alisema kiasi hicho ni sawa na asilimia 18 ya fedha zote zilizolipwa huku dawa za saratani na huduma ya kusafishwa figo (dialysis) zikitumia fedha nyingi zaidi. Alisema magonjwa yasiyoambukiza ni mzigo mkubwa kwa mfuko huo.

Dawa za saratani zinaila zaidi NHIF. Haya ni magonjwa yanayotokana na mtindo wa maisha, kuna huduma ya kusafishwa damu kwa wagonjwa wa figo, tunatumia Sh35.4 bilioni kwa mwaka,” alisema.

Konga, alisema mpaka sasa mfuko huo una wanachama 4,831,233 sawa na asilimia nane ya Watanzania wote huku asilimia sita wakihudumiwa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) huduma nyingine za bima zikihudumia asilimia moja. Hata hivyo, alisema kuna udanganyifu mwingi unaofanywa na watoa huduma hali inayouumiza mfuko huo lakini wanapambana na hali hiyo.

“Udanganyifu upo na tumekuwa tukichukua hatua, tutasitisha mikataba itakayoonekana inahatarisha uendelevu wa mfuko. Tumekuwa tukichukua hatua ikiwamo kupiga faini, kuwaripoti wahusika katika mabaraza yao kuhakikisha tumelipia huduma halali kulingana na miongozo,” alisema Konga.

Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mashirika ya umma ya Machi 2022, inaonyesha NHIF ilipata hasara ya Sh109.71 bilioni.

Wananchi watahadharisha

Christopher Wana, mkazi wa Temeke alisema gharama za matibabu ni ghali na endepo hakutakuwa na bima Watanzania wengi watatumia mitishamba.

“Ugonjwa wowote matibabu yake yapo juu, kwa vipato vyetu hivi hatuwezi kumudu kujitibu hasa magonjwa haya ya kisukari au presha, ni muhimu kwa Serikali kuiwezesha NHIF ili huduma ziwe endelevu kwa wananchi, tukisikia mfuko umekufa maana yake wananchi ndio tumekufa,” alisema.

Naye Suzana Andrew, wanachama wa NHIF mkoani Geita alisema “hivi majuzi nilienda hospitalini lakini nikaambiwa dawa nikanunue, hali ikiendelea hivi, sisi wenye kipato cha chini tutaumia. Hakuna mbadala wa maisha, ukikosa huduma unakufa. Rais aangalie hili la NHIF kwa umakini mkubwa.”

Warda Anthony, mkazi wa Kigamboni alisema NHIF ni mkombozi wa wananchi wengi hasa wasiomudu gharama za matibabu.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi: 31-08-2022
 
Bima ya afya inasaidia sana aiseee kwa walioitumia na kunufaika nayo watanielewa.
 
Hivi Mwigulu naye kwani ni msomi mkuu??
Hii ni moja ya mashirika yaliyoanzishwa bila upembuzi yakinifu.
Serikali ijifunze toka serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Benjamin William Mkapa.
Mkapa alianzisha kwa weledi mkubwa TANROADS na TRA ya sasa.
Tunashindwa nini kujifunza na tuna ma PhD yanaozea vichwani mwa kina Mwigulu.
 
Sure mkuu
Watanzania tuwe waelewa hakuna tatizo lisilo na jibu..nature ya matatizo ya kufilisika be it kampuni, mtu binafsi, kikundi nk ni poor planning na uwezo mdogo kwenye usimamizi..! Ni mambo ya ajabu kabisa taasisi ya aina ya NHIF inaongozwa na watu wenye uwezo mdogo kiuongozi na usimamizi..

Huwezi kuwa kiongozi ikiwa umeshindwa kuona dalili za taasisi kulemewa mapema kabisa na ukashindwa kuchukua hatua kuokoa hali hiyo, lakini unasubiri kuja kulalamika hadharani kwamba taasisi imelemewa.. Ukifika hatua hiyo ni bora uondoke hapo sababu umekiri kushindwa tayari.. Bodi ya NHIF na Mkurugenzi wake hawastahili kubaki hapo tena.
 
Kati ya yote utapeli wa wabongo na wategemezi nadhani vinachangia pakubwa .
 
Back
Top Bottom