Waziri Ummy: Marufuku Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuingiza Siasa kwenye taaluma ya Uuguzi

Waziri Ummy: Marufuku Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuingiza Siasa kwenye taaluma ya Uuguzi

Wakuu wa wilaya na mikoa wako chini yake, lazima atoe tamko kuzibiti ma-RC na ma-DC kukiuka sheria na kuonea watu
Ma RC na ma Dc hawako chini yake, na wala hawawajibiki kwake. Nadhani Waziri kakurupuka tu. Watumishi wengi wa mkoani wanawajibika wizara ya Utumishi. RCs na Dcs wanawajibika kwa Rais kwani yeye ndo mteuzi wao. Rcs wanahapishwa na Rais, na DCs wanaapishwa na RCs.

Isipokuwa, baadhi ya mambo ya kiutendaji katika serikali za mitaa uhusisha ofisi za wakuu wa Mikoa na wilaya kama kupata taarifa za ulinzi na usalama. Pia bajeti za serikali za mitaa upitia ofisi ya DC na RC na kuwasilishwa TAMISEMI.

Hata huyo waziri akiwa na ziara mikoani au wilayani, hapokelewi na mkuu wa mkoa. Sana sana ni DC ndo ataambatana nae. Na bado hana maamlaka ya kumuagiza.

Sheria ya kuweka mtu ndani, labda ibadilishwe, lakini kuwatishia RCs na Dcs hapo kachemka. Kwani sheria inawapa mamlaka hayo. Ambayo hata yeye waziri hana.

Na hii ni kwasababu za kiusalama. Kwani RCs na Dcs ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na Usalama, taarifa ya Ulinzi na usalama hata huyu waziri haiendi kwake bali uenda moja kwa moja kwenye balaza la ulinzi na Usalama la Taifa, ambalo Rais kama amiri jeshi mkuu ndiye uongoza kikao hicho. Huku kukiwa na vyombo vyote vya juu vya usalama.

Kama anahitaji hiyo isifanyike wafute sheria husika. Lakini asiwaone RCs na Dcs kuwa ni watu wa chini. Wale wanamuakilisha Rais kwenye maeneo yao. Ndo maana hata ziara ya Rais mikoani, Rais uwa karibu na Mkuu wa mkoa, na taarifa ya mkoa usomewa Rais. Huyu waziri wa Tamisemi, yeye yupo kivuli tu. Hata hawezi somewa taarifa ya Mkoa na mkuu wa mkoa.

TAMISEMI japo imeundwa na mikoa na wilaya na mitaa, lakini katika uwajibikaji wa watumishi wa mkoani na wilayani ni utumishi, Tamisemi huko ni kwa taarifa.

Watumishi wa Halmashauri ndo uwajibika moja kwa moja TAMISEMI. Wakurungezi wa majiji hata wao kinidhamu ni Rais.
 
Wewe ni Kihongosi au Hapi?
Kukusaidia tuu mganga mkuu wa mkoa boss wake ni mkuu wa mkoa, na mganga mkuu wa wilaya boss wake ni mkuu wa wilaya. Hao watu ni viungo wa wizara ya afya at their local government kama ilivyo katika wizara zingine zote.

Kuna structure kabisa wizara ya afya inayotambua nafasi ya mkuu wa mkoa na mkuu wilaya kwenye kusimamia implementation ya sera za afya kwa ngazi zao.

Dr Gwajima amelalamikia sana ilo jambo, mara kadhaa amesema hao watu (wakuu wa mikoa na wilaya) wanapewa majukumu ilhali mifumo yenyewe ya usimamizi wa afya awailewi matokeo yake mganga wa mkoa na wilaya wakiwa wazembe kila kitu kinakuwa ovyo mpaka waziri ashuke kutatua; wakati mkuu wa mkoa na wilaya wapo.

Moja ya agenda zake ni kuwapa hao watu training za management skills za afya au kuja na new circumvent policy ambayo implementation zake na usimamizi azihitaji mkuu wa mkoa wala wilaya.

Ummy Mwalimu amekaa kwenye hiyo wizara hapo miaka mitano nina uhakika hafahamu ni regulation ipi inayosema ivyo. Let alone kuona mapungufu yake kama mwenzake.

Huyo dada ajikite na mambo mengine huko TAMISEMI ambapo ni pagumu bila kujiongezea mzigo mwingine. Operation za afya amuwachie Dr Gwajima au naibu wake TAMISEMI mwenye ufahamu wa sector ndio maana akawekwa. Aache kulazimisha vitu ambavyo hana skills navyo.

Tatizo lenyewe kumuelewa Dr Gwajima inabidi uilewe management ya afya vinginevyo wengi mnamuona kama anaeropoka tu, huyo mtu ni wa level zingine kwenye hiyo wizara.
Wakuu wa wilaya na mikoa wako chini yake, lazima atoe tamko kuzibiti ma-RC na ma-DC kukiuka sheria na kuonea watu
Framework and policy implementation ya wizara ya afya zinawapa roles wakuu wa mikoa na wilaya kwenye kusimamia sera; azimtambui waziri wa TAMISEMI. Jukumu lake sio la operation za wizara ya afya kuna mwenyewe anaitwa Dr Gwajima.
 
Kwa kweli baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya ni tatizo kubwa. Ni kweli baadhi yao wanaingilia taaluma siyo ya uuguzi tu, hata ya taaluma zingine. Inabidi tusome vizuri sheria zinasemaje na kuanza kuwachukulia hatua kwa kuwashtaki mahakamani wale wanao 'act arbitrarily'.
 
Nadhani hata Waziri wa Utawala Bora alishalisemea hili kuhusu wakuu wa wilaya kuacha kuweka ndani watu. Alikuwa anaongelea suala la kurudisha miiko ya utawala bora.

Nadhani sekta zote ziheshimiwe.
 
Matamko pekee haitoshi, itungwe sheria/kanuni kuwabana hao wakuu wa Wilaya/mikoa ili wasijaribu kuwaingilia watumishi wote wa serikali sio wauguzi pekee.
 
Huyo waziri Ummy anapiga siasa za kichovu na kuchekesha walionuna. Kwa taarifa yake hakuna Mkuu wa mkoa wa wilaya anamuogopa, maana wao ndio waliratibu na kusimamia uchaguzi uliowaingiza ccm madarakani. Sasa kama walijiingiza kwenye siasa, hadi yeye akawa mbunge hatimaye waziri, ni kipi atawazuia kufanya? Isitoshe huyo waziri Ummy sio aliyewateua hao wakuu wa mikoa na wilaya, hivyo hana lolote anaweza kuwafanya.
badilika rafiki!
 
Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu amesema ni marufuku kwa wanasiasa kuingilia taaluma ya Uuguzi.

Waziri Ummy amesema tabia ya Wakuu wa Mikoa au Wilaya kuwakamata Wauguzi na Madaktari na kuwaweka ndani haikubaliki kabisa na atakayethubutu kuwachezea watumishi wa afya yeye kama Boss wao atawashughulikia ipasavyo.

Waziri Ummy amesema hayo mkoani Manyara.

Chanzo: ITV habari
Hii mambo ya nita..., tuta..., wata... ipasavyo imetuchosha, huwa wanamtishia nani? Mamlaka si wanayo wanaogopa nini kushughulika mpaka watishie?
 
Well done mama tunapiga halafu tunapuliza - bado tuko kitu kimoja na mwendazake''
 
Ma RC na ma Dc hawako chini yake, na wala hawawajibiki kwake. Nadhani Waziri kakurupuka tu. Watumishi wengi wa mkoani wanawajibika wizara ya Utumishi. RCs na Dcs wanawajibika kwa Rais kwani yeye ndo mteuzi wao. Rcs wanahapishwa na Rais, na DCs wanaapishwa na RCs....
Kama kapewa maagizo na rais aliongelee hili.

Unasemaje hapo?
 
Kama kapewa maagizo na rais aliongelee hili
Unasemaje hapo?
Rais anauwezo wa kuongea na wakuu wa mikoa moja kwa moja si lazima kumtumia waziri. Na wakuu wa mikoa wakati wowote wanauwezo kuongea na Rais. Hii ni kwa mujibu wa utendaji kazi. Heri maagizo hayo apewe Waziri Mkuu, ili kuyatoa kwa RCs lakini si waziri ati awape maagizo ma RCs. Hata Rais anajua taratibu za kiutendaji.
 
Rais anauwezo wa kuongea na wakuu wa mikoa moja kwa moja si lazima kumtumia waziri. Na wakuu wa mikoa wakati wowote wanauwezo kuongea na Rais. Hii ni kwa mujibu wa utendaji kazi. Heri maagizo hayo apewe Waziri Mkuu, ili kuyatoa kwa RCs lakini si waziri ati awape maagizo ma RCs. Hata Rais anajua taratibu za kiutendaji.
Waziri amejiongeza.
 
Back
Top Bottom