Umemaliza utata, kikao kifungwe.Waziri aingilie kati vipi wakati umeshasema ni shule binafsi? Kila shule ina utaratibu wake, unadhani wakiruhusu hivyo kila mzazi kumtembelea mtoto wake anavyo jisikia kutakuwa na shule tena hapo? Na vipi kuhusu yule mtoto ambaye hato tembelewa huoni kwamba atakuwa anajisikia unyonge? Kama kuna tatizo hasa wasiliana na uongozi watakujuza maendeleo ya mtoto wako, ila ukiona umeshindwa huo utaratibu unaweza kumhamisha mtoto wako bila kusumbua watu wengine.
Siku moja nilikwenda kumtembelea mwanangu na kuhudhuria mkutano wa mwaka wa wazazi. Baada ya mkutano kuna kama masaa mawili hivi, mzazi unakaa na mwanao kula nae na kupiga story. Nilipomaliza kupiga story na mwanangu, ile naagana nae, akaniambia tazama baba jirani yetu hajafika, mwanae yule pale analia. Kweli nageuka kumtazama mtoto ameshindwa hadi kula kwa kuwa hakuna mzazi /mlezi aliyemtembelea.
Nilipiga simuvaongee na mamake, akamwambia sikuwa na nauli. Aliniomba nimwachia japo hela ya sabuni. Nilifanya hivyo na mtoto akapata angalau ahueni.
Tuchukulie kila mwezi wazazi watembelee watoto wao. Kwa wazazi wasio na uwezo wa kutosha kumudu nauli, itakuwaje kisaikolojia kwa watoto wao?
Halafu mawazo haya ni ya kishamba sana. Hivi miaka ile unatoka Mtwara unapangiwa sekondari Mwanza, tulikuwa tunatembelewa na wazazi? Januari hadi Juni no mzazi wala rafiki na kama huna nauli ya kuendea kwenu unabaki shule hadi Desemba. Shule zilijua hilo na zilitoa nafasi kwa wasio na nauli unajiandikisha kubaki shuleni.
Kwa sasa tunadekeza sana watoto kiasi cha kutaka umfuate kila alipo kila mara. Ni sehemu ya kuharibu watoto.