Watu tunaweza Ku comment kirahisi sana kwa kuwa hatuko kwenye position ya hao watu 100 ambao familia zao zitakosa makazi. Siamini kama hao watu kila mtu alijijia tu akajenga. Ni lazima waliuziwa. May be na matapeli kama ni kweli kiwanja cha huyo alieshinda kesi.
Kibinadamu tu, unawezaje kumbomolea mwenzio nyumba iliyomgharimu mamilioni tena usikute ya mkopo kisa ardhi mali yako. Nafikiri ni vyema serikali ingekaa na pande zote ili waone kila upande unanufaikaje.
Kiukweli Mimi sina hiyo nyumba ila nafeel maumivu wanayopitia hawa watu. Dunia tunapita. Imenikumbusha kipindi watu wanabomolewa kwa kuvamia eneo la yule mama mchungaji, aisee kuna baba anatoka job anakuta vyombo na familia wako nje, nyumba ishaanguka, alianguka na kupoteza fahamu, kuja kuzinduka ni machozi. Mwanaume kulia si jambo dogo. Leo hii mama mchungaji yuko ndani ya ardhi, ardhi na vilivyoko juu yake kaviacha. Kweli ilikuwa ni mali yake, ila asingepungukiwa kuwaachia wale maskini kisehemu tu katika eneo kubwa alilonalo, mbaya zaidi wao walitapeliwa na walikuwa tayari kumlipa vile viwanja.