Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Wadau hamjamboni nyote?
Wakati mvutano unaendelea huko Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya kisasi ya Israel dhidi ya Iran, Marekani imeionya Tehran dhidi ya mipango yoyote wa kulipiza kisasi.
Pentagon imesema kuwa mashambulizi ya Israel ya Jumamosi yanakusudiwa kumaliza uhasama kati ya mataifa hayo mawili.
"Iran haipaswi kufanya kosa la kujibu mashambulizi ya Israel, mashambulizi ambayo yanapaswa kuwa mwisho wa mtafaruku huu," alisema Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.
Rais wa Marekani Joe Biden alisema anatumaini kuwa mashambulizi hayo dhidi ya Iran yatakuwa mwisho wa mzunguko wa muda mrefu wa kuongezeka kwa mivutano. “Natumaini huu ndio mwisho,” aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi.
Wakati huo huo, Iran ilionekana kupuuza shambulizi hilo, ikisema kuwa ina majukumu katika kulinda amani na usalama wa kanda hiyo.
Source: India Today