Mzazi pole sana kwa tatizo hill, naomba Mimi nikueleweshe kidogo japo Mimi ni mtumishi katika hiyo idara, kwanza Mzazi ninaomba uwe na positivity thinking kwa walimu na serikali yako.Usiwe na ideology ya kwamba unapigwa(UNAIBIWA) maana ukijifanya mjanja utashangaa motto anarudi akiwa hewa kabisa na kufeli mitihani take ya mwisho.
Mbili, Elimu ya elimu ya sekondari kwa kidato cha tank IPO palepale au zaidi ya zamani kwa sababu ya kuajiri walimu wengi zaidi kwa sababu idadi ya walimu ni ndogo kuliko idadi halisi ya wanafunzi wanaochaguliwa katika hizo SHULENI hivo inafanya pia shule zimsaidie motto aweze kufanikisha ndoto zake kwa kumnunulia baadhi ya vitabu vya ziada vitavyomsaidia kujisomea akiwa nyumbn au shuleni.
Tatu,Kuhusu vifaa vya kujifunzia kwenye maaabara kama dissecting kit hili lipo tangu zamani na ni muhimu sana kwa mwanafunzi wa kidato cha tano na sita ili aweze kufaulu mitihani yake.
Nne,MWAMBIE MTOTOakapambane aendako atakutana na vijana wa kilaaina magenius waliotoka vijijini ambao wanajua zaidi na hawana vitabu kabisa lakini ni Vipanga hatari na hawajui MSAMIATI WA TUITION!!!!Asiwafuate maisha yao ataumbuka yeyye akapambane mpk chozi la mwisho na mwambie mwalimu anamtakia masomo mema na ufikirio mzuri na wa tija huko aendako Asiendekeze Sifa na zinaaa ama vitu vya kisasa labda kama vinamsaidia sawa
Vizuri sana. Hata hivyo...
1. Pamoja na yote haya, sina hakika kama umeelewa "logic" ya mjadala huu niliouanzisha...
2. Lengo langu la kuibua mjadala huu wa kielimu kwa staili hii ni ili kila mtu anayeelewa ajadili na kujibu maswali muhimu kadhaa;
å Kwanini mambo yako hivi?
å Tatizo liko wapi?
å Je, hivi ndivyo mambo yanavyopaswa kuwa?
3. Wewe umejitambulisha kuwa ni mwalimu. Na umejaribu kunielewesha sana, lakini bahati mbaya sijakuelewa kwa sehemu kubwa kwa SBB;.
å Katika maswali matatu hayo hapo juu, umejibu swali moja tu. Umekubali kuwa, haya mambo ndivyo yalivyo, ni kawaida kabisa..
å Umenipa onyo kuwa, mzazi NIKOMAE TU na mwanangu akizubaa ataruka na zero...!!?? Jibu la hili ni rahisi tu. That has never happened before and it will never happen to my children no matter what....!!
å Nisifikiri kuwa napigwa (NAIBIWA) kwa sababu ya kuibua hoja hii. Really? Serious?
å Na mwisho umenitaka niwe na POSITIVE THINKING to teachers and the government at large...
## Kwa hoja zako hizi, ni ushahidi kuwa wala hujaelewa mantiki (logic) ya mjadala huu...
4. Lakini, It's alright. Let me try to be positive about your school, you teachers and the government kama ulivyoshauri kwa sababu that's not a big deal at all...
5. Na sasa baada ya maelezo yako yooote hayo, naomba nijibu kwa ufupi baadhi ya hoja yako na pia nikuachie wewe changamoto kadhaa;
MOSI; IDADI YA WALIMU KUWA NDOGO KULIKO IDADI YA WANAFUNZI:
Maswali kwako:
¶ Ni kosa la nani hili..?
¶ Ni jukumu la nani ku - balance mambo kwa maana ya kutafuta/kuajiri walimu ili kuleta uwiano kati ya walimu na idadi ya wanafunzi?
¶ Hakuna walimu mitaani wasio na ajira?
¶ Kwanini wako mitaani huku shule zikiwa hazina walimu? Unadhani tatizo ni nini?
¶ Unadhani suluhisho la hili ni nini?
PILI; UHABA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA = IKO HIVYO TOKA ZAMANI..
Maswali kwako:
¶ Nani ana wajibu kuhakikisha shule za umma ziko equipped na vifaa vya kufundishia na kujifunzia?
¶ Wewe unadhani kwanini hali iko hivi?
¶ Je wewe kama mwalimu unaijua na kuitambua Sera ya elimu Tanzania?
¶ Unafahamu kuwa katika serikali hata katika maisha ya mtu binafsi kuna kitu kinaitwa "sera na mipango?"
¶ Je, unadhani mambo ndivyo yanavyotakiwa kuwa? Kama jibu lako ni "NDIYO", tuishie hapo tusiendelee na mjadala huu. Lakini kama jibu lako ni " SIVYO" basi twende kazi tuendelee kujadiliana hadi tupate mwafaka...
HIVI NDIVYO ILIVYO TOKA ZAMANI..!!??
Kwanza, naomba nishangae kuwa, kauli hii imetoka kwa mwalimu kitaaluma..!!
å Je, hapa una maana ya kuwa, shule za umma kukosa vifaa vya kujifunzia na kufundishia ndivyo ilivyo toka zamani, ni kawaida hiyo? Au siyo mwalimu?
√• Je, hapa una maana pia kuwà, shule za umma kutokuwa na uwiano sawa kati ya idadi ya walimu na wanafunzi ndivyo ilivyo toka zamani, ni kawaida hiyo? Au siyo mwalimu?
Maswali kwako:
¶ Hii "ndivyo ilivyo toka zamani" ina maana gani?
¶ "Zamani" kwako ni lini kwani?
¶ Wewe ni mwalimu kweli? Una muda gani toka uanze kufundisha? Umesoma shule gani? Kama ni hizi zenye shida hii, basi kumbe NI KAWAIDA..!!
SASA mimi nakuambia hivi ndugu yangu, MAMBO HAYAKO HIVI TOKA ZAMANI...!!
Kuna tatizo la KISERA na KIMIPANGO katika nchi yetu na hii ndiyo imeharibu mambo haya. Hukupaswa ufundishe shule yenye mapungufu haya. Uwingi wa wanafunzi (students/pupils enrollment increment) siyo hoja na kamwe siyo utetezi wa kutetea mapungufu haya...
Nchi yetu kwa maana ya huko serikalini uliko kunakosekana mambo haya na kama yapo basi kuna tatizo la kutojali (negligence);
1. Mipango madhubuti
2. Vipaumbele vya matumizi ya rasrimali fedha
3. Commitment (utashi wa kisiasa)
4. Matumizi mabaya ya fedha za umma kunakotikana na namba 2 hapo juu...