Waziri wa Elimu anasimamia asichokiamini? Mwanae anasoma English Medium

Du!
 
... hiyo ndio inaitwa the ruling class Chief! Kuiondoa ili kurudisha madaraka kwa wananchi sio lelemama! Shida zaidi ni mbumbumbu waliotengenezwa makusudi "kuiabudu" the ruling class.
Jamii ikaelimika tutawatoa tu hakuna namna, hata sahivi hawaongozi kwa amani kama miaka 20 iliyopita wana pressure sn
 
Mkuu Yule jamaa ambaye ameshaenda zake kuna waziri katika Serikali yake angeweza kuwa na msuli wa Kumbishia ?
 
Mkuu Yule jamaa ambaye ameshaenda zake kuna waziri katika Serikali yake angeweza kuwa na msuli wa Kumbishia ?
... basi leo wasimame hadharani waseme walitishwa tutawasamehe kinyume chake ndio hao hao wanaendekeza upumbavu wa legacy; tuwaeleweje? Mbona Dr. Diallo kaeleza yake na waTz wamemwelewa vizuri sana?
 
Kweli Tanzania ni nchi ya ajabu kama ulivyosema ndio maana huelewi kuwa hata shule za binafsi za english medium zinasimamiwa na wizara ya elimu! Pia unaelezea watoto wa Ndalichako kusoma hizo shule za english medium kwa kudhania tu bila kuwa na uhakika ana watoto wangapi na wanasoma shule zipi lakini umeandika uzushi kuwaaminisha watu kitu usichokifahamu. Tatu unazungumzia enzi ya Nyerere miaka ya sitini, sabini na themanini wakati hakukuwepo hizo shule unazoziita english medium.

Fanya kazi ujiletee maendeleo itakusaidia kupunguza stress imayozaa chuki ambazo hazisaidii kitu.
 
Mzee... Naona umewaamulia leo[emoji23][emoji23]... Punch after punch
 
Mawaziri wote wanatakiwa watoto wao wasome shule za umma
Mtanzania yeyote mwenye pesa lazima atampeleka mwanae/ wanae shule za private ( english medium) hata wewe unayelialia humu ni kwa sababu huna hela vinginevyo wanao umgewasomesha private.

Siku zote matunzo ya watoto yanatakiwa yaakisi uwezo wa wazazi.

Ukiwa na pesa ukiugua utaenda hospitali ya private hali kadhalika na elimu ni hivyo hivyo. Kiwango cha pesa ulichonacho au unachoingiza
ndio determinant uishi wapi, utibiwe wapi na mwanao asome shule gani.

Hivyo si kosa mawaziri kusomesha watoto wao shule za binafsi.
 
Tuanze na Mtaka atuambie watoto wake wanasoma shule za wapi na nchi gani

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Haya ni mawazo mufilisi sana.... mambo ya familia ya waziri ni mambo yake binafsi. Uwaziri ni kazi yake, na watoto wake ni mambo ya familia yake yeye na mume au mke wake, wanapanga mtoto akasome wapi, sio wananchi ndio wamuamulie.

Tuache mawazo ya kishamba, tupambane kuboresha huduma za elimu ili ziwe na viwango vinavyolingana na hizo English Medium lakini sio kuwavuta watu huku chini. Uwaziri ni wa kwake, kamwe usiende kuamua familia zao zinaishi vipi.
 
Hawa wenye watoto wanaosoma canada na international school matamko yao hayajabeba uhalisia wowote kwa wadanganyika wanyonge....
 
Acha ukasuku tutajie mtoto wa Waziri anayesoma nje ya nchi au kwenye english medium.
 
Ngongo
Kuna kosa Mtanzania yeyote kusomesha watoto shule anayoipenda? Hilo sidhani kama ni kosa kwa mtu yeyote yule. Hilo ni suala la kifamilia na ni maamuzi ya kifamilia. Hayapaswi kuingiliwa.

Hoja iwe ni jinsi gani Waziri anatatua changamoto za Watanzania katika suala zima la elimu. Apigwe mawe au apeee sifa eneo hilo, na sio mambo binafsi ya kifamilia.

Hata akisomesha mtoto Harvard, it's none of our business. Our business is for the minister to do his job accordingly.

Kwa hili umekuwa unfair!
 
Kwani watoto wa Mataka wanasoma wapi?
 
Umesema Nyerere alisomesha watoto wake shule za Kayumba, sawa.

Mzee Mwinyi alisomesha watoto wake Uingereza. Mzee Jomo Kenyatta alisomesha watoto wake international school leo hii Uhuru Kenyatta ni Rais na Hussein Mwinyi ni Rais.

Watoto wa Nyerere waliosoma shule za Kayumba wameishia wapi???

Jamani acheni mawazo ya "ujima". Ukiwa Waziri au siyo waziri ili mradi tu una uwezo, somesha watoto wako hata kama ni Ulaya wapeleke wakasome, elimu ni muhimu sana kwa watoto.

Elimu yetu ya Tanzania haijitoshelezi, wote tulimwona Rais aliyepita alivyokuwa na mapungufu ya kukosa elimu ya nje. The guy had no exposure.

Waacheni wenye uwezo wasomeshe watoto wao kwenye shule za maana. Hizo za Kayumba ni zenu ninyi maskini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…