Waziri wa Fedha: Serikali itaanzisha ushuru wa huduma za mitandaoni ‘Digital Service Tax’

Waziri wa Fedha: Serikali itaanzisha ushuru wa huduma za mitandaoni ‘Digital Service Tax’

Mwigulu Nchemba waziri wa fedha wa hovyo kabisa kutokea tangu tupate Uhuru.
Mwigulu Nchemba original Ni msukuma na yupo, anajulikana.

Alipochana bungeni bajeti ya kambi rasmi ya upinzani akathibitisha kwa mara nyingine.

Funika bovu ni pale alipoanza kujiandika kwenye mawe na majabali nchi nzima kwamba yeye Ni raisi.
Kupiga chata alifanya ras jeff kapita enzi zile akiwa kijana mdogo, chini ya miaka 18
Huyo ras jeff kapita ni kijana mtiifu wa CCM wale wanaofaa kazi za wasiojulikana. Chata zake pale Mbeya town zinazubaa kila chocho anaonekana mtu wa vijiweni huyu
 
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaanzisha ushuru wa huduma za mitandaoni ‘Digital Service Tax’, “hili ni eneo jipya ambalo tunalifanyia kazi, katika bajeti zinazofuata litakuwa ingizo jipya. Mataifa mengi yanageukia kodi hii.”

Kazi na iendelee!
Ni ujinga kuleta ushuru kwenye hizo zinazoitwa digital service na wakati wameshindwa kuboresha huduma za kupokea malipo kimtandao kutoka mataifa mengine.
 
Natamani sana kukijua Chuo Kikuu kilichompa hiyo 'Doctorate' yake hiyo ili nikidharau kama ninavyomdharau Yeye.

Nashukuru hajasoma Chuo Kikuu changu bora, pendwa na barikiwa cha SAUT Mwanza au hiki cha Dar es Salaam ( School of Graduate Studies ) Msimbazi Center ambacho kinatoa 'Geniuses' tupu nchini Tanzania.
Alipewa PhD kwa kisiasa.
 
Kodi ya kuwa na mke/mume 😂😂😂 kodi ya kuwa na mchepuko 🤣🤣🤣🤣


Nashauri waanzishe hata kodi ya kutembea ama kodi ya kulala usiku.

Waweke kodi ya kuvaa nguo, ukivaa nguo tu unalipa kodi. Ama kodi ya kuongea. Ukiongea tu unalipa kodi

Nashauri waweke kodi ya kila kitu.
 
Nashauri waanzishe hata kodi ya kutembea ama kodi ya kulala usiku.

Waweke kodi ya kuvaa nguo, ukivaa nguo tu unalipa kodi. Ama kodi ya kuongea. Ukiongea tu unalipa kodi

Nashauri waweke kodi ya kila kitu.
Bila kusahau kodi ya kupumua na machangamsho ya chakula cha usiku.
 
😳😳😳😳 Are you serious? Maambukizi mangapi ya HIV yamezuiliwa na ndom? Millions sina maana kwamba hizo taulo si muhimu.

Kondomu sio muhimu wewe ka taulo za kike
 
Magufuli mlisema anaua biashara [emoji23][emoji23][emoji23]huyu wa sasa ni anajali wawekezaji wa kigeni mbona mnaleta lawama
 
Ni hasara na msiba mkubwa sana kwa Watanzania kuwa na bunge la maccm tupu.
 
Tuna bahari,mbuga za wanyama,maziwa matatu makubwa,dhahabu,almasi,tanzanite na nk.Lakini bado hazina faida kwa wananchi. Kuna nchi zimepunguza mzigo wa kodi kwa wananchi kwa usimamizi bora wa rasilimali.Haina faida kua na rasilimali.Mfano gas ya mtwara leo hii ukiuliza inafaida gani kwetu hata jibu watakalo kupa litakukasilisha tu.Hebu viongozi wetu badilikeni simamieni rasilimali zetu vizuri zitusaidie kupunguza mzigo wa kodi.

Sent from my SM-M305F using JamiiForums mobile app
 
Lazima Mwigulu atakua na tatizo sehemu fulani hivi
 
Back
Top Bottom