Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Hamna jema..
Sasa hivi itakuwa inatangazwa waliorecover tu. Ukisikia mgonjwa ni mmoja ama wawili.

Baada ya ile idadi 89 kutangazwa na watu kuanza kumshambulia rais akashtuka na ndiyo lengo LA mkutano wake wa juzi kupiga biti.

Haya yote hayaondoi kasi ya maambukizi na vifo hata serikali ikiendelea kuficha uhalisia. Na hii ni kwa sababu hakuna jipya linalofanywa kuthibiti maambukizi.

Hivyo ni swala la kila RAIA kujipambania..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ya ajabu sana hii kuwahi kutokea..

Me nadhani wananchi ndio wenye nchi hivyo wapewe updates zote zinazohusu huu Ugonjwa bila hivyo ni utumiaji m'baya wa madaraka..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rafiki yangu aligundulika ana corona siku 7 zilizopita ila hali yake kwa sasa ni njema kabisa,hana dalili zozote za ugonjwa japokuwa bado yupo hospitali na vipimo vya kuthibitisha kupona bado havijachukuliwa.Ila yupo fit nashukuru mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesema tuwe na kiwango cha ujinga,kikizidi ni tatizo!Kwahiyo unaamini kabisa wamefukizwa hospitalini ndio maana wamepona?So juzi Rais kaongea,Jana wakafukizwa na leo wamepona na kuachiwa,akili zenu mnazijua wenyewe!
Maneno mengi uelewa mdogo, nilichoandika hujaelewa sasa unakuja na litmus test za akili zetu, sijui zangu na za nani.
Kufukiza ni medical treatment ipo, usivurugwe na hilo neno la Kiswahili. Ikiitwa humidifier, nebulizer vipi?!
 
Kafuata ushauri wa Rais, sasa angetoa taarifa iliyokamilika zaidi; maambukizi mapya kama wapo ataje idadi, vifo kama vipo, then na hao waliopona.

Ila huo ushauri wa bosi wake nao ni kama mtego, wasije sema wamepona wengi ili wamfurahishe jamaa, kumbe ukweli ni kinyume chake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waziri alitakiwa awe na standard format ya kutolea hizi taarifa. Kitaalamu ni muhimu kueleza wagonjwa wapya ni wangapi hata kama hakuna kwa wakati huo.

Hiki ndio kipimo kikubwa cha jinsi ugonjwa unavyo endelea nchini. Taarifa ya vifo ni muhimu pia. Karantini wako wangapi ni indicator nyingine muhimu pamoja na waliopona. Kutokutoa taarifa muhimu ni sawa na kupotosha umma.
 
Pierre baada ya kutoloka Amana [emoji54]
Screenshot_2020-04-24-17-33-35-1.jpg
 
Magufuli alisema wamepona 100 mbona waziri kasema wamepona 37 na sio 100!! Tumuamini nani kati yao?
Mkuu ungesema wewe hivyo ungeambiwa unapika data, unapotosha umma nani mchochezi. Wakubwa hawadanganyi yaani si waongo bali hukosea. Wewe na mimi ndio waongo na .......
 
Maneno mengi uelewa mdogo, nilichoandika hujaelewa sasa unakuja na litmus test za akili zetu, sijui zangu na za nani.
Kufukiza ni medical treatment ipo, usivurugwe na hilo neno la Kiswahili. Ikiitwa humidifier, nebulizer vipi?!
Wewe umedakia mambo kwa juu juu tu!Ushauri wa kidaktari uliotolewa ni kuwa kufukiza moshi wa joto sio sahihi!Hakuna anayeweza kuhimili hewa ya 100 °C iingie kwenye pua zake ili zikaue virus kwenye mapafu!Tumia akili!

Ushauri wa kidaktari so far ni kula mlo kamili pamoja na matunda kuuoa mwili uwezo wa kupambana!Sasa ninyi mnakuja na bla blah zisizo na maana hapa!
 
Mkuu, kiwango cha ujinga kilichoruhusiwa na TBS ni kiasi gani? Natania🥰😀😀
Ujinga usizidi 10%!Sasa ikiwa balanced 50% hapo ndio tunaona matatizo kama ya huyo mchangiaji!
Natania tu!
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi sasa jumla ya Wagonjwa waliopona ni 48 ambao ni kati ya Wagonjwa 108 waliothibitika kuwa na Ugonjwa huo, ila kwa sasa hawana dalili

Amesma, "Tuna vifo 10, na hivyo tukabakiwa na wagonjwa 274 na kati ya 11 tumeshawatolea taarifa kuwa wamepona. Ni kweli kama alivyosema Rais Magufuli katika watu 263 waliobaki, 108 hawana ugonjwa wowote"

Ameongeza, "Watua hao 108, hawana homa, kifua, kikohozi wala chochote, ila tuliwazuia katika vitua ili kusubiri vipimo vya mwisho na kuthibitisha kama hawana maambukizi kabla ya kuwaruhusu kwenda nyumbani."

Amesema leo wameruhusu watu 37, na kuwa vipimo vyao vimeonesha hawana maambukizi ya #COVID19. Ametoa wito kwa jamii kuwa isiwanyanyapae na kuongeza kuwa wengine 71 vipimo vyao vinasubiri siku 2-3 wataruhusiwa kurudi nyumbani
Taarifa za kumfurahisha Mchato zimeanza kutoka
 
Kumbe ni kweli rais wetu alikuwa sahihi na wataalam wetu walikuwa ama wrong au walikuwa bado wana hakiki uponaji wa wagonjwa.....Unajibu maombi×3 twakushukuu baba🎼🎼 Ewe Mungu tusaidie iwe ni kweli.
 
Wewe umedakia mambo kwa juu juu tu!Ushauri wa kidaktari uliotolewa ni kuwa kufukiza moshi wa joto sio sahihi!Hakuna anayeweza kuhimili hewa ya 100 °C iingie kwenye pua zake ili zikaue virus kwenye mapafu!Tumia akili!Ushauri wa kidaktari so far ni kula mlo kamili pamoja na matunda kuuoa mwili uwezo wa kupambana!Sasa ninyi mnakuja na bla blah zisizo na maana hapa!
Una uhakika na wewe hukurukia mambo juu juu na vipimo vyako vya akili?! Kwenye eneo hili uelewa wangu naamini si haba. Acha mass judgements.
 
Back
Top Bottom