Wakuu wa wilaya na mikoa wako chini yake, lazima atoe tamko kuzibiti ma-RC na ma-DC kukiuka sheria na kuonea watu
Ma RC na ma Dc hawako chini yake, na wala hawawajibiki kwake. Nadhani Waziri kakurupuka tu. Watumishi wengi wa mkoani wanawajibika wizara ya Utumishi. RCs na Dcs wanawajibika kwa Rais kwani yeye ndo mteuzi wao. Rcs wanahapishwa na Rais, na DCs wanaapishwa na RCs.
Isipokuwa, baadhi ya mambo ya kiutendaji katika serikali za mitaa uhusisha ofisi za wakuu wa Mikoa na wilaya kama kupata taarifa za ulinzi na usalama. Pia bajeti za serikali za mitaa upitia ofisi ya DC na RC na kuwasilishwa TAMISEMI.
Hata huyo waziri akiwa na ziara mikoani au wilayani, hapokelewi na mkuu wa mkoa. Sana sana ni DC ndo ataambatana nae. Na bado hana maamlaka ya kumuagiza.
Sheria ya kuweka mtu ndani, labda ibadilishwe, lakini kuwatishia RCs na Dcs hapo kachemka. Kwani sheria inawapa mamlaka hayo. Ambayo hata yeye waziri hana.
Na hii ni kwasababu za kiusalama. Kwani RCs na Dcs ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na Usalama, taarifa ya Ulinzi na usalama hata huyu waziri haiendi kwake bali uenda moja kwa moja kwenye balaza la ulinzi na Usalama la Taifa, ambalo Rais kama amiri jeshi mkuu ndiye uongoza kikao hicho. Huku kukiwa na vyombo vyote vya juu vya usalama.
Kama anahitaji hiyo isifanyike wafute sheria husika. Lakini asiwaone RCs na Dcs kuwa ni watu wa chini. Wale wanamuakilisha Rais kwenye maeneo yao. Ndo maana hata ziara ya Rais mikoani, Rais uwa karibu na Mkuu wa mkoa, na taarifa ya mkoa usomewa Rais. Huyu waziri wa Tamisemi, yeye yupo kivuli tu. Hata hawezi somewa taarifa ya Mkoa na mkuu wa mkoa.
TAMISEMI japo imeundwa na mikoa na wilaya na mitaa, lakini katika uwajibikaji wa watumishi wa mkoani na wilayani ni utumishi, Tamisemi huko ni kwa taarifa.
Watumishi wa Halmashauri ndo uwajibika moja kwa moja TAMISEMI. Wakurungezi wa majiji hata wao kinidhamu ni Rais.