Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa azungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa azungumza kuhusu uwekezaji wa Bandari

Mkurugenzi mkuu wa TCAA mamlaka ya anga, pia ni mwanasheria aliyehusika katika mikataba mingi ya serikali kuanzia 2015.
Asante. Cha msingi ni kusikiliza kilio cha watu kuhusu maboresho ya mkataba wa aina hii. Kulazimisha uko sawa wakati unaonekana una shida, inapoteza imani na wale wanaoutetea.
Nchi hii ni yetu sote. Tuko watu mil 60. Kutosikiliza wengi kunaleta sintofahamu zisizo na sababu. Ksema wanalazimisha kwenda peke yao, wakaacha wengi nyuma, pia ni kujilisha uongo. Lazima kwa kiasi kikubwa twende pamoja
 
Hata maboresho huenda ikawa mashaka!

Wanashauri Rais aupige chini mara moja Kwa a manufaaa ya Umma?!
 
Hajajibu maswali ambayo mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka kujua uyo DP - WD. Makubaliano/mkataba ni w miaka mingapi?

Yani wandishi w Habari wa Tanzania hawajui kuhoji wao ni Ndioooooooooo kama wabunge tu.
 
Naomba nikili wazi nimefatilia Kwa umakini mjadara wa Bandari yetu ulioongozwa na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri ndugu Ta Balile nikili Mimi nmeelewa mengi Sana ambayo nilikuwa pumbuwazi!

Yamesemwa mengi lazima tukubaliane Tu yakuwa asilimia 35% za hisa za kampuni ya Dp world zitauzwa Kwa wazawa tukubaliane yakuwa zitaondoka na MTU kama sio watu.

Nasema hivyo uku nikireje na kukumbuka yakuwa MH Ta kalamagi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera anayo nguvu kubwa ya ushawishi happ Bandarini na tukutumbuke,Mzee kalamagi hakuwa mmiliki wa Ticks alikuwa dalali Tu baadae akapewa mgao wa hisa akaliingiza taifa lilipo kupitia bandari yetu.

Lazima tukubaliane yakuwa nguvu kubwa inayopigwa dhidi ya vifungu vya mkataba kuna sehemu ya ndulu inachangiwa na mwenyekiti huyu wa Γ§cm.

Ninavyooona Hali hii ili kuitimisha Jambo ili vyema ni Bora kampuni ya Dp world hiO asilimia 35% zimilikiwe na serikali na sio watu binafsi.

Kinyume chake hizo zitakuwa Mali ya wabunge walio kwenda Dubai,zitakuwa Mali ya akina kitenge na kundi lake, zitakuwa na makame Mbalawa,waziri usika najua hawezi kukubali akose maana amenangwa Sana Mzee wa wawatu.
 


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Dar es Salaam muda huu kuhusu uwekezaji wa Bandari.

Mbarawa:
Pamoja na Serikali kuendeleza juhudi za maboresho ya Bandari zetu, bado ufanisi katika utoaji huduma wa Bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.

Hali ya ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na nyingine nyingi zinazoendeshwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania upo chini sana, udhaifu huo unaonekana katika utendaji wa kila siku wa Bandari zetu pamoja na ukusanyaji wa mapato

Bandari ya Dar imeendelea kuwa nyuma dhidi ya Bandari shindani katika Kanda, mfano wastani wa meli kusubiri nangani ni siku 5 sawa na Saa 120 ikilinganishwa na siku 1 na saa 6 kwa bandari ya Mombasa.

Meli kutumia muda mrefu kupakia shehena kantini kwa wastani wa siku tano wakati kimataifa ni siku moja inayokubalika kimataifa.

Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana mifumo ya kisasia ya TEHAMA, kutokuwepo kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari ya kuhifadhia shehena za mizigo pamoja na maegesho ya kutosha ya kuegeshea meli.

Changamoto nyingine ni kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa inayobadilika mara kwa mara kutokana na teknolojia na hivyo kuwa na gharama kubwa.

Athari za kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni meli kusubiri muda mrefu nangani, mfano gharama ya meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takribani Dola 25,000 (Tsh. Milioni 58).

Meli kutumia wastani wa siku tano kupakia na kupakua shehena ukilinganisha na siku 1 inayokubalika kimataifa.

Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa, hivyo kusababisha bandari yetu kuwa inayolishwa na Bandari nyingine.

Uwezo mdogo wa Bandari ya Dar unaikosesha Nchi mapato makubwa ambayo yangeweza kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa Nchini.

Ili kutoendelea na hali hiyo, Serikali iliingia makubaliano 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji na Kampuni ya TICTS, mkataba ambao ulidumu kwa miaka 22 na kuipa haki za kipekee TICTS kuendesha shughuli za gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam huku maeneo mengine yakihudumiwa na TPA.

Desemba 2022, Serikali ya Awamu ya 6 baada ya kuona mkataba hauendani na maslahi mapana ya Nchi yetu iliamua kusitisha mkataba huo.

Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania ilipokea mapendekezo ya wawekezaji mbalimbali Duniani, lengo kuu likiwa ni kufungua masoko ya kimkakati katika kufungua eneo la bidhaa na usafirishaji ndani ya Nchi na maeneo yanayotuzunguka.

Baada ya uchambuzi wa kina Serikali ilianzisha majadiliano na Kampuni ya DP World kwa sababu zifuatazo:

Uwezo mkubwa wa uendeshaji wa shughuli za Bandari Afrika, Asia, Ulaya, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Australia.

DP World ina uwezo na kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambapo bidhaa zinatoka hadi kwa walaji wa bidhaa.

DP World inamiliki zaidi ya meli 400 za mizigo, ina uzoefu wa uendeshaji wa Bandari 6 Afrika na zaidi ya Bandari 30 Duniani kote.

Wawekezaji wengine waliowasilisha mapendekezo yao hayakukidhi sifa kwa mwekezaji ambaye alihitajika.

Mkurugenzi TCCA: Hakuna ardhi ya Tanzania ambayo itauzwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini, Hamza Johari amewatoa hofu Watanzania kuhusu tarifa za kuwa nchi imeuzwa kutokana na mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai akisema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 14, 2023 alipokuwa akizungumza katika mkutano na wahariri jijini Dar es Salaam huku akiwataka watu kutoingiza siasa kwenye masuala yahusuyo uchumi wa nchi na kusisitiza kuwa mkataba huo ni mzuri.

Upuuzi mtupu. Ndiyo maana wanaotetea mkataba huu, wanaonekana dhahiri kuwa ni waongo, wanafiki, majizi na wala rushwa. Tofauti na wanaopinga ambao hoja zao zinaonekana wazi, wanaotetea wanabwabwaja tu.

Kweli ni ngumu sana kuutetea uovu.

Kama wangekuwa ni watu wakweli wangekuwa wanasoma vifungu vya mkataba na vifungu vya sheria na katiba kuonesha jinsi mkataba huo ulivyokidhi sheria zetu.

Wangekuwa ni wakweli wangeonesha tangazo la kuitisha tenda. Wangekuwa ni wakweli wangeyataja hata makampuni yaliyoshindanishwa na DP.

Kwa ujinga walio nao, na dhamira yao chafu, wanaishia kusema eti DP imewekeza kwenye nchi 30 LAKINI hawathubutu kuitaja hata nchi moja kati ya hizo 30 yenye mkataba wa kishenzi kama huu wa kwetu.
 
Serikali iweke watu makini kujibu hoja za bandari
Sahihi kabisa wengi wanaongea viongozi wakubwa tu wa serikali na bunge na wabunge viichwani hamna kitu wanachoelewa kwa undani kuhusu hicho kitu kinaitwa makubaliano au mikataba.Wengine kazi kutukana na vitusho ohh serikali ina mkono mrefu ooh wapingaji washughulikiwe hoja ya maana haw

Wako empty mno vichwani wanahangaika ku force kuwa watu waelewe faida za uwezekezaji wa DP World

Wananchi hawana shida na kujua faida wanapigia yowe vipengele vilivyomo kwenye hayo makubaliano wanavyodhani vibovu ndio concern yao

Hawana shida na Dp World kama mwekezaji

Mwanasheria aliyesimamia hayo makubaliano Hamza Johari kaeleza vizuri mno

Wanasiasa wasidakie dakie sana mambo ya kitaalamu wawaachie wataalamu husika waliohusika na makubaliano wafafanue ni nini hicho walikikubali kwa wananchi wakiwa timu ya makubaliano

Binafsi nimemwelewa sana Hamza Johari

Anaelewa kila kitu kwa kina kilichoko kwenye makubaliano

Mikataba yote itakayotengenrzwa kwenye mikataba na Dp world apewe uongozi kama team leader wa uandishi wa hiyo mikataba nina imani naye
 
Serikali iweke watu makini kujibu hoja za bandari
Sahihi

Wengine kazi kutukana na vitisho ohh serikali ina mkono mrefu ooh wapingaji washughulikiwe hoja ya maana kama za Hamza Johari hawana

Sijui wanamtisha nani washenzi wakubwa kwenye issue za.maslahi ya nchi hakutakiwi kutishana wala ubabaishaji jenga hoja

Mtu ana hoja atoe sio ohh serikali ina mkono mrefu mara ohh wapingaji wamenunuliwa mara ooh wapiganaji wachukuliwe hatua mara ohh vizee vipingaji vijinga na vipumbavu au ohh wapingaji ndio walikuwa wezi bandarini
Hoja dhaifu mno
Hamza Johari kajenge hoja za uhakika
 
Back
Top Bottom