Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Huwezi kuelewa mzigo wanaobebeshwa wanafunzi wa shule za kutwa mpaka pale utakapojaribu kuubeba mfuko wa madaftari wanaobeba wakienda shuleni. Kitendo cha watoto kulazimishwa kwenda na Vitabu vya kiada na Madaftari ya Masomo yote shuleni kila siku kinawaletea wanafunzi hao matatizo kwenye uti wa mgongo.
Hivi kila shule si ina ratiba ya Masomo. Kwa nini watoto wabebeshwe mzigo wa madaftari na vitabu kwa masomo yasiyohusika kwa siku hiyo.
Kama Ratiba inaonesha kutakuwa na masomo manne ni kwa nini mtoto asibebe madaftari ya masomo hayo tu?
Miaka ijayo jamii itaingia gharama ya kutibu watu wazima chungu nzima watakaokuwa wanaumwa uti wa mgongo, chanzo kikiwa ni uzembe tu wa walimu kulazimisha watoto kubeba mzigo wa madaftari na vitabu bila ya sababu.