Waziri wa fedha ingilia kati sakata la uboreshaji wa mashine za EFD, kamishna wa TRA ataleta balaa kubwa

Waziri wa fedha ingilia kati sakata la uboreshaji wa mashine za EFD, kamishna wa TRA ataleta balaa kubwa

Kawaida wabongo kila zoezi wanasubiri mwishoni ndio wanakurupuka wengi wanategemea watahudumiwa hio siku ya mwisho.
1.nida
2.tin verification
3.passport
Na sasa hivi zoezi hili wamesubiri mwezi umeisha ndio wanaenda na kuomba muda uongezwe.
Mimi nilipeleka mashine yangu Dec 30 wakati wengi bado wanakula sikukuu na ilikuwa upgraded siku hio hio.
 
Mtu anayelipa kodi halali 100% kwenye hii serikali ya kizuyunani hana akili.. Loopholes zipo kibao, chezeni nazo..

Mimi nacheza nazo, na nawaumiza sana tu..
 
Kuna siku nililalamika kuhusu ili jambo kuna kichaa mmoja akaona ni suala dogo. Magufuli ajaribu kuangalia sana hawa TRA hawana nia njema kbs na kama ndio anawatuma kuna jambo analitafuta. Kulikuwa na uharaka gani? EFD zina serial number zina TIN namba hili janga la BARCODE linakuja kuharibu kbs biashara za watu. TRA wajiangalie biashara haifanywi kwa sifa za kijinga unatoa mwezi mmoja ili iweje.
 
Kingine ni kwamba kuna gharama ya marekebisho hayo zinazolipwa na Mfanyabiashara binafsi , na kuna baadhi ya mashine hazikubali hiyo software , hivyo ni lazima huyo mfanyabiashara anunue mashine mpya , jambo kama hili katika biashara hizi za sasa unawezaje kuweka muda wa siku 30 ?
Mashine yangu ilikubali upgrade,sikununua na ilifanywa bure na supplier.
 
Kuna siku nililalamika kuhusu ili jambo kuna kichaa mmoja akaona ni suala dogo. Magufuli ajaribu kuangalia sana hawa TRA hawana nia njema kbs na kama ndio anawatuma kuna jambo analitafuta. Kulikuwa na uharaka gani? EFD zina serial number zina TIN namba hili janga la BARCODE linakuja kuharibu kbs biashara za watu. TRA wajiangalie biashara haifanywi kwa sifa za kijinga unatoa mwezi mmoja ili iweje.
Unajua kwanini wameweka hio system ya barcode?
 
Unashauri zoezi lingechukua muda gani?
Swali lako lielekezwe kwa mawakala , angalau kila wakala anajua idadi ya mashine alizosambaza na bila shaka anajua kwa siku 1 angeweza kurekebisha mashine ngapi , baada ya hapo ingekuwa rahisi sana kwa TRA kujua zoezi hilo laweza kwisha kwa muda gani
 
Biashara yoyote yenye mauzo ghafi 14m na kuendelea.
hii unamaanisha Kwa mwaka mkuu sio?
mauzo ghafi Kwa ngeli ni nini?
je yakiwa chini ya 14m unataka nini mtu akinunua kitu? Au najitengezea za kwangu stationery?
 
On upgrading of EFD:Kuna tatizo upande wa Wakala wa Permagon Mwanza Nyerere Road wanalazimisha wafanya biashara kununua betri mpya kwa ajili ya EFD ili hali zilizokuwepo zinafanya kazi. Hoja eti mfumo mpya ili ufanye kazi vizuri lazima uweke betri mpya. This technicality is nonsense Mamlaka ziangazie hili. Ni usumbufu na inaongeza gharama
Yes huu ujinga mawakala wanapiga watu sana

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Wacha kamba wewe, mwezi moja unatosha sana nyinyi mmezoea kazi ndogo kama hizi kufanywa kwa miezi sita. Hakuna huo mpango hivi sasa. Baada ya mwezi lazima wamalize wafanye kazi usiku na mchana.
Ndugu umewahi kufanya biashara yoyote hata ya genge lakuuza pilipili maana ulichoongea hapa inadhihirisha ni mtumwa wa ajira

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza nikupongeze kwa kujua kudiscuss. Kitu kistaarabu sio Kama hawa wengine kitu hakijui anakurupuka tu kuongea
Mimi nachojua mkuu kwanza tra walitoa waraka
Pili waliblock mashine zote.kama unavojua efd yako ikiwa na shida immediately unatakiwa ureport.sasa Kama mashine umezimiwa tuassume huna taarifa ya kuupgrade mashine then umefanyeje biashara mwezi mzima bila mashine??
Unaongea usichokijua nadhani wee ni muajiriwa huwezi kuelewa kitu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Kingine ni kwamba kuna gharama ya marekebisho hayo zinazolipwa na Mfanyabiashara binafsi , na kuna baadhi ya mashine hazikubali hiyo software , hivyo ni lazima huyo mfanyabiashara anunue mashine mpya , jambo kama hili katika biashara hizi za sasa unawezaje kuweka muda wa siku 30 ?
Ndugu nikisoma comments za huyo anaejiita natafuta naona Nchi bado ina wajinga wengi sana

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Hili jambo wanaliona labda ni dogo lakini kuna manung'uniko makubwa ndani ya mioyo ya wafanya biashara kwa sababu jambo hili lingepewa muda lifanyike vizuri. Nenda pale ' web technologies ' pale Fire, Kariakoo kuna msongamano mkubwa sana usio wa lazima ambao hata unaweza kuleta madhara mengine na hasa kutokana na hali ilivyo huko duniani kwa sababu hatuwezi kujua nani kaja jana au juzi na huko alikutana na watu gani.

Kwa sababu kodi inalipwa na imekuwa ikilipwa ni swala la kufanya 'upgrading' tu,basi lipewe muda lifanyike kwa ufasaha bila madhara au manung'uniko na kuanza kuisema vibaya serikali kwa sababu tunajua lengo ni zuri kutokana na hili zoezi. Tunaomba hata ikibidi Rais alisikie hili na kulitolea tamko ili muda wa zoezi hili uongezwe.

Mmh! Mmeshindwa kuyaongea hayo kule chamani? Mmeshindwa kujua serikali ni uwakilishi wa watu?

Huvu mnanung'unikiwa. Nyie ni wawakilishi wa nani?
 
Back
Top Bottom