Waziri wa Ardhi azuia mchakato wa kutaka kubomoa nyumba zaidi ya 100 zilizopo Mapinga

Miaka hiyo walikuwepi Kina Jaji Mwalusanya. Lugakingira and the like. Tunataka majaji warudi kama wa enzi hizo

Ni kweli kabisa.

Lugakingira na Mwalusanya walikuwa kimbilio letu.

Sasa Lugakingira na Mwalusanya wamekufa. Tukakwama tena!

Amekuja Paulo Makonda, amekuja Jerry Slaa. Ndio nikauliza, na Slaa akifa na Makonda akifa itakuaje ??????? Na huyo Mama aliyetoa agizo kwa Waziri, na yeye akifa ?

Mwafrika hapo anakwambia unaleta nuksi, unawachulia wenzio kifo. Mwafrika hawazi kwamba hata Rais anaweza kufa. Hata kama yamemtokea, hajifunzi, kichwa kizito.

Haya, hawafi. Vipi kama ni corrupt? Rais corrupt, anaagiza mema Bagamoyo kujikosha, kuwahadaa wanyonge wasio na elimu, lakini anauza Longido kwa Mwarabu. Tunafanyaje ?

Tujenge mifumo!
 
Mimi nazani hao hao wenye viwanja ndio hua wa panga mpango na wenyeviti. Kuwatapeli wananchi. Kwaakili yakawaida nyumba aiyoti kama uyoga
 
Waziri piga kazi.mahakama za tz ni uchafu mtupu.zinapendelea watu wenye pesa tu.mahakama zetu uchwara zinanuka rushwa.
 

..jamaa aliyeshinda kesi atafutiwe eneo lingine na serikali ili kuwanusuru hao wavamizi.
 
Kisheria hii imekaaje? Watu wamevamia, wamepelekwa mahakamani na wameshindwa, waziri anakuja kusitisha how?
Busara itumike .. hadi nyumba 100 zinajengwa mwenye ardhi ulikuwa wapi ?
 
Tena kwa kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa... Kura moja vs kura 300 .. huyu mama aliyeshinda awe na uchungu basi aingie na huruma nyumba 100 ni nyingi sana .. atazikwa ataacha hiyo ardhi
 
Tena kwa kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa... Kura moja vs kura 300 .. huyu mama aliyeshinda awe na uchungu basi aingie na huruma nyumba 100 ni nyingi sana .. atazikwa ataacha hiyo ardhi
Umenena vyema Mkuu Kuna member anaitwa ras jeff kapita anapambana na Mimi Kwa matusi tu kisa kumuunga mkono Slaa😄😄Ardhi tutaiacha jamani tuwe na huruma.
 
Hapana mimi ni mume pia nina maslahi ya kuibutuo zero yako kama nilivyoibutua jana
Upo kwenye siku zako wewe au unatafuta mabwana hapa?acha kushobekea wanaume wenzio.Sasa mwambie huyo landlord wako tumepiga stop na hakuna kitu atafanya.
 
Ingekuwa Mimi ndiyo nimeshinda kesi,ningezibomoa halafu nione kifuatacho ITV.

BTW:LHRC huwezi kuwasikia kwenye hili labda angekuw Makonda.
Unakuta mmiliki naye anajua alipitia michakato michafu hivyo amasitasita licha ya kushinda kesi. Nyumba zaidi ya 80 hiyo issue sio mchezo unazungumzia watu 16 (mke na mume watoto excluded) na assume kila nyumba ina mke na mume. Ni serikali ya kijinga tu inaeeza kukaa kimya na isotie neno
 
Ukweli usemwe....
Mahakama imekuwa kichinjio cha haki kwa baadhi ya kesi kwa miaka mingi tangu enzi za Nyerere.
Mahakama haijawahi kuwa safi kwa 100/%.
 
Hajatengua hukumu, bali ameahirisha utekelezaji ili wakae waongee waone kama kunaweza kuwa na nusura.
Yeye ni sehemu ya utekelezaji (execution) mahakama haitekelezi, kwa hiyo muwe na subra.
 
Mapinga Bagamoyo ni sehemu yenye utapeli mkubwa sana wa ardhi.

Pata picha umenunua eneo lako na una hati au document zote halali, wanakuja matapeli (Mmoja maarufu kule anaitwa Mwanahamisi) anawauzia watu kitapeli wanajenga.

Wewe ungefanyaje?
 
Kwahiyo waziri amezuia amri ya mahakama?

Mgeni sana wewe mjini, siku hizi hati feki kibao na mnapelekwa mahakamani na mwenye hati feki anashinda kesi sbb ana fedha na mnabomolewa nyumba zenu kwa amri ya mahakama, kumbe ni fedha imetembea na mahakama ina binadamu sio malaika, majaji ni binafamu, hivyo sio kila hukumu ya mahakama imetoa haki sahihi, kuna hukumu nyingine unajua na kushuhudia haki amepewa asiye sahihi sbb ya rushwa tupu, acheni upuuzi, hamjasikia bungeni hadi Waziri Silaa kamtaja yuko Jaji mmoja anashirikiana na matapeli ya ardhi anakina Msama alafu anatoa hukumu kwa kupewa rushwa..!! Na kasema atapeleka jina lake kwa viongozi wa juu ili wamchunguze na Waziri ana ushahidi

So sio kila hukumu imetoa haki, nyingine inabidi Serikali ingalie upya kuona haki iko wapi ili ikibidi rufaa inakatwa ili kesi irudi upya mahakamani.
 
Lakini bado waziri hana mamlaka ya kuingilia uamuzi wa Mahakama....
Sheria ni msumeno.
 
Hatakama Kuwe na Rushwa ama lah, Waziri hana mamlaka ya kuingia hukumu ya mahakama....
 
Hajatengua hukumu, bali ameahirisha utekelezaji ili wakae waongee waone kama kunaweza kuwa na nusura.
Yeye ni sehemu ya utekelezaji (execution) mahakama haitekelezi, kwa hiyo muwe na subra.
Wakae waongee kwa mamlaka ipi wakati uamuzi ulishatolewa.....🤣🤣🤣
Kwahyo ili aje na uamuzi mwingine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…