Waziri wa fedha ingilia kati sakata la uboreshaji wa mashine za EFD, kamishna wa TRA ataleta balaa kubwa

Kwanza nikupongeze kwa kujua kudiscuss. Kitu kistaarabu sio Kama hawa wengine kitu hakijui anakurupuka tu kuongea
Mimi nachojua mkuu kwanza tra walitoa waraka
Pili waliblock mashine zote.kama unavojua efd yako ikiwa na shida immediately unatakiwa ureport.sasa Kama mashine umezimiwa tuassume huna taarifa ya kuupgrade mashine then umefanyeje biashara mwezi mzima bila mashine??
 
Block nadhani imeanza tarehe 7 January kwa wale niliwaona mimi kwenye mkutano inaonekana walikuwa wakitumia hizo machine mpaka tarehe 5 siku iliyofuata wakapokea txt message tarehe 7 mwisho ndio taharuki ilipoanzia.

Kwa kifupi ni kwamba zoezi alikuratibiwa vizuri. Hakuna tofauti na sakata la vitambulisho vya NIDA au simu inazimwa. Watu wanatoa matangazo bila ya capacity planning na kwenye hili la TRA jumlisha na poor communication strategy too.
 
Tatizo labda elimu pia watanzania tuna uzembe wa kutojali vitu
 
Tatizo labda elimu pia watanzania tuna uzembe wa kutojali vitu
Hiyo ni popote duniani binadamu wengi tu wazembe ndio maana mabadiliko yanaendana raising awareness campaigns; kitu ambacho TRA awakufanya apparently.
 
Hiyo ni popote duniani binadamu wengi tu wazembe ndio maana mabadiliko yanaendana raising awareness campaigns; kitu ambacho TRA awakufanya apparently.
Kingine ni kwamba kuna gharama ya marekebisho hayo zinazolipwa na Mfanyabiashara binafsi , na kuna baadhi ya mashine hazikubali hiyo software , hivyo ni lazima huyo mfanyabiashara anunue mashine mpya , jambo kama hili katika biashara hizi za sasa unawezaje kuweka muda wa siku 30 ?
 
TRA wameshindwa ku maintain website tu.

Wiki nzima ya kwanza ya 2021 website yao ilikuwa down.

Huko kwenye mitandao ya kulipa kodi wakiharibu sishangai.
 
Una mashine?
Kwa mwekezaji mkubwa kama mimi ninayemiliki viwanda kadhaa nakosaje mashine kwenye nchi hii ambayo mashine ni lazima ? Halafu kingine unachopaswa kukijua ni kwamba mtu mmoja aweza kuwa hata na mashine 15 au zaidi kutokana na mtandao wa biashara zake nchi nzima , sasa angalia jinsi ilivyo
 
Mbona kwa wenye viwanda program ya kuupdate ilianza toka mwezi wa kumi?? Au wewe kiwanda chako cha wapi?? Watu wa chadema Kila kitu mnapinga nchi hii. Tuache tulipe kodi
 
Rarely they consider thing which might go wrong kabla ya kuweka deadlines zao.
 
Mbona kwa wenye viwanda program ya kuupdate ilianza toka mwezi wa kumi?? Au wewe kiwanda chako cha wapi?? Watu wa chadema Kila kitu mnapinga nchi hii. Tuache tulipe kodi
Kiukweli mimi nimepata taarifa mwezi huu wakati tra waliposem hawataongeza muda. Yaani kumbe deadline ilishaisha
 
Mkuu una biashara yoyote unayoisimamia au uliyoianzisha?
Biashara yangu mimi, wewe inakuhusu nini? Ndiyo majungu hayo unataka kutafuta umaarufu kupitia mtandao wa JF - Aibu!
 
Biashara yangu mimi, wewe inakuhusu nini? Ndiyo majungu hayo unataka kutafuta umaarufu kupitia mtandao wa JF - Aibu!
Wacha1. Wewe ni mkongwe ndungu yangu.
Sihitajiki kubishana na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…