Waziri wa Kilimo, zao la bangi ni muhimu sana kwa maendeleo ya haraka

Waziri wa Kilimo, zao la bangi ni muhimu sana kwa maendeleo ya haraka

Wanachojali ni kuongeza idadi ya magari mapya kila uchao. Hawezi kupitia uzi huu kujifunza
Hayo ya magari na matumizi ya kifahari yatawageukia vibaya sana siku moja.

Huwezi kuwa unakopa pesa halafu unajaza magari ya anasa. Ni ujinga wa hali ya juu huo.

Magari ya anasa inatakiwa pale bajeti yetu tumekidhi wenyewe na pesa za miradi ya maendeleo imetosha, ile surplus, no problem ukizifanyia fahari.

Siyo kwa hali yetu ya sasa.

Wanafikiri wanatupenda sana wanaotukopesha? Au ni kuwa sisi wajanja sana au tuna uwezo sana wak kulipa ndiyo watukopesha. Hapana, ni chambo kile, wanatuvulia nacho wazima wazima.

Ni wakati sasa tusimame kabisa kukopa, iwe kwa mradi wa maendeleo au kwa chochote kile. Kama kipato chetu hakitoshi ku balance, tishushe matumizi, mpaka tukidhi nayo kwa kipato chetu hicho hicho.

Tusijiingize wenyewe kwenye ndoano ya madeni
 
Hapo ndio na kukubali dadake, sijui kwanin mama akuvuti ktk serikali kama alivyo fanya kwa kina zuhura😁😁🙏
Kusishauri serikali na kuwatumikia Watanzania siyo lazima kuwa serikalini.

AlhamduliLlah ni nature yangu tu.
 
Wakoloni sio watu wema, walituambia gongo Ni haramu wakati konyagi Ni halali, tusivyo jielewa Hadi Sasa hivi gongo tunaamini Ni mbaya.
Ugandan waragi Ni gongo hii hii, sijaona mganda aliyedhurika kwa kunywa waragi lkn nimeona mbunge mlevi wa beer ambaye imemuadhiri Hadi hfawezi kuchambua la kuongea
Yes. Hiyo ni baadhi tu ya mifano hai. Wapo waliokufa kabisa(RIP) kutokana na kunywa kupitiliza konyagi, Jogoo, Visungura na vilevi vikali na halali vya aina hiyo.
 
Hayo 👆 👆 ni kweli, ila lazima hatua za kuchukua (mchakato)ziwepo. Na hatua ya kwanza kabisa kabisa ni kulitambua zao hilo na kuondoa Marufuku ya Kisheria dhidi ya zao hilo yaani kulihalalisha. Watu wawe huru kuwa na zao hilo na sio kama ilivyo sasa linazalishwa kwa kificho na kutumika kwa kificho. i.e. Haliwezi kuwa ni biashara Halali. Kibiashara (black mkt.)lipo ila ni kwa kificho. Kwa mantiki hiyo, wafanyabiashara halali i.e. wenye leseni (Wanunuzi/wateja wahitaji) watakutana na Wakulima/Wazalishaji kwa uwazi na Serikali (Wizara husika) itafanya kazi yake ya kusimamia na kudhibiti ubora wa viwango. Ifike mahali zao la bangi liweze kuchangia ukuaji wa viwanda vya hapa nchini esp. viwanda vya madawa.
Ni kweli kuvuta haifiki hata 1.% ya umuhimu wake na hata wavutaji wake sio sio alarming kama tunavyoambiwa kwani hakuna supporting data.
Hilo nalo wazo.

Mimi naona kwanza ni kufunguliwa kituo cha utafiti, halafu wakati huo huo wakulima wachache kila mkoa wapewe vibali vya kuzalisha mbegu zinazofaa kwa aina fulani ya matumizi. Kwa sababu mimea ya bangi "hemp" ipo aina nyingi.

Kuruhusu matumizi binafasi ni sawa, lakini mbegu zipi zinazoruhusiwa? Hilo ndiyo muhimu.

Hata Hollanda walioanza kuruhusu miaka mingi sana iliyopita, wameruhusu aina fulani za mbegu na kiwango fulani na wauzaji wanapewa leseni kihalali kabisa.
 
Mheshimiwa Hussein Bashe, natumai na Rais wetu mama Samia Suluhu Hasan na washauri wake wengine utawafikia ujumbe huu.

Zao la bangi za aina tofauti tofauti (different varieties of hemp) linastawi vizuri sana Tanzania. Ni wakati muafaka, tena tumechelewa sana, kuanzisha zao la bangi kwa faida. Zao la bangi linaweza kututowa kwenye umasikini kwa haraka sana.

Baadhi ya faida zinazotokana na zao la bangi ni pamoja na:

Dawa aina mbali mbali, zinazotumika hivi sasa mahospitalini na dawa mbadala.

Pia bangi inaweza kutengeza karatasi, inaweza kutengeza mbao, inaweza kutengeza, "vigae" vya kuezekea, "boards" mbali mbali za kujengea na kuundia fanicha, inaweza kutengeza bodi za magari ambazo ni bora kuliko za mabati.

Licha ya hayo, inaweza kutengeneza virutubisho mbali mbali vya kutumika na binadam, wanyama na mimea. Pamoja na madawa ya kuzuia wadudu wa mimea.

Pia bangi inaweza kutengeneza mafuta ya kutumika kwenye magari ambayo ni bora kuliko ethanol na methanol.

Kinachotakiwa kufanywa ni kuanza na aina moja au mbili ya bidhaa muhimu na kufunguliwa kituo maalum cha utafiti na kuzalisha mbegu bora kwa biashara.

hatuna haja ya kutegemea mataifa ya nje kwenye hili, tunaweza kuzalisha mali ghafi zetu wenyewe na kuwauzia nje bidhaa zinazotokana na bangi. Ni kujipanga tu.

Nafahamu Bashe utaweza hili kwa ufanisi mkubwa ukilivalia njuga. Weka legacy kijana kupitia bangi.

Nafahamu wengi wakisikia "bangi" akili zao zinakwenda katika kilevi cha bangi. Kilevi cha bangi ni matumizi duni ya bangi, ingawa na yenyewe inaweza kufanyiwa tafiti ikapatikana mbegu isiyo na madhara na ikauzwa kihalali kuliko hivi sasa tunaletewa mbegu za kutia watu wazimu. Mpaka skanka limejaa sasa hivi linaumiza vijana.

Tuondokane na ujinga na kufata watu wa magharibi. Tumepata elimu ili itukombowe siyo tuendelee kuwa wajinga wa kuburuzwa kama misukule, wanachotaka mabwana wakubwa ndiyo tukifate, ni wakati Tanzania tukajifanyia yetu wenyewe na hao wakubwa tuwaimbishe nyimbo tunazotaka sisi. Rasilimali tunazo, kwanini watuendeshe na mali zetu?

Uchumi tunao lakini tunaukalia, Nyerere. Kwa kudanganywa tu na nchi za magharibi tutaendelee kuwa watumwa wao daima.

Naamini ndani ya miaka mitatu ya kuruhusu zao la bangi na tafiti zake za kina, hatutakopa tena nje, sisi tutakuwa wakopeshaji.

Nawasilisha.
Maisha yanaenda kasi sana sana
 
Yes exactly. Inabidi kuwepo na Uthubutu na kufanya maamuzi ya maksudi.
 
Pia bangi inaweza kutengeza karatasi, inaweza kutengeza mbao, inaweza kutengeza, "vigae" vya kuezekea, "boards" mbali mbali za kujengea na kuundia fanicha, inaweza kutengeza bodi za magari ambazo ni bora kuliko za mabati.
kutoka Bangi mpaka Mbao... ushauri huu hakika Waziri ataukataa ni uwongo
 
Ni kweli kabisa - kuanzia madawa, mafuta ya aina zote, chanzo cha Nishati(Fuel), kamba za kujengea n.k. n.k. Lakini faida zooote hizo Serikali na Wizara zake Mambo ya ndani, Kilimo na Mifugo, Ofisi ya PM na nyinginezo wamezifumbia macho na wameshupalia eti ni zao Haramu.
Huwa nashawishika kuwauliza wale wenye imani zao, Je; Mungu aliumba Haramu ?
Hapana, Mwenyezi Mungu hajaumba haramu, isipokuwa kuna vitu alivyoviharamisha na kuna vitu vya halali kabisa lakini tunaviharamisha wenye kwa kuvitumia vibaya mpaka vinakuwa na madhara kwetu.

Kiislam hata wali kama unakudhuru ni haramu kwako.

Upo hapo ulipo?
 
Mkuu; waTz Raia walishaamka kitambo ila Serikali yao bado inakoroma usingizini. Nadhani Dozi ya mkoloni (Brainwash) ilizidishwa kipimo kwa Serikali na mamlaka zake. e.g. Waliopo humo serikali na vyombo vyake kwa kificho ni watumiaji mno wa zao hilo; ila wakija huku kwetu hadharani wanatukazia ss macho.
Tena ilizidi kweli kweli, mpaka leo tunamuona wa magharibi ana maana kuliko sisi wenyewe, wakati hana maana yoyote kwetu. Anatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa tu.
 
Bangi inatakiwa ihalalishwe tutumie ili vijana tutumie
20240622_204827.jpg
 
Serikali ikiruhusu hii mambo narudi shamba kuwekeza
Hilo zao moja likianzishwa linaweza kutowa ajira za zaidi ya million mbili haraka sana. Kinachotakiwa ni kuanza na kituo kimoja tu cha utafiti wa kina.

Hemp Reseach and Development Centre.

Kila mwenye ubunifu wake aende hapo akapate elimu ya aina ya mbegu, kuotesha kwa faida na matumizi yake kwa kila aina ya mbegu.

Ni very simple. Wala haihitaji "rocket science", tuna wasomi wengi wanaoweza kufanya huo utafiti kiulaini kabisa.
 
Mheshimiwa Hussein Bashe, natumai na Rais wetu mama Samia Suluhu Hasan na washauri wake wengine utawafikia ujumbe huu.

Zao la bangi za aina tofauti tofauti (different varieties of hemp) linastawi vizuri sana Tanzania. Ni wakati muafaka, tena tumechelewa sana, kuanzisha zao la bangi kwa faida. Zao la bangi linaweza kututowa kwenye umasikini kwa haraka sana.

Baadhi ya faida zinazotokana na zao la bangi ni pamoja na:

Dawa aina mbali mbali, zinazotumika hivi sasa mahospitalini na dawa mbadala.

Pia bangi inaweza kutengeza karatasi, inaweza kutengeza mbao, inaweza kutengeza, "vigae" vya kuezekea, "boards" mbali mbali za kujengea na kuundia fanicha, inaweza kutengeza bodi za magari ambazo ni bora kuliko za mabati.

Licha ya hayo, inaweza kutengeneza virutubisho mbali mbali vya kutumika na binadam, wanyama na mimea. Pamoja na madawa ya kuzuia wadudu wa mimea.

Pia bangi inaweza kutengeneza mafuta ya kutumika kwenye magari ambayo ni bora kuliko ethanol na methanol.

Kinachotakiwa kufanywa ni kuanza na aina moja au mbili ya bidhaa muhimu na kufunguliwa kituo maalum cha utafiti na kuzalisha mbegu bora kwa biashara.

hatuna haja ya kutegemea mataifa ya nje kwenye hili, tunaweza kuzalisha mali ghafi zetu wenyewe na kuwauzia nje bidhaa zinazotokana na bangi. Ni kujipanga tu.

Nafahamu Bashe utaweza hili kwa ufanisi mkubwa ukilivalia njuga. Weka legacy kijana kupitia bangi.

Nafahamu wengi wakisikia "bangi" akili zao zinakwenda katika kilevi cha bangi. Kilevi cha bangi ni matumizi duni ya bangi, ingawa na yenyewe inaweza kufanyiwa tafiti ikapatikana mbegu isiyo na madhara na ikauzwa kihalali kuliko hivi sasa tunaletewa mbegu za kutia watu wazimu. Mpaka skanka limejaa sasa hivi linaumiza vijana.

Tuondokane na ujinga na kufata watu wa magharibi. Tumepata elimu ili itukombowe siyo tuendelee kuwa wajinga wa kuburuzwa kama misukule, wanachotaka mabwana wakubwa ndiyo tukifate, ni wakati Tanzania tukajifanyia yetu wenyewe na hao wakubwa tuwaimbishe nyimbo tunazotaka sisi. Rasilimali tunazo, kwanini watuendeshe na mali zetu?

Uchumi tunao lakini tunaukalia, Nyerere. Kwa kudanganywa tu na nchi za magharibi tutaendelee kuwa watumwa wao daima.

Naamini ndani ya miaka mitatu ya kuruhusu zao la bangi na tafiti zake za kina, hatutakopa tena nje, sisi tutakuwa wakopeshaji.

Nawasilisha.
Kama Kenya inavyonufaika na miraa/mirungi
 
Hili zao liruhusiwe tu nipande hata hapa home kwa matumizi binafsi
 
Back
Top Bottom