GenuineMan
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 6,260
- 14,470
mmuache apumzike.Enzi za bwana yule ungetokwa mapovu kama yeye ndie anayeikuibia laivu saivi unalalamikia dawasa na sio rais mwenyewe. Je kama hayo ni maagizo toka juu
Hahahah.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mmuache apumzike.Enzi za bwana yule ungetokwa mapovu kama yeye ndie anayeikuibia laivu saivi unalalamikia dawasa na sio rais mwenyewe. Je kama hayo ni maagizo toka juu
Hapa umenena,niliwahi kuwalaumu sana DAWASCO, wakanishauri hivyo hivyo.Nikaleta fundi kuja kuangalia mpira unaopeleka maji kwenye tanks kubwa za juu ulikua unavuja kidogo kidogo sasa fikiria panavuja muda wote na ilikuwa sehemu ya garden hata hujui kama panavuja.Niliporekebisha tu sikuwa hi tena kugombana na DAWASCO swala la Bill.Kagueni miundombinu ya maji, saa zingine connector zinavujisha.
Kwa mazingira ya Dsm ya mchanga mwingi ni ngumu kugundua maji yanamwagika.
Wewe naye soma Mita ili ulinganishe.
Jaribu weka Tank, jaza Tank afu funga kwenye Mita, kwenye koki inayopeleka maji kwenye mita.
Basi tulieni sasa na huyu alaumiwe.Msifokee watu kwakuwa wanamlaumu Rais mnayempenda.Endeleeni kumlaumu JPM na wao waache wamlaumu aliyepo kwa sasaHizi ndiyo gharama za kuwa Kiongozi.Kama kuna mtu aliharibu hii nchi ni Magufuli. Yeye ndio muasisi wa huu upuuzi wa kusema rais, rais kwa kila jambo. Na watanzania wajinga wakawa wanaamini kila kitu ni rais. Ikafikia hadi mahali usipomtaja rais kwenye jambo fulani unaonekana uko kinyume naye.
bill za dawasa ni za kupikwa tu, wasoma mita wanatoka ofisini wanakusanyana kwenye vi pub wanakula na kulewa tu. wakimaliza kulewa wanaanza kupika bill.Kwako ndugu Waziri mwenye dhamana ya mambo ya maji.
Iko hivi:
Bili ambazo watu wa DAWASA wanawatumia wananchi siyo bili za kweli, haziakisi matumizi halisi ya maji ya wateja. Ni bili za kupikwa.
Haiwezekani bili yako kwa miezi ya nyuma iwe ni shilingi X halafu ghafla bin vuup bili inaamza kuja mara tatu ya ulivyokuwa ukitumia.
Ndugu Waziri, DAWASA na wizara ya maji isituone sisi wananchi ni Wapumbavu. Tunajua kuwa Unit Moja ya maji ni Lita 1000. Na Tunajua kuwa bei ya Maji kwa Unit Moja ni around shilingi 1670 hivi. Unapomletea mtu bili ya Maji ya Shilingi laki moja kwa mwezi maana yake ni kuwa katumia Unit 59.9 kwa mwezi ambayo ni sawa na Lita 59900! Hii inawezekanaje wakati Matumizi ni ya kawaida, kupikia, kuoga, kufua na maji hayatumiki kibiashara wala kwa kilimo na WALA HAKUNA LEAKAGE YOYOTE?
Ndugu Waziri nataka nikueleze ukweli, Familia nyingi zinatumia Chini ya Unit moja au maximum Unit moja kwa siku, lakini cha ajabu bili zinakuja zikiwa inflated sana.
Ndugu waziri,
Ninafahamu, kuwa kuna uhuni katika usomaji wa mita, wakati mwingine wale vijana hawazunguuki kusoma hizo mita wanakadiria!
Wakati mwingine kuna uhuni unafanyika kwenye kutuma meseji ya kiwango ambacho mtu anadaiwa, Sometime Message ya malipo haitaji Units ambazo mtu kazikuta mwanzo wa mwezi na mwisho wa mwezi anatajiwa Pesa tu. Yote hii ni kuficha traces ili wananchi wawe gizani kama billing imefanyika kwa haki au la
Ndugu Waziri,
Kisingizio kikuu ambacho DAWAS hutoa ni kwamba kuna leakage, lakini keakage wananchi tunaijua, kama kuna leakage basi Mita lazima itakuwa inazunguuka hata kama mtu hatumii maji!- Hapa kuna magumashi hapa
Ndugu Waziri,
Athari za kubambikiza watu kodi ya Maji ni watu kumchukia rais.
Kwa kuwa nchi hii hii power na mamlaka in reality ziko kwa rais( achilia mbali wananchi), basi madhila na maumivu yao lawama na manung'uniko haya ya bili za kubambika za maji wanamtupia rais. Na kwa kuwa maji yanagusa watu wote ndani ya familia, basi kitendo cha mlipa bili kumnung'unikia rais mbele ya familia nzima kunaifanya familia nzima isimuelewe rais.
Rai yangu:
1. Timiza wajibu wako kwa kuchunguza hizi bili feki za DAWASA
2. Vijana wavivu wasiokwenda site kusoma bili ila wanakaa kwenye computer kuzitengeneza fukuza kazi.
3. Toeni tamko la kuelezea kinagaubaga juu ya hili jambo linaloikwaza jamii
4. Shirikisheni wananchi kwenye kusoma mita. Mkisoma mita acheni kipande cha fomu kuwa mlikuja saa ngapi kusoma hiyo mita, mmekuta unit ngapi na mumtake mteja akahakiki. Siyo mnakuja kimyakimya kama wachawi. Hatuwaamini sisi!
Vijana wamepuwa target la makusanyo wasipofikisha wana fukuzwa kazi we unadhani watafanyaje sasa ili kupambania ugali lazima wafoji bills
Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
Mara nyingi zile mita hazina tatizo lolote lile.Hapa umenena,niliwahi kuwalaumu sana DAWASCO, wakanishauri hivyo hivyo.Nikaleta fundi kuja kuangalia mpira unaopeleka maji kwenye tanks kubwa za juu ulikua unavuja kidogo kidogo sasa fikiria panavuja muda wote na ilikuwa sehemu ya garden hata hujui kama panavuja.Niliporekebisha tu sikuwa hi tena kugombana na DAWASCO swala la Bill.
Kama maji yanavuja, hata kama ni leakage ndogo mita huwa inatembea. Sasa unakuta leakage hakuna, mita imetulia tuli pindi usipotumia halafu wanakubambika bili si la sayari hiiHapa umenena,niliwahi kuwalaumu sana DAWASCO, wakanishauri hivyo hivyo.Nikaleta fundi kuja kuangalia mpira unaopeleka maji kwenye tanks kubwa za juu ulikua unavuja kidogo kidogo sasa fikiria panavuja muda wote na ilikuwa sehemu ya garden hata hujui kama panavuja.Niliporekebisha tu sikuwa hi tena kugombana na DAWASCO swala la Bill.
Mara nyingi kwa kaya zenye familia ya wastani na matumizi ya kawaida ikiwemo umwagiliaji wa bustan 80-100K per month kama bill ni kawaida kabisaMara nyingi zile mita hazina tatizo lolote lile.
Miundombinu yetu ndio tatizo,sisi walikuwa wanalipa 200000 kila mwezi, baada ya kufatilia bill ikashuka hadi 97
U
Kwanza wasoma mita hawana uwezo wa kupita kila nyumba kusoma.
Hawana huo muda wa kujiumiza.
PILI, Sometimes MAJI hayatoki na wao hawana huo muda wa KULA HASARA.
BILL zinakadiriwa tu.
Kubali kataa, hiyo ndio HALI HALISI.
Basi tulieni sasa na huyu alaumiwe.Msifokee watu kwakuwa wanamlaumu Rais mnayempenda.Endeleeni kumlaumu JPM na wao waache wamlaumu aliyepo kwa sasaHizi ndiyo gharama za kuwa Kiongozi.
Mara nyingi zile mita hazina tatizo lolote lile.
Miundombinu yetu ndio tatizo,sisi walikuwa wanalipa 200000 kila mwezi, baada ya kufatilia bill ikashuka hadi 97
Maji yalikuwa yanavuja kwenye connectors, yaani lita lita 3000 kwa sikuTatizo lilikuwa ni nini hasa mpaka bill ilikuwa 200,000?
Tatizo nikwa wale wasoma mita ,sina uhakika na hili ila zamani nilisikia nikama wanalipwa kutokana idadi ya mita wanazo zisoma
Nyie Ni wazima? Sasa si upeleke picha ya mita kwa Sasa idara ya maji waambie haujafika hukoMbaya zaidi katika kuonyesha hizo units 15 wameandika kuwa nimetumia kutoka units 385 mpaka 400 wakati huu mita inasoma unita 389.
Unapiga simu badala uendeMimi waliniwekea units 40 wakati mimi kwa mwezi natumia units 5 tuu..
Meter inasoma umetumia units 5 ..ila bili kubwa na units nyingi...
Nimepiga simu mpaka nimechoka..
Wanatuma msg kwamba watakuja kukata maji.. Nawasubiri.. Safari hii watanijua... Na maji yenyewe wanaleta baada ya wiki mbili maeneo ya Kinyerezi