Waziri wa Elimu kataza wanafunzi kulazimishwa kwenda na madaftari yote shule

Waziri wa Elimu kataza wanafunzi kulazimishwa kwenda na madaftari yote shule

Namba mbili ni wazazi wenyewe kujitakia
Wala sio kujitakia.... kuna watu wapo karibu na shule nzuri zote wana huo mfumo (binafsi nna machaguo so sio ishu hata mwanangu akifika la saba wala hatoenda boarding ntatafuta tu utaratibu muda ukifika).

Kuna vitu huwa vinaanza kwa shule chache then wengine wanaiga, vitu vingine ni wizara ya elimu kuingilia kati isiwe lazima. Mzazi anaetaka mwanae akae boarding ampeleke na sisi tusiotaka tukae nao nyumbani.
Kulazimisha watoto wa primary wakae boarding ni unyanyasaji kwakweli na inachochea kulea taifa la watoto wajinga wasiovalue makuzi ya familia in the future
 
Nadhani tuliowengi humu tumesoma St.Kayumba na tunafahamu kuwa walimu ni nadra sana kufuata ratiba ya darasa mathalani unakuta mwalimu wa somo la siku husika hajafika shule hivyo itampasa mwalimu/walimu waliopo waje kuwafundisha darasani ili mradi tu isipite siku bila kufundishwa angalau somo lolote lile.
My take kwa wizara wangetengeneza LOCKER kama wenzetu Ulaya na kila mwanafunzi angekuwa na locker yake itakayoweza kuwa maalamu kwakuhifadhi vitabu na vitu vingine vya mwanafunzi.
Hii ndio solution
 
Somo kuwepo na kufundishwa ni mambo mawili tofauti. Jee maudhui ya somo lenyewe yanalingana na lengo la kumfanya mtoto awe anajitegemea na siyo tegemezi wa stadi.

Mtoto kufua tu nguo zake mwenyewe hawezi ndiyo anaweza kuwa fundi Baiskeli huyo??
Nyumba ina kijana muhitimu wa la saba 13 yrs hawezi kutunza garden ya pale nyumbani mpaka mlipe mtu. Nonsense kabisa
 
Umeongea point kubwa mno mkuu. Nilijaribu kubeba begi la kijana wangu wa darasa la 6 na utu uzima wangu lilinielemea.
Nilikwenda shule na kuhoji hili swala la kubebeshwa madaftari yote. Jibu nililipopewa ni kuwa mbali ya kuwa na ratiba, hutokea kama mwalimu wa kipindi husika hayupo basi mwingine anaingia kufidia.
Niliforce kupewa ratiba yake ya darasa na kuanza kumpa madaftari husika tu kwa kila siku, kilichotokea kila akija ana malalamiko ya kupigwa kws kutokuwa na daftari la somo kupelekea kugudundua kuwa hata huwa hawana ratiba maalum.
Wanaoumia ni watoto wanaobebesha mizigo kuliko umri wao.
 
Kwa mfano fikiria mwalimu wa somo la hisabati hayupo,na ana kipindi.
Ikabidi mwalimu mwingine wa Kiswahili akataka afundishe badala yake.
Huoni kuwa kama wasingekuwa na madaftari ya Kiswahili wangesomaje?.
 
Unajenga shule Kila kona

Ila facility zingine za kurahisisha elimu Bora hazipo mfano hizo lockers/makabati ya wanafunzi kuhifadhia vitu vyao shuleni.

Au wabuni meza za kisasa wanazotumia darasani wawekea humo baadhi ya daftari na vitabu.

Au lockers ziwe darasani au kwenye korido za madarasa
 
Nyumba ina kijana muhitimu wa la saba 13 yrs hawezi kutunza garden ya pale nyumbani mpaka mlipe mtu. Nonsense kabisa
Hapo tena, hiyo mbona kawaida sana siku hizi. Wewe unasema kijana wa Darasa la Saba, wapo wa chuo mtu anakuja kusafisha mitaro ya nyumba yao yeye yupo bize kuchat.
 
Mtoto miaka mi3 ushampeleka shule
Ukiwa mama wa nyumbani na una walezi wa uhakika huwezi ona shida kulea nyumbani... lakini familia za mama daktari baba daktari mpo daslam kazi muhimbili nyumbani kibaha.... kuliko kukaa na dada wa kazi muuaji, shule lazima ihusike mapemaaa sana (sio boarding)

Otherwise wababa wajifunge mkanda kutafuta kipato ili wamama walee watoto na kufanya kazi ndani ya masaa makazi na kuachana na overtime.

Otherwise wa mkoani tunapeta, malezi ni magumu lakini sio kama wa mjini daslam
 
Kwa mfano fikiria mwalimu wa somo la hisabati hayupo,na ana kipindi.
Ikabidi mwalimu mwingine wa Kiswahili akataka afundishe badala yake.
Huoni kuwa kama wasingekuwa na madaftari ya Kiswahili wangesomaje?.
Kwahiyo unatetea mtoto wa miaka 11 kubeba kilo mbili mgongoni kila siku??????
 
Ukiwa mama wa nyumbani na una walezi wa uhakika huwezi ona shida kulea nyumbani... lakini familia za mama daktari baba daktari mpo daslam kazi muhimbili nyumbani kibaha.... kuliko kukaa na dada wa kazi muuaji, shule lazima ihusike mapemaaa sana (sio boarding)

Otherwise wababa wajifunge mkanda kutafuta kipato ili wamama walee watoto na kufanya kazi ndani ya masaa makazi na kuachana na overtime.

Otherwise wa mkoani tunapeta, malezi ni magumu lakini sio kama wa mjini daslam
Tatizo jingine ni kina mama kutotaka mabinti wakubwa wawe walezi wa watoto wao (Baby sitter) badala yake wanataka watoto wao walelewe na vitoto vya miaka 13 toka vijijini huko.

Kina mama wakibadili mitizamo ya kwanza ajira ziataongezeka na usalama wa watoto majumbani utaongezeka pia.
 
elimu ya utumwa imagine mpka leo mtoto anafundishwa kua tulikua nyani cha kujiuliza hilo somo lina faida gani kwenye maisha ya utandawazi huu
 
Unajenga shule Kila kona

Ila facility zingine za kurahisisha elimu Bora hazipo mfano hizo lockers/makabati ya wanafunzi kuhifadhia vitu vyao shuleni.

Au wabuni meza za kisasa wanazotumia darasani wawekea humo baadhi ya daftari na vitabu.

Au lockers ziwe darasani au kwenye korido za madarasa
mbona hii sisi tulitumia tena kulikua na mfumo unapoanza form 1 unachonga kiti na meza unaoewa mchoro toka shule kwenye form ya kujiunga
 
Kwa mfano fikiria mwalimu wa somo la hisabati hayupo,na ana kipindi.
Ikabidi mwalimu mwingine wa Kiswahili akataka afundishe badala yake.
Huoni kuwa kama wasingekuwa na madaftari ya Kiswahili wangesomaje?.
Hiyo siyo shule sasa. Maana ya shule ni pamoja na kuwepo kwa Ratiba na ni lazima ifuatwe!!
 
Tatizo jingine ni kina mama kutotaka mabinti wakubwa wawe walezi wa watoto wao (Baby sitter) badala yake wanataka watoto wao walelewe na vitoto vya miaka 13 toka vijijini huko.

Kina mama wakibadili mitizamo ya kwanza ajira ziataongezeka na usalama wa watoto majumbani utaongezeka pia.
Binafsi kitu dada wa kazi hakipo tena kwenye hesabu za familia yangu, changamoto ni nyingi lakini kijiji changu nakimudu..... dada wa kazi awe mkubwa au mdogo ni swala la kubahatika tu mauza uza ni mengi.

Kiuhalisia kama mnataka malezi ya watoto yawe na tija, mama hatakiwi kuwa mtu wa kufanya kazi ya kurudi nyumbani usiku. Mama by saa kumi jioni ukiwa nyumbani mambo mengi yanaenda sawa...

Lakini hii ya kurudi Monday to Friday saa mbili usiku, siku 2 weekend hazitoshi kulea mtoto hata kama una dada mzuri vipi, mtoto ni wa wazazi dada ni msaidizi
 
Hili ni janga mkuu Watoto wamekua kama wapakia mizigo mpaka usiku kabla hawajalala wapewe paracetamol ya kutuliza maumivu ya Mgongo.
 
Nadhani tuliowengi humu tumesoma St.Kayumba na tunafahamu kuwa walimu ni nadra sana kufuata ratiba ya darasa mathalani unakuta mwalimu wa somo la siku husika hajafika shule hivyo itampasa mwalimu/walimu waliopo waje kuwafundisha darasani ili mradi tu isipite siku bila kufundishwa angalau somo lolote lile.
My take kwa wizara wangetengeneza LOCKER kama wenzetu Ulaya na kila mwanafunzi angekuwa na locker yake itakayoweza kuwa maalamu kwakuhifadhi vitabu na vitu vingine vya mwanafunzi.
Nimesoma kayumba vidudu mpaka form 4 na hatukua tunabeba mawe aisee kama hivi
 
Huwezi kuelewa mzigo wanaobebeshwa wanafunzi wa shule za kutwa mpaka pale utakapojaribu kuubeba mfuko wa madaftari wanaobeba wakienda shuleni. Kitendo cha watoto kulazimishwa kwenda na Vitabu vya kiada na Madaftari ya Masomo yote shuleni kila siku kinawaletea wanafunzi hao matatizo kwenye uti wa mgongo.

Hivi kila shule si ina ratiba ya Masomo. Kwa nini watoto wabebeshwe mzigo wa madaftari na vitabu kwa masomo yasiyohusika kwa siku hiyo. Kama Ratiba inaonesha kutakuwa na masomo manne ni kwa nini mtoto asibebe madaftari ya masomo hayo tu?

Miaka ijayo jamii itaingia gharama ya kutibu watu wazima chungu nzima watakaokuwa wanaumwa uti wa mgongo, chanzo kikiwa ni uzembe tu wa walimu kulazimisha watoto kubeba mzigo wa madaftari na vitabu bila ya sababu.
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom