Waziri Ummy: Marufuku Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuingiza Siasa kwenye taaluma ya Uuguzi

Wanasiasa tabia zao za kuchanganya taalamu na cheap popularity ndio vina li cost hili taifa kuna mambo mengi ambayo yamekuwa kero kwa vile politicians wameamua kudharau taaluma
 
Jafo aliwahi kumuombea msamaha RC Happi kwa madaktari nao wakamuelewa!
Kuomba msamaha si majukumu ya utendaji. Mtu yoyote anaweza kuomba msamaha, na msamaha haulazimishwi. Mfano hata bosi wako ukiona kafanya jambo fulani linawanyima raha wengine waweza waomba msamaha kwa niaba.

Hiyo kuomba msamaha ni kwa mtu yoyote yule ili kujenga matumaini. Tofautisha maagizo na kuomba msamaha. Kwani wakuu wa mikoa na wilaya. Sheria inawapa haki hiyo.
 
Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu amesema ni marufuku kwa wanasiasa kuingilia taaluma ya Uuguzi.

Waziri Ummy amesema tabia ya Wakuu wa Mikoa au Wilaya kuwakamata Wauguzi na Madaktari na kuwaweka ndani haikubaliki kabisa na atakayethubutu kuwachezea watumishi wa afya yeye kama Boss wao atawashughulikia ipasavyo.

Waziri Ummy amesema hayo mkoani Manyara.

Chanzo: ITV habari
Dunia inaenda kasi sana, hamna kipindi ambacho watumishi wa kada afya walidharirishwa kama kipindi Ummy akiwa waziri afya, hakuwahi kusema chochote. Nakumbuka kuna Dr huko Arusha aliitwa kutoka shambani tena akiwa off na kulazimishwa kutibu wagonjwa.
 
Wanasiasa tabia zao za kuchanganya taalamu na cheap popularity ndio vina li cost hili taifa kuna mambo mengi ambayo yamekuwa kero kwa vile politicians wameamua kudharau taaluma
Unajua katika politics kote duniani, ni kushika madaraka na kutafuta umaarufu. Hizi ndizo kusudi kubwa la siasa duniani. Ndo maana katika siasa hawajali sana elimu yako, Wanachojali je, unauwezo wa kushawishi, je umaarufu?

Kikubwa ni kuchukua au kumiliki madaraka. Wanasema ukitaka taaluma basi ajiliwa kama mtumishi wa kawaida ili uoneshe weledi wa taaluma. Hiyo ndo siasa. Ndo maana vituko vya wanasiasa haviishi duniani. Ni vichekesho, kila mtu anaibuka kivyake kwa staili yake ili kujenga umaarufu.
 
Ma RC na ma Dc hawako chini yake, na wala hawawajibiki kwake. Nadhani Waziri kakurupuka tu. Watumishi wengi wa mkoani wanawajibika wizara ya Utumishi. RCs na Dcs wanawajibika kwa Rais kwani yeye ndo mteuzi wao. Rcs wanahapishwa na Rais, na DCs wanaapishwa na RCs...
Sheria hiyo haijatoa Mamlaka uyasemayo.

Mtumishi wa Umma anawajibishwa kwa Mujibu wa Standing order.

Na hakuna Mahali standing order imeelekeza kwamba Mtumishi wa Umma akikosea atawekwa Mahabusu.

Cha Kukusaidia TAMISEMI = Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa hivyo Basi Maelekezo ya Waziri Ni Sahihi kwa Wahusika Halisi.
 
Bado Engineers Mana kila mwanasiasa ni Engineer mpaka diwani wa darasa . Ngoja kwanza tupime compressive strength ya tofali kwa kulinyanyua na kulipigiza chini
Kweli Mkuu! Wanasiasa wengine wakiona Mkandarasi anaweka Prime Coat kwenye ujenzi wa barabara wanaanza kusema Lami gani hii unaweka, vunja mkataba na mkandarasi huyu". Yaani wanasiasa wamesoma Multidiscipline Courses.
 
Sheria hiyo haijatoa Mamlaka uyasemayo.

Mtumishi wa Umma anawajibishwa kwa Mujibu wa Standing order.

Na hakuna Mahali standing order imeelekeza kwamba Mtumishi wa Umma akikosea atawekwa Mahabusu.

Cha Kukusaidia TAMISEMI = Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa hivyo Basi Maelekezo ya Waziri Ni Sahihi kwa Wahusika Halisi.
Ahsante kwa ufafanuzi murua!
 
Nadhani hata hujui sheria inayo mpa mamlaka RCs na Dcs kumweka mtu ndani.
"Standing Order" nadhani unaitamka lakini hujui inahusika na nini kwa mtumishi wa Umma. Elewa katika utumishi wa Umma kuna sheria zinazoongoza utumishi wa Umma. Na kuna miongozo ya haki za kiutumishi. Hivyo tofautisha "Standing Order" na Sheria za utumishi wa Umma.

Standing order inatoa muongozo wa haki za kiutumishi. Lakini Sheria za utumishi wa Umma na kanuni zake za mwaka 2002, Inaeleza sheria nzima, na taratibu zote za kimaadili, utendaji na hata maelekezo ya kanuni za adhabu.
Hivyo usisome tu Standing order ukadhani kila kitu kimeelezwa humo. Elewa kwanza "Standing Order ni nini na inatumika wakati gani?

Kisha elewa Sheria za utumishi wa Umma na kanuni zake ni zipi na zinatumika kwenye nini?
Kuna katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo imewaelezea RCs ni nani? Na kisha Kuna sheria ya usalama, soma ujue Rcs na DCs wamepewa majukumu gani? Na utambue kuwa katika utumishi kuna utumishi wa kisiasa na utumishi wa kawaida. Je watumishi wa kisiasa wanaongozwa na sheria ipi katika uwajibishwaji wao!

Kuhusu kumwajibisha mtumishi wa umma umwajibishi kwa Standing Order bali unamwajibisha kwa Sheria za utumishi wa Umma na kanuni zake za mwaka 2002, ambayo inaeleza taratibu zote za uajibishwaji, na kutoa kanuni zake.

Unapongelea TAMISEMI naelewa kirefu chake. Ila ujue kuna miundo ya kiutumishi. Kimuundo katika utumishi maafisa wote wa Mkoani wanawajibika Wizara ya Utumishi. Nakupa mfano. Hospitali ya wilaya watumishi wake na Mganga Mkuu wa wilaya wanawajibika kwa Mkurugenzi wa halmashauri.
Lakini Mganga Mkuu wa mkoa, na manesi au wauguzi wanawajibika kwa RAS. Hata uhamisho wao wanapitishiwa kwa RAS na utumishi. Wakati Wilayani ni Mkurungezi kwa RAS na TAMISEMI.
Hiyvo Tawala za mikoa zipo ndani ya Tamisemi kwakua zinasimamia Serikali za mitaa. Lakini kimuundo wa Utumishi haziko Tamisemi moja kwa moja. Bali zinakuwa chini ya Wizara ya Utumishi. Hata wanapopandishwa vyeo inatoka moja kwa moja Utumishi. Tamisemi upokea tu nakala. RAS, ASS, Wataalamu wote mkoani, DAS, Afisa Tawala hawa wote wanakuwa chini ya Wizara ya Utumishi ndiko wanako wajibika kimuundo na si TAMISEMI.
 
Haya matamko hayana msaada wowote, zitengenezwe policy na sheria tu ndiyo muarobaini, lasivyo ni kelele tu
Mbona hata Sera na Sheria zinasiginwa pia Mkuu! hujayaona ya Covid-19 mle mjengoni Mkuu. Wabunge wanamstua Spika kuwa kuna wabunge hewa ndani ya Bunge wanakula keki kifisadi yeye anachekelea na kujipiga kifua kuwa hataweza kuwatoa.
 
Maajabu Tanzania hayaishi unakuta mwana ccm hajua a wala b kwenye taaluma ya afya halafu anamchimba biti dakatari au muuguzi.
 
Nadhani hata hujui sheria inayo mpa mamlaka RCs na Dcs kumweka mtu ndani.
"Standing Order" nadhani unaitamka lakini hujui inahusika na nini kwa mtumishi wa Umma. Elewa katika utumishi wa Umma kuna sheria zinazoongoza utumishi wa Umma. Na kuna miongozo ya haki za kiutumishi. Hivyo tofautisha "Standing Order" na Sheria za utumishi wa Umma.

Standing order inatoa muongozo wa haki za kiutumishi. Lakini Sheria za utumishi wa Umma na kanuni zake za mwaka 2002, Inaeleza sheria nzima, na taratibu zote za kimaadili, utendaji na hata maelekezo ya kanuni za adhabu.
Hivyo usisome tu Standing order ukadhani kila kitu kimeelezwa humo. Elewa kwanza "Standing Order ni nini na inatumika wakati gani?

Kisha elewa Sheria za utumishi wa Umma na kanuni zake ni zipi na zinatumika kwenye nini?
Kuna katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo imewaelezea RCs ni nani? Na kisha Kuna sheria ya usalama, soma ujue Rcs na DCs wamepewa majukumu gani? Na utambue kuwa katika utumishi kuna utumishi wa kisiasa na utumishi wa kawaida. Je watumishi wa kisiasa wanaongozwa na sheria ipi katika uwajibishwaji wao!

Kuhusu kumwajibisha mtumishi wa umma umwajibishi kwa Standing Order bali unamwajibisha kwa Sheria za utumishi wa Umma na kanuni zake za mwaka 2002, ambayo inaeleza taratibu zote za uajibishwaji, na kutoa kanuni zake.

Unapongelea TAMISEMI naelewa kirefu chake. Ila ujue kuna miundo ya kiutumishi. Kimuundo katika utumishi maafisa wote wa Mkoani wanawajibika Wizara ya Utumishi. Nakupa mfano. Hospitali ya wilaya watumishi wake na Mganga Mkuu wa wilaya wanawajibika kwa Mkurugenzi wa halmashauri.
Lakini Mganga Mkuu wa mkoa, na manesi au wauguzi wanawajibika kwa RAS. Hata uhamisho wao wanapitishiwa kwa RAS na utumishi. Wakati Wilayani ni Mkurungezi kwa RAS na TAMISEMI.
Hiyvo Tawala za mikoa zipo ndani ya Tamisemi kwakua zinasimamia Serikali za mitaa. Lakini kimuundo wa Utumishi haziko Tamisemi moja kwa moja. Bali zinakuwa chini ya Wizara ya Utumishi. Hata wanapopandishwa vyeo inatoka moja kwa moja Utumishi. Tamisemi upokea tu nakala. RAS, ASS, Wataalamu wote mkoani, DAS, Afisa Tawala hawa wote wanakuwa chini ya Wizara ya Utumishi ndiko wanako wajibika kimuundo na si TAMISEMI.
I Rest my case with You.

Ahsante kwa Kushiriki!
 
Huyo Waziri hana uwezo wa kumchukulia hatua Mkuu wa Mkoa yeyote, HANA.

Mawaziri na Wakuu wa Mikoa wote wako "pool" moja. Anaweza akashauri tu.

Aache kudemka na yeye na kubweka bweka hovyo. Kuwekwa hapo it doesn't mean yeye ni wa pekee kuliko aliyemtangulia, ni hiyo hiyo SIASA ndio imemuweka hapo. Apeleke uswahili wake huko! Ala!
Nikweli kabisa, labda akamuchongee kwa Rais.
 
Kukusaidia tuu mganga mkuu wa mkoa boss wake ni mkuu wa mkoa, na mganga mkuu wa wilaya boss wake ni mkuu wa wilaya. Hao watu ni viungo wa wizara ya afya at their local government kama ilivyo katika wizara zingine zote.

Kuna structure kabisa wizara ya afya inayotambua nafasi ya mkuu wa mkoa na mkuu wilaya kwenye kusimamia implementation ya sera za afya kwa ngazi zao.

Dr Gwajima amelalamikia sana ilo jambo, mara kadhaa amesema hao watu (wakuu wa mikoa na wilaya) wanapewa majukumu ilhali mifumo yenyewe ya usimamizi wa afya awailewi matokeo yake mganga wa mkoa na wilaya wakiwa wazembe kila kitu kinakuwa ovyo mpaka waziri ashuke kutatua; wakati mkuu wa mkoa na wilaya wapo.

Moja ya agenda zake ni kuwapa hao watu training za management skills za afya au kuja na new circumvent policy ambayo implementation zake na usimamizi azihitaji mkuu wa mkoa wala wilaya.

Ummy Mwalimu amekaa kwenye hiyo wizara hapo miaka mitano nina uhakika hafahamu ni regulation ipi inayosema ivyo. Let alone kuona mapungufu yake kama mwenzake.

Huyo dada ajikite na mambo mengine huko TAMISEMI ambapo ni pagumu bila kujiongezea mzigo mwingine. Operation za afya amuwachie Dr Gwajima au naibu wake TAMISEMI mwenye ufahamu wa sector ndio maana akawekwa. Aache kulazimisha vitu ambavyo hana skills navyo.

Tatizo lenyewe kumuelewa Dr Gwajima inabidi uilewe management ya afya vinginevyo wengi mnamuona kama anaeropoka tu, huyo mtu ni wa level zingine kwenye hiyo wizara.

Framework and policy implementation ya wizara ya afya zinawapa roles wakuu wa mikoa na wilaya kwenye kusimamia sera; azimtambui waziri wa TAMISEMI. Jukumu lake sio la operation za wizara ya afya kuna mwenyewe anaitwa Dr Gwajima.
Yeye Ummy anasimamia majengo na tools tu, lakini siyo Rasilimali watu.
 
Sheria hiyo haijatoa Mamlaka uyasemayo.

Mtumishi wa Umma anawajibishwa kwa Mujibu wa Standing order.

Na hakuna Mahali standing order imeelekeza kwamba Mtumishi wa Umma akikosea atawekwa Mahabusu.

Cha Kukusaidia TAMISEMI = Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa hivyo Basi Maelekezo ya Waziri Ni Sahihi kwa Wahusika Halisi.
Anaye wekwa ndani ni nani sasa kwa mamlaka ya mkuu wa mkoa na wilaya.
Mwananchi wa kawaida au?
 
Kweli Mkuu! Wanasiasa wengine wakiona Mkandarasi anaweka Prime Coat kwenye ujenzi wa barabara wanaanza kusema Lami gani hii unaweka, vunja mkataba na mkandarasi huyu". Yaani wanasiasa wamesoma Multidiscipline Courses.
Ila kazi yake ama mtaji wake ni illiterate ya cheap popularity ya wananchi wajinga Kama mie na mwingine Mana sijakufahamu
 
Back
Top Bottom