A
Anonymous
Guest
Kero ya wizi wa mita za maji Iringa mjini.
Siku za hivi karibuni kumejitokeza na wimbi la wizi wa mita za maji. Wizi huo umekithiri kiasi kwamba ukibiwa mita leo, na kesho ukienda ku report utapewa control number ulipie shilingi laki moja kama malipo ya kufungiwa mita mpya halafu ukifungiwa mita mpya usiku wa siku hiyo hiyo unaibiwa tena.
Hivi meneja wa IRUWASA Mkoa haoni hii kero kwamba imekua kubwa na kwamba inawatia wananchi hofu ya kulipia tena mita mpya. Au IRUWASA wameridhika na hii ya wizi wa mita ili waendelee kuingiza pesa za malipo ya mita mpya baada ya wizi??
Tunaomba Waziri wa maji utusaidie wananchi wa Iringa mjini, hii kero imekua kubwa mno na inatia hasira kuona hakuna juhudi zozote zinazochukuliwa IRUWASA kukomesha hii hali, ndio kwanza wizi unaendelea kila siku.