Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 6,696
- 6,734
π π π π π π π πKwanini Bandari za zanzibar ziwemo wakati tayari washapewa Makaburu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
π π π π π π π πKwanini Bandari za zanzibar ziwemo wakati tayari washapewa Makaburu
Na wewe utahama lini nchi kuwafuata hao mabwana zako Waarabu wa Dubai?Hama nchi
Ngumi ya chembe hii....na bado! Maana wanajichanganyaAma kweli wameshikwa pabaya.
Mkurugenzi mkuu wa TCAA mamlaka ya anga, pia ni mwanasheria aliyehusika katika mikataba mingi ya serikali kuanzia 2015.Hivi Hamza Johari ni nani katika mkataba huu? Anaupambania sana
Humo humoooooooooooooo mzee mwenzanguMpuuzi mkubwa, bladifaken
Asante. Cha msingi ni kusikiliza kilio cha watu kuhusu maboresho ya mkataba wa aina hii. Kulazimisha uko sawa wakati unaonekana una shida, inapoteza imani na wale wanaoutetea.Mkurugenzi mkuu wa TCAA mamlaka ya anga, pia ni mwanasheria aliyehusika katika mikataba mingi ya serikali kuanzia 2015.
Why?Leo Mbowe ahairishe tu Mkutano wake.
Leo watu wanajadili kongamano la waandishi wa habari na wizara ya miundombinu.Why?
Hayo ya Mkataba sijui Makubaliano naona wamekosa tafsiri sahihiSasa wanakubali kwa vigezo vipi vilivyoainishwa na kueleweka?
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam muda huu kuhusu uwekezaji wa Bandari.
Mbarawa:
Pamoja na Serikali kuendeleza juhudi za maboresho ya Bandari zetu, bado ufanisi katika utoaji huduma wa Bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
Hali ya ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine nyingi zinazoendeshwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania upo chini sana, udhaifu huo unaonekana katika utendaji wa kila siku wa Bandari zetu pamoja na ukusanyaji wa mapato
Bandari ya Dar imeendelea kuwa nyuma dhidi ya Bandari shindani katika Kanda, mfano wastani wa meli kusubiri nangani ni siku 5 sawa na Saa 120 ikilinganishwa na siku 1 na saa 6 kwa bandari ya Mombasa.
Meli kutumia muda mrefu kupakia shehena kantini kwa wastani wa siku tano wakati kimataifa ni siku moja inayokubalika kimataifa.
Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana mifumo ya kisasia ya TEHAMA, kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari ya kuhifadhia shehena za mizigo pamoja na maegesho ya kutosha ya kuegeshea meli.
Changamoto nyingine ni kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa inayobadilika mara kwa mara kutokana na teknolojia na hivyo kuwa na gharama kubwa.
Athari za kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni meli kusubiri muda mrefu nangani, mfano gharama ya meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takribani Dola 25,000 (Tsh. Milioni 58).
Meli kutumia wastani wa siku tano kupakia na kupakua shehena ukilinganisha na siku 1 inayokubalika kimataifa.
Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa, hivyo kusababisha bandari yetu kuwa inayolishwa na Bandari nyingine.
Uwezo mdogo wa Bandari ya Dar unaikosesha Nchi mapato makubwa ambayo yangeweza kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa Nchini.
Ili kutoendelea na hali hiyo, Serikali iliingia makubaliano 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji na Kampuni ya TICTS, mkataba ambao ulidumu kwa miaka 22 na kuipa haki za kipekee TICTS kuendesha shughuli za gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam huku maeneo mengine yakihudumiwa na TPA.
Desemba 2022, Serikali ya Awamu ya 6 baada ya kuona mkataba hauendani na maslahi mapana ya Nchi yetu iliamua kusitisha mkataba huo.
Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania ilipokea mapendekezo ya wawekezaji mbalimbali Duniani, lengo kuu likiwa ni kufungua masoko ya kimkakati katika kufungua eneo la bidhaa na usafirishaji ndani ya Nchi na maeneo yanayotuzunguka.
Baada ya uchambuzi wa kina Serikali ilianzisha majadiliano na Kampuni ya DP World kwa sababu zifuatazo:
Uwezo mkubwa wa uendeshaji wa shughuli za Bandari Afrika, Asia, Ulaya, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Australia.
DP World ina uwezo na kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambapo bidhaa zinatoka hadi kwa walaji wa bidhaa.
DP World inamiliki zaidi ya meli 400 za mizigo, ina uzoefu wa uendeshaji wa Bandari 6 Afrika na zaidi ya Bandari 30 Duniani kote.
Wawekezaji wengine waliowasilisha mapendekezo yao hayakukidhi sifa kwa mwekezaji ambaye alihitajika.
Mkurugenzi TCCA: Hakuna ardhi ya Tanzania ambayo itauzwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini, Hamza Johari amewatoa hofu Watanzania kuhusu tarifa za kuwa nchi imeuzwa kutokana na mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai akisema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 14, 2023 alipokuwa akizungumza katika mkutano na wahariri jijini Dar es Salaam huku akiwataka watu kutoingiza siasa kwenye masuala yahusuyo uchumi wa nchi na kusisitiza kuwa mkataba huo ni mzuri.
Sahihi kabisa wengi wanaongea viongozi wakubwa tu wa serikali na bunge na wabunge viichwani hamna kitu wanachoelewa kwa undani kuhusu hicho kitu kinaitwa makubaliano au mikataba.Wengine kazi kutukana na vitusho ohh serikali ina mkono mrefu ooh wapingaji washughulikiwe hoja ya maana hawSerikali iweke watu makini kujibu hoja za bandari
SahihiSerikali iweke watu makini kujibu hoja za bandari