Waziri wa Elimu na TAMISEMI, ni sawa Wanafunzi Shule za Serikali kuambiwa waende na dissecting kit na vitabu vya tahasusi?

Kwa ada ya elfu 70 unategemea apate mahitaji yote shuleni?
Mpeleke private ada milioni 4 atapata kila kitu
 
Unatetea nini hapa...?

Kwamba watu au serikali ijenge shule halafu isi - equip shule zake na vifaa vya kujifunzia na kufundishia..? Nini maana ya shule sasa?

Nielewe tunajadili na kutetea "shule kwa wote" bila kujali uwezo wa mtu...

Tena hapa tunajadili "shule za serikali". Sijui unaelewa?

Wewe unavyoona kwa kuwa mimi na wewe tunako hako ka uwezo ka kutoa hizo unazoiita "photocopies " unadhani kila mtu anaweza kutoa photocopies, si ndiyo eeeh..??
 
Bila shaka mwanao kasoma shule ya kata kwenye elimu bure
USIMNUNULIE DIRECTION KIT ATA TUMIA NINI?
Hujaelewa mantiki ya hoja yangu, rudia tena kunisoma AU fuatilia mjadala, hoja yako imeshajibiwa huko juu...
 
Huyu mzazi mchachu kweli,
Unataka vianze vitabu , wanyeshewe halafu uje upake tena?
Ada 70,000/= na unataka mwanao akute kila kitu? Kalipe milioni tano private atakuta kila kitu.
Kwamba ni bora asomee nyumbani. Mkuu hakuna kinachoshindikana. Msomeshe nyumbani tu.
Kama ukimpeleka, hao jamaa watajuta kuchagua mtoto wako!
 
A levo gharama na hapo jiandae kumpeleka twisheni akirudi likizo.
 
Hujaelewa mantiki ya hoja yangu, rudia tena kunisoma AU fuatilia mjadala, hoja yako imeshajibiwa huko juu...
Kwa kifupi ni kwamba serikali haina uwezo wa kukidhi mahitaji ya kila mwanafunzi kuanzia awali mpaka kidato cha sita ndiyo maana tangu primary wazazi tunatoa michango
Zamani wakati sisi tunasoma tulikuwa tunapewa hadi daftari bure na ada ilikuwa shilingi 100/-
 
CCM ni waongo mno.
Serikali ya CCM ni wanafiki na wazandiki wanasema elimu bure ni uwongo huku wazazi wakiamini,huko mashuleni hakuna vitabu kuanzia shule za msingi hadi sekondari unashangaa wazazi yaani maccm yanaamini sijui hawa watanzania wamelogwa au vipi!
Hivi ni nani aliwambia huko. A-Level elimu inatolewa bure?!

Kwanza Elimu Bure siyo sela ya taifa.
 
Well said sister
 
Asante sana ndugu...

Wewe umeelewa na umejadili hoja na kwa namna hii tunaweza kupata suluhisho...

Ni kweli tatizo hapa ni mfumo mbovu wa elimu kuanzia Sera mpaka kwenye funding system ya shule zetu...

Udhaifu mkubwa wa wachangiaji wengi wa mada hii, wanadhani hii hali ni ya kawaida tu na twende hivi hivi...

Hapana, hii siyo kawaida. Kuna matatizo ya kisera na mipango katika nchi yetu...

Mfano utakuwaje na shule ya masomo ya sayansi halafu usiwe na maabara iliyo full equipped na vifaa vyake? Hiyo dessecting kit si ni sehemu ya vifaa vya maabara...?

Pamoja na kwamba kwa sasa tutakwenda hivi kwa sisi wazazi kulipa kodi ya maendeleo direct, na ada na michango mbalimbali huko shuleni kununua vitabu nk, lakini lazima serikali na yeyote anayetaka kuanzisha shule awe na mpango madhubuti kuhakikisha inayoanzishwa iwe shule kweli na siyo mabañda ya kufugia Kuku...
 
Kama vitabu vitakuwa mali yake hapo hakuna shida. Ila kwa lundo la mahitaji hayo du!!
 
Hela ya Kuhonga vimada unayo ila ya kumnunulia vitabu mwanao ndio unalalama mpaka mishipa ya shingo inakutoka.

Wazazi wengine ni hovyo kabisa!!.
 
Kwa kweli, orodha uliyoambatisha kwenye andiko lako ( Joining instructuon) ni ndefu haswa, ila kuhusu vitabu hilo ni muhimu sana kwa mwanao. Shule za Serikali nyingi (na pengine hata Binafsi) haziwezi kuwa na vitabu sawa na idadi ya wanafunzi. Library unaweza kuta nakala 20 za vitabu lakini wanafunzi wapo 300. Kwa hiyo, nakusahauri, mnunulie Mwanao vitabu vyake kama unajali maendeleo ya kitaaluma yake. Vinginevyo atakwenda kulima zaidi kuliko Kusoma, jambo ambalo ndio limempeleka huko. Pia shule hapo haina hatia sana kwa sababu hayo mahitajo hadi uletewe wewe yamepitia hatua kadhaa ikowemo bodi ya shule pia Afisa Elimu/Mkurugenzi kuyapitia hayo mahitaji ndio Joining Instruction iruhusiwe kuanza kutumika. Elimu ni gharama.
 
Vizuri sana. Hata hivyo...

1. Pamoja na yote haya, sina hakika kama umeelewa "logic" ya mjadala huu niliouanzisha...

2. Lengo langu la kuibua mjadala huu wa kielimu kwa staili hii ni ili kila mtu anayeelewa ajadili na kujibu maswali muhimu kadhaa;

å Kwanini mambo yako hivi?
å Tatizo liko wapi?
å Je, hivi ndivyo mambo yanavyopaswa kuwa?

3. Wewe umejitambulisha kuwa ni mwalimu. Na umejaribu kunielewesha sana, lakini bahati mbaya sijakuelewa kwa sehemu kubwa kwa SBB;.

å Katika maswali matatu hayo hapo juu, umejibu swali moja tu. Umekubali kuwa, haya mambo ndivyo yalivyo, ni kawaida kabisa..
å Umenipa onyo kuwa, mzazi NIKOMAE TU na mwanangu akizubaa ataruka na zero...!!?? Jibu la hili ni rahisi tu. That has never happened before and it will never happen to my children no matter what....!!
å Nisifikiri kuwa napigwa (NAIBIWA) kwa sababu ya kuibua hoja hii. Really? Serious?
å Na mwisho umenitaka niwe na POSITIVE THINKING to teachers and the government at large...

## Kwa hoja zako hizi, ni ushahidi kuwa wala hujaelewa mantiki (logic) ya mjadala huu...

4. Lakini, It's alright. Let me try to be positive about your school, you teachers and the government kama ulivyoshauri kwa sababu that's not a big deal at all...

5. Na sasa baada ya maelezo yako yooote hayo, naomba nijibu kwa ufupi baadhi ya hoja yako na pia nikuachie wewe changamoto kadhaa;

MOSI; IDADI YA WALIMU KUWA NDOGO KULIKO IDADI YA WANAFUNZI:

Maswali kwako:

¶ Ni kosa la nani hili..?
¶ Ni jukumu la nani ku - balance mambo kwa maana ya kutafuta/kuajiri walimu ili kuleta uwiano kati ya walimu na idadi ya wanafunzi?
¶ Hakuna walimu mitaani wasio na ajira?
¶ Kwanini wako mitaani huku shule zikiwa hazina walimu? Unadhani tatizo ni nini?
¶ Unadhani suluhisho la hili ni nini?

PILI; UHABA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA = IKO HIVYO TOKA ZAMANI..

Maswali kwako:

¶ Nani ana wajibu kuhakikisha shule za umma ziko equipped na vifaa vya kufundishia na kujifunzia?
¶ Wewe unadhani kwanini hali iko hivi?
¶ Je wewe kama mwalimu unaijua na kuitambua Sera ya elimu Tanzania?
¶ Unafahamu kuwa katika serikali hata katika maisha ya mtu binafsi kuna kitu kinaitwa "sera na mipango?"
¶ Je, unadhani mambo ndivyo yanavyotakiwa kuwa? Kama jibu lako ni "NDIYO", tuishie hapo tusiendelee na mjadala huu. Lakini kama jibu lako ni " SIVYO" basi twende kazi tuendelee kujadiliana hadi tupate mwafaka...

HIVI NDIVYO ILIVYO TOKA ZAMANI..!!??

Kwanza, naomba nishangae kuwa, kauli hii imetoka kwa mwalimu kitaaluma..!!

å Je, hapa una maana ya kuwa, shule za umma kukosa vifaa vya kujifunzia na kufundishia ndivyo ilivyo toka zamani, ni kawaida hiyo? Au siyo mwalimu?

√• Je, hapa una maana pia kuwà, shule za umma kutokuwa na uwiano sawa kati ya idadi ya walimu na wanafunzi ndivyo ilivyo toka zamani, ni kawaida hiyo? Au siyo mwalimu?

Maswali kwako:

¶ Hii "ndivyo ilivyo toka zamani" ina maana gani?
¶ "Zamani" kwako ni lini kwani?
¶ Wewe ni mwalimu kweli? Una muda gani toka uanze kufundisha? Umesoma shule gani? Kama ni hizi zenye shida hii, basi kumbe NI KAWAIDA..!!

SASA mimi nakuambia hivi ndugu yangu, MAMBO HAYAKO HIVI TOKA ZAMANI...!!

Kuna tatizo la KISERA na KIMIPANGO katika nchi yetu na hii ndiyo imeharibu mambo haya. Hukupaswa ufundishe shule yenye mapungufu haya. Uwingi wa wanafunzi (students/pupils enrollment increment) siyo hoja na kamwe siyo utetezi wa kutetea mapungufu haya...

Nchi yetu kwa maana ya huko serikalini uliko kunakosekana mambo haya na kama yapo basi kuna tatizo la kutojali (negligence);

1. Mipango madhubuti

2. Vipaumbele vya matumizi ya rasrimali fedha

3. Commitment (utashi wa kisiasa)

4. Matumizi mabaya ya fedha za umma kunakotikana na namba 2 hapo juu...
 

Sina tatizo na yote haya...

Sina tatizo na kulipia kila kitu so long as mtoto asome na kupata anachokitaka..

Swali langu ni hili; Je, hivi ndivyo mambo yanavyopaswa kuwa ktk shule za umma?
 
Mzazii shule nyingi hazina vitabu narudia tena hazina vitabu na vikiwepo nivile vya TIE(Tanzania Institute of Education) ambavyo viko shallow mnoo
Tunaelewana kweli? Mjadala hapa ni shule kukosa vitabu kabisa na kuwataka wanafunzi waende na maboksi ya vitabu shuleni...!

Hata hiivyo, vya Tanzania Institute of Education (T.I.E) navyo ni vitabu. Viwepo hivyo hivyo mashuleni kwa wingi. Tatizo hata hivyo pengine havipo kabisa...!

Mapungufu atayaona mwanafunzi (mwanangu) mwenyewe akishafika huko. Yeye ndiye atasema baba/mama nahitaji kitabu cha ziada (reference books) hiki ama kile ili kinisadie na nitanunua (kama uwezo upo)...

Kuna wenye watoto wengine hawana uwezo kabisa wa kutoa hata photocopy achilia mbali kununua vitabu. Wakikuta hivyo shuleni, watatumia hivyo hivyo na watafaulu...
 
Wengi hawaelewi haya...

Kimsingi mjadala ulitakiwa ujadiliwe kwa kuhusianisha vipaumbele vya nchi yetu ktk matumizi ya rasrimali fedha...

Sasa naona wanaochangia mada hii humu wengi ni vijana wadogo pengine product ya shule za kata zenye mapungufu haya na wao wanadhani mambo ndivyo yalivyo na kawaida tu...

Asante sana kwa mchango wako ndugu JokaKuu..
 
[emoji23][emoji23]Kumbe mzazi na yeye alipita shule tena special school[emoji23] acheni kumlaumu sasa

Hakuna anayenilaumu...

Kila mtu anajadili hoja hii kulingana na upeo, ufahamu na uelewa wake katika jambo hili..

Yote ni mawazo mazuri na yanakubalika ktk msingi wa uhuru wa mjadala...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…