Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Ukizingatia Ijumaa ya leo kuna ibada mbili zikusanyazo idadi kubwa ya waumini...

Ibada ya Ijumaa kuu...

Ibada ya kila Ijumaa kwa waumini wa kiislaam...



Cc: mahondaw
 
Hii nchi hii?unazuia msongamano kwa kufunga shule then makanisa yanaendelea tu,umy mbona mnacheza na afya za watanzania?
 
Enewei bado tuna muda kidogo, kama lockdown ya nchi nzima itasababisha tatizo kubwa kuliko tatizo la ugonjwa wenyewe, basi ifanyike lockdown ya mkoa kwa mkoa, kusiwe na muingiliano wa watu kutoka mko mmoja kwenda mwingine ili wananchi waendelee shughuli zao za kila siku huku wakichukua tahadhari zilizotolewa na mamlaka husika. Tuwena huruma ya kibinadamu angalau kwa wale wenye matatizo mengine ya afya pamoja na wazee wetu. Be humble, don't be the source of harm and don't harm your fellow human being 🙏🏽
 
Hawa kuna kitu wanatuficha hasa kwenye takwimu za walioambukizwa huu ugonjwa nchini. Ngoja ngoma isambae watafichua wenyewe.
Waziri ameeleza kile anachokijua.....
ww kama kuna jambo unaona limefichwa fichua
 

Kwamba rais kasema hakuna kufunga kazi na Ummy kakubali. Sasa wanalia lia nini?

Nini hawakuambiwa?

Kwa nini Ummy hakumwachia rais uwaziri wake kama ni shinikizo lake kuwa kazi zisisimame hata kama sote tufe?

Nani anayeongoza hii vita ambaye:

1. Kashindwa kuwa wa msaada ugonjwa usiingie.
2. Kashindwa pia kuudhibiti ugonjwa isisambae.

Anayo mawazo ya kuuzuia usisambae au yupo yupo tu kamwachia Mungu?

Muda wa kupata majibu ni sasa.
 
Mzee hizi issue za immunity nazijua sana mkuu

Nmesoma miaka mitano nikaadd mingine saba mzee

Ngoja bhana tuone [emoji38]
No, they are affected but they have strong immunity to resist the disease. Hizo ndio zilikuwa speculation zao. By the way, ngoja tuone itakuwaje!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kauli hizi watanzania tujiandae kisaikolojia chochote chaweza tokea, na tusubiri hizo siku chache zijazo tamko gani laja sanjari na uvaaji wa barakoa pindi watu watokapo majumbani
 
Kadri hizi habari zinavotoka naanza kuziona dalili mbaya najiona kabisa muda mfupi ujao nabeba kila kilicho cha muhimu narudi zangu kijijini hadi pale hill janga litakapokuwa limepita. Allah tuepushe
Unataka kuwapelekea korona kijijini acha hizo
 
Ukitaka kujua kama wanaficha au wanasema ukweli, ebu fanya kautafiti kadogo mtaani kwako. Wameugua wangapi hapo? Wamekufa wangapi hapo? Kama hawapo mtaani kwako wa mtaa wa nani? Ufipa?
Huu ujinga ndio mnaoutegemea kuwalaza akili watu.

Hebu eleza kama Tanzania nzima wakifa watu mia mbili kwa siku, kutokana na sababu yoyote ile, kama utajua hapo ulipo kuwa hao watu wamefariki siku hiyo?

Hata serikali yenyewe haina takwimu hizo!

Na huo ndio usingizi wa pono unaokulaza wewe.
 
Kwa tangazo la waziri jana.. kuna ulazima wa dar kufungwa.

Watu wasitoke na wala mtu asiingie kama wachina walivyo fanya wuhan.


Pia viongizi wote wanatakiwa kupimwa corona mapema wabunge, mawaziri, etc.


Madaktari wote na wahudumu wa afya wanatakiwa kupimwa kila siku.


Wengi wanaona dalili sio nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…