Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Mdau kuelezea kuhusu mchakato wa kubomoa nyumba zaidi ya 100 zilizopo Mapinga Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani, Serikali imechukua hatua ya kusitisha mchakato huo, malalamiko ya awali soma hapa ~ Nyumba zaidi ya 400 za Mapinga (Bagamoyo) kuwekewa X ili zivunjwe kuna harufu yenye shaka, Waziri Silaa fuatilia kinachoendelea
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ameingilia kati mgogoro wa ardhi uliozua taharuki katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani kati ya wananchi zaidi ya 100 na mtu mmoja ambaye aliyejulikana kwa majina ya Sevestine Mtunga ambaye anadai kumiliki eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 12 baada ya Mahakama kuwataka wananchi hao kuondoka eneo hilo.
Waziri Silaa ameelekeza zoezi hilo lisimame kwanza na kumuomba mwakilishi wa Sevestin Mtunga ampe muda ili Serikali iweze kulifanyia kazi swala hilo na kuondoa taharuki kwa wananchi kama maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumwelekeza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bi Halima Okash kukutana na pande zote kuanzia Jumanne 18 Juni 2024.