Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa azungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari

Kwa kudanganyika kwako kirahisi, sikupatii picha ungekuwa mwanamke halafu mrembo
πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£
 
Hawakuwa waandishi walikuwa wapambe sijawahi ona mwandishi aliekwenda shule anauliza maswali namna ile??Wengine walikuwa wanauliza maswali na kujijibu wenyewe kweli Tanzania ni nchi ya miujiza
Ndio mkuu nomeona yule dada aliyeseam aliandaa makala
 
unasifia nini? Isingekuwa kelele tayari ilashipita hiyo. Kelele zinasaidia kuweka mambo sawa
 
Msingwa alikuwepo? maana yeye upuuzi wake hesabu zake kasema kuna trillion 27 kwa Mwaka wakati wataalamu hawajui wala hawajapatana kiasi cha fedha.. njia ya muongo ni fupi!
 
Binafsi naona Hamza Johari ndie kashusha hoja za nguvu za makubaliano hayo na Dp World zinazoekeweka kwa wananchi nikiwemo mimi akieleza kwa lugha rahisi eleweka hata kwa layman

Nilichogundua kwenye hili sakata kumbe kuna watu wenye akili nyingi kama Hamza Johari lakini system haiwapi nafasi za juu za utawala wa nchi hawatutendei haki wananchi wajirekebishe Hamza Johari kuwa.na cheo kidogo cha Mkrugenzi wa hali ya hewa ni dharau na kutotutendea haki watanzania wajirekebishe kwa kweli

Hamza kuwa hiyo nafasi ya ukurugebzi mkuu wa anga ni kumuonea akili yake iko beyond ya hicho cheo

Anastahili kikubwa zaidi
 

Ndio anaruhusu watumie katiba yao ndani ya nchi yetu? Naye ni msomi? haogopi consequences zake? πŸ₯²πŸ₯²πŸ₯²πŸ₯²πŸ₯²
 
Mbarawa huyu Magufuli alimuona mjinga sana akamtimua.
 

Ni ngumu sana kuwaamini watu waongo waongo. Tumeshanganywa sana kwenye mambo tata. Escrow, gas Mtwara ambayo walisema sasa shida ya umeme itakuwa historia, bandari ya Bagamoyo ambayo sijui kwanini haijawahi kutokea.

Kwanini kwenye hili la bandari ya Dar Es Salaam? Kwanini tusione kufeli kwa ile bandari mpya kumekuwa kigezo cha kunyakua hii iliyopo?
Albert Einstein aliwahi kusema, kujiuliza kuna maana kubwa na kuna sababu zake. Naamini wote tunatitakia mema nchi yetu. Tunapoulizana tusionane wakaidi. Tunajuana sana na tunataka kila mtu awajibike na kutimiza wajibu wake ipasavyo
 
Ndio anaruhusu watumie katiba yao ndani ya nchi yetu? Naye ni msomi? haogopi consequences zake? πŸ₯²πŸ₯²πŸ₯²πŸ₯²πŸ₯²
Hapana hukunielewa wala hujamwelewa nafikiri hawatumii katiba ya mtu au nchi yeyote wanatumia sheria ya mikataba ya kimataifa ilivotungwa Viena ili kulinda mikataba yote duniani kwa hiyo uelewe hapo shida ni Hizo aina tatu
 
Mbarawa huyu Magufuli alimuona mjinga sana akamtimua.
Serikali impe cheo kikubwa zaidi ya Ukurugenzi wa wa anga Hamza Johari

Ateluliwe hata mbunge vya uteuzi a Raisi kisha apewe uwaziri haraka wa eneo lake yuko vizuri


Kuacha watu wenye akili nyingi na watetea maslahi ya nchi kama Hamza Johari kutokukuwa juu uongozi wa kitaifa ni kutotutendea haki wananchi

System ya nchi ijue hilo

Alipo ni cheo cha chini mno ni kumuonea na kuonea watanzania
 
Mbarawa huyu Magufuli alimuona mjinga sana akamtimua.
Mavi ya kale hayanuki binadamu aweza jirekebisha usiwe mtumwa wa Historia

Kwenye hili la makubaliano na DP World limekaa vizuri baada ya mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya anga ambaye pi aalikuwa mwenyekiti wa kuangalia kama DP world iwekeze Tanzania or not

Kichwani yuko vizuri mno tena sana
 
  • Mapungufu ya bandari ya Dar ndio yametumika kuwapa DP hati miliki BANDARI ZOTE ZA BAHARI NA MAZIWA TANZANIA BARA.
  • DP inaendesha bahari 6 Afrika nzima, ila kwa Tanzania bara pekee imejipatia bandari na maeneo ya kimkakati yasiyo na idadi wala ukomo
 
Hamza Johari aliyekuwa team leader kwenye majadiliano na Tp World apewe hongera nyingi na maua kwa kusimamia maslahi ya taifa
 
Huyu Waziri Mbarawa mbona hajajikita kujibu hoja za wanaoupinga mkataba huo? Hakuna anayesema hatuhitaji wawekezaji kwenye bandari, wala hakuna anayekataa kuwa bandari zetu zinahitaji maboresho makubwa. Kinachokataliwa ni mkataba mbovu ambao unatufunga mikono ya kukaribisha mwekezaji mwingine, hauna namna ya kuuvunja hata kama mambo yakiharibika. Yeye anatakiwa ajikita kwenye vifungu vinavyodaiwa kuwa vibovu. Anaishia tu kusema ni mkataba mzuri bila kufafanua vile vifungu vyenye ukakasi!!
 
Wanafiki ndo wapo karobu Na mama ukiagundulika ulikuwa Karibu na bwana yule lazima utupwe nje .wapi kabudi, lukuvi
 
Wanafiki ndo wapo karobu Na mama ukiagundulika ulikuwa Karibu na bwana yule lazima utupwe nje .wapi kabudi, lukuvi
Wahuni walimdanganya mama kwamba mafanikio yake ni kuwafukuza waliokuwa karibu na Magufuli.

Hilo la kuwafukuza amefanikiwa kwa 100%.

Baada ya kuwatimua, sasa Meli imepoteza mwelekeo
 
Wanafiki ndo wapo karobu Na mama ukiagundulika ulikuwa Karibu na bwana yule lazima utupwe nje .wapi kabudi, lukuvi
Kabudi na Lukuvi walikwisha choka sana tena wanadharau wanawake hawana sifa za ukweli na demokrasia ya haki za watu hawafai
 
Wahuni walimdanganya mama kwamba mafanikio yake ni kuwafukuza waliokuwa karibu na Magufuli.

Hilo la kuwafukuza amefanikiwa kwa 100%.

Baada ya kuwatimua, sasa Meli imepoteza mwelekeo
Magufuli na manabii zake walikuwa wanahukumu watu kufa na kuwasulubisha mungu hapendi hayo akaingilia kati kama unamtaka mfuate ahera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…