Waziri wa Ardhi azuia mchakato wa kutaka kubomoa nyumba zaidi ya 100 zilizopo Mapinga

Oops !! Hili Bhalaa Kubwa Sana Sana
 
Mamlaka ya Rais kwenye Ardhi yakoje!?
 


Kunapokuwa Kuna Hukumu ya Mahakama, Mamlaka ya Waziri wa Ardhi au Kamishina wa Ardhi yanakoma katika kupangisha au kugawa au kumilikisha Ardhi hiyo kwa mtu mwingine yoyote tofauti na yule aliyeshinda Kesi (Decree Holder), unless kuwe na Makubaliano maalumu Kati ya Decree Holder na Watu hao wengine.
 
Kwanza Kwa kesi hii Waziri hajaingilia maamuzi ya Mahakama.

Pili kisheria mahakama ilikuwa inajadili nani ni mpangaji halali wa Ardhi yenye utata na mahakama haikujadili kama Waziri anayo mamlaka ya kufanya "Reallocation" kwenye Ardhi yenye utata au lah!!??
 
Kwanza Kwa kesi hii Waziri hajaingilia maamuzi ya Mahakama.
Endapo kama Waziri huyo hajasitisha zoezi la utekelezaji wa hukumu ya Mahakama (yaani hajasitisha ubomoaji wa Nyumba za Judgement Debtors wote) au Kama amekata Rufaa kupinga hukumu hiyo, basi atakuwa hajaingilia Maamuzi ya Mahakama. Lakini endapo kama ametoa maagizo kwamba zoezi la ubomoaji wa Nyumba za Judgment Debtors lisitishwe kwanza, basi atakuwa ameingilia Maamuzi ya Mahakama.
 
Nadhani kasitisha Kwa muda. Siyo maamuzi ya mahakama bali jinsi ya utekelezaji wa maamuzi hayo ya mahakama.
 
Nadhani kasitisha Kwa muda. Siyo maamuzi ya mahakama bali jinsi ya utekelezaji wa maamuzi hayo ya mahakama.
Hata kusitisha kwa muda kwa utekelezaji wa hukumu ya Mahakama, Waziri huyo anapaswa aende kufungua Maombi/Kesi ndogo Mahakamani (Stay Execution) ili kuzuia utekelezaji wa hukumu hiyo. Kutoa maagizo yoyote Yale ya kusitisha kwa muda utekelezaji wa hiyo Hukumu ya Mahakama bila ya kufungua Kesi ndogo au bila ya kukata rufaa, inahesabika ni kuingilia Maamuzi ya Mahakama
 
Na chanzo cha yote haya ni ccm kupitia viongozi wao wa serikali za mitaa!! Kwa imeshakuwa kama sheria kuwa kila ardhi isyopimwa ikiuzwa lazima wapate chao!! Likitokea la kutokea wanakimbia!! Hapo mala nyingi ni busara zaidi ndio hutumika, watu wana miaka 15,hapo na kuna nyumba zaidi ya mia, muda wote huo mlikuwa wapi walipokuwa wakijenga??
 
Ekari 12 nyumba 400!
 
Nakuelewa.
 
kama maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumwelekeza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bi Halima Okash kukutana na pande zote kuanzia Jumanne 18 Juni 2024.
HATUTAKI HISANI ya maagizo ya Rais. Tunataka sheria na mifumo ifanye kazi.

Ukikubali unusurike kwa maagizo ya Rais itabidi ukubali siku akitumia nguvu hiyo hiyo kuamuru muondoke auze eneo kwa Mwarabu.

Rais Joseph Biden wa Marekani angeweza kujifungia ndani miezi sita wala wasijue, na himaya bado ikasimama kwa sababu nchi ile inaendeshwa kwa sheria na mifumo. Na kamwe haingilii migogoro ya ardhi.

Kwanza hawana migogoro ya ardhi, nchi ishapimwa. Na bahari yao pia ishapimwa, kila bonde na mwamba na barafu baharini, na the deepest point ndani ya Atlantic Ocean, wanajua ilipo. Sisi tumeshindwa kupima nchi kavu. Pimbi wakubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…