Waziri wa Ardhi azuia mchakato wa kutaka kubomoa nyumba zaidi ya 100 zilizopo Mapinga

Waziri wa Ardhi azuia mchakato wa kutaka kubomoa nyumba zaidi ya 100 zilizopo Mapinga

Katiba inasema ardhi ni mali ya serikali, mwananchi ni mpangaji tu, waziri ndiye mwenye dhamana ya ardhi, hapo unaonaje? Ahakikishe kuwa hapakuwa na hata chembe ya rushwa.
Kwanza katiba inasema ardhi ni mali ya umma
Na katiba inasema : Mahakama ni moja ya mhimili wa umma, haitakiwi iingiliwe kwenye uamuzi wake....
Kama mtu hajaridhika na maamuzi ni akakate rufaa katika mahakama ya Juu...

Kuchunguza rushes mahakamani siyo kazi ya Waziri.
 
Watu tunaweza Ku comment kirahisi sana kwa kuwa hatuko kwenye position ya hao watu 100 ambao familia zao zitakosa makazi. Siamini kama hao watu kila mtu alijijia tu akajenga. Ni lazima waliuziwa. May be na matapeli kama ni kweli kiwanja cha huyo alieshinda kesi.
Kibinadamu tu, unawezaje kumbomolea mwenzio nyumba iliyomgharimu mamilioni tena usikute ya mkopo kisa ardhi mali yako. Nafikiri ni vyema serikali ingekaa na pande zote ili waone kila upande unanufaikaje.

Kiukweli Mimi sina hiyo nyumba ila nafeel maumivu wanayopitia hawa watu. Dunia tunapita. Imenikumbusha kipindi watu wanabomolewa kwa kuvamia eneo la yule mama mchungaji, aisee kuna baba anatoka job anakuta vyombo na familia wako nje, nyumba ishaanguka, alianguka na kupoteza fahamu, kuja kuzinduka ni machozi. Mwanaume kulia si jambo dogo. Leo hii mama mchungaji yuko ndani ya ardhi, ardhi na vilivyoko juu yake kaviacha. Kweli ilikuwa ni mali yake, ila asingepungukiwa kuwaachia wale maskini kisehemu tu katika eneo kubwa alilonalo, mbaya zaidi wao walitapeliwa na walikuwa tayari kumlipa vile viwanja.
Unaweza ona huruma...
Ila kama walivamia eneo la mtu ,sheria ifuatwe.....

Tatizo ndani ya hii nchi ,watu tunadhani tunaweza jenga kila sehemu, mwishowe haya ndiyo yanatukuta.
 
Mimi nazani hao hao wenye viwanja ndio hua wa panga mpango na wenyeviti. Kuwatapeli wananchi. Kwaakili yakawaida nyumba aiyoti kama uyoga
Kuna mazingira una kuta hata mwenye kiwanja hajui, kinachoendelea labda yupo mbali, anakuja tapeli anakiuza hicho kiwanja, tena anapata back up ya uongozi wa eneo kuwa ndio mwenye kiwanja halisi na wanaandika hati!! Unajenga maisha yanaendelea, ndipo anaibuka mwenye mali halisi!! Mwenye kiwanja akikiuza kiwanja mala mbili ni rahisi ku deal naye, kuliko unapouziwa na tapeli
 
Kwanza katiba inasema ardhi ni mali ya umma
Na katiba inasema : Mahakama ni moja ya mhimili wa umma, haitakiwi iingiliwe kwenye uamuzi wake....
Kama mtu hajaridhika na maamuzi ni akakate rufaa katika mahakama ya Juu...

Kuchunguza rushes mahakamani siyo kazi ya Waziri.
Ni sawa ila kuna mazingira mengine lazima busara lazima itumike!! Wewe una eneo lako, umeliacha watu wamejenga hadi nyumba zimefikia 500,watu wanaishi, ndipo unakuja kuibuka kuwa eneo ni lako, na kweli kisheria ni lako lakini hawa watu wote wakati wanajenga ulikuwa wapi??! Kinachofanyika ni hao watu kukulipa kulingana na kila mmoja na ukubwa wa kiwanja chake, tu.
 
Wakae waongee kwa mamlaka ipi wakati uamuzi ulishatolewa.....🤣🤣🤣
Kwahyo ili aje na uamuzi mwingine...
Hukumu inaweza kutolewa na watu wakaongea na kutengeneza settlement deed/deed of settlement. Ikakubaliwa na mahakama na ikawa registered.
Bila kutumia waziri au mjumbe wa nyumba kumi, just lawyers to draft it.
Hujui hilo?
 
Hajatengua hukumu, bali ameahirisha utekelezaji ili wakae waongee waone kama kunaweza kuwa na nusura.
Yeye ni sehemu ya utekelezaji (execution) mahakama haitekelezi, kwa hiyo muwe na subra.
kisheria naruhusiwa kufanya hivyo? lakini hapo inaonekana yeye sio mtekelezaji wka sababu sio mvamizi
 
kisheria naruhusiwa kufanya hivyo? lakini hapo inaonekana yeye sio mtekelezaji wka sababu sio mvamizi
Waziri = wizara= Rais = Executive ( vrb. Execution).
Unaruhusiwa mradi wote muwe watu wazima wenye akili timamu bila shuruti. Hukumu ni kwamba inakupa upperhand ili mtu mbishi akitaka aje kukupigia magoti na wewe ukikubali basi hamna noma.
 
Sijaelewa vizuri mkuu ina maana hao uliowataja wapo juu ya sheria?
 
Back
Top Bottom