Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin aionya Iran kuwa ikithubutu kujibu shambulizi la Israeli huo ndiyo utakuwa mwisho wake!

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin aionya Iran kuwa ikithubutu kujibu shambulizi la Israeli huo ndiyo utakuwa mwisho wake!

Samahani mkuu; please I'm sorry. Hiyo conclusion yako kwamba alionya......, kwamba "USA aliogopa consequence ya majibi kutoka Iran" umetoa kichwani kwako au umesoma sehemu? Unajua madhara ya nuclear KUVUJA? Wengi humu tunachangia kwa mahaba na ushabiki zaidi kuliko facts. Israel amekua anafanya anacho kitaka Tehran muda wowote na sio leo, over 10 years na Iran hajawahi kufanya chochote kwa Israel hadi vita hivi vya juzi! Brothers, hivi tunatunzaga risiti kweli? Israel kaua wataalamu wa nuclear wa Iran tena pale pale Tehran na Iran ilijua kwamba hizo ni kazi za Mossaid and he did nothing, Israel juzi ameua rais wao akiwa under escorts ya chopper za jeshi and Iran did nothing, kama haitoshi, wakati wa mazishi ya rais Rais same Israel kaja kaua kiongozi mkuu wa Hamas mahali alipowekewa ulinzi wa kutosha? Guys, wekeni ushabiki pembeni, jadirini facts. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, Iran kamshambulia mu Israel only 2 times na mara zote Israel kajibu, though hi ya pili alichukua over 3 weeks; bado utasema mazayuni waoga? Hi ya pili, USA walivujisha kwamba soon Israel ataishambulia Iran, jamaa wakasitisha but look, juzi wamepiga, propaganda zimekua nyingi kwamba eti madhara yamekua kidogo, wengi humu tukaaminishana, kila mmoja na upande wake, kwa mtu asie na mahaba angejiuliza swali, Israel kapeleka ndege za kivita 100 Iran, Iran anasema madhara yamekua kidogo, that's good, now two questions:-
1. Ndege 100 halafu ushindwe kutungua hata moja na udanganye kwamba hakukua na madhara?
2. Why unakimbilia umoja wa mataifa kwenda kushtaki na hakukua na madhara na wewe unajiamini, mashtaka yako eti Israel kanishambulia, what did you do to him on 01 October?
Ni wavivu wa kufikiri pekee yao ndio wanaweza kudhani Iran hakuathirika na mashambulizi ya juzi Jumamosi
Ndege zilikuwa nje ya Iran zilikuwa kwenye anga la Iraq waliogopa ata kusogea anga la Iran ni kama vile unapiga kwa kutokujiamini unaogopa ogopa lakini mwisho wa siku si umeona icho walichorusha kimepanguliwa, hakuna madhara aibu tupu waliopata hao mazayuni
 
Sasa kwanini Wasionye Israel Waje kuonya Iran..

Yaani Chukulia Wewe Ni mwalimu Kuna mwanafunzi W Darasa la pili kampiga makofi na Fimbo mwanafunzi wa Darasa la sita halafu unamuonya mwanafunzi wa Darasa la.Sita na unamuambia asirudishe kumpiga wala kumuadhibu atakiona Cha moto..

Kwanini usimuonye Mwanafunziwa Darsa la Pili aache kumchokoza??

Hata Israel alionywa asilipize lakini Israel akakaidi na kulipa . US sasa
anamuonya Iran kwa sababu Irani akilipa kisasi ,Israel atarusha tena makombora na mwishowe atalipua visima vya mafuta na vinu vya nyuklia
 
Wadau hamjamboni nyote?

Wakati mvutano unaendelea huko Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya kisasi ya Israel dhidi ya Iran, Marekani imeionya Tehran dhidi ya mipango yoyote wa kulipiza kisasi.

Pentagon imesema kuwa mashambulizi ya Israel ya Jumamosi yanakusudiwa kumaliza uhasama kati ya mataifa hayo mawili.

"Iran haipaswi kufanya kosa la kujibu mashambulizi ya Israel, mashambulizi ambayo yanapaswa kuwa mwisho wa mtafaruku huu," alisema Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema anatumaini kuwa mashambulizi hayo dhidi ya Iran yatakuwa mwisho wa mzunguko wa muda mrefu wa kuongezeka kwa mivutano. “Natumaini huu ndio mwisho,” aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi.

Wakati huo huo, Iran ilionekana kupuuza shambulizi hilo, ikisema kuwa ina majukumu katika kulinda amani na usalama wa kanda hiyo.

Source: India Today
Huyu Kiranja amekuwa msemaji wa Israel
 
Isaya 60:9-10
[9]Hakika yake visiwa vitaningojea,
Na merikebu za Tarshishi kwanza,
Ili kuleta wana wako kutoka mbali,
Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao,
Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako,
Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli,
Kwa kuwa amekutukuza wewe.
[10]Na wageni watajenga kuta zako,
Na wafalme wao watakuhudumu;
Maana katika ghadhabu yangu nalikupiga,
Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu.

Hao USA wanajipendekeza kama Neno la Mungu linavyosema
Angekuwa anajipendekeza Israël angepiga visima vya mafuta bila kusikiliza US anaongea nini
 
Ndege zilikuwa nje ya Iran zilikuwa kwenye anga la Iraq waliogopa ata kusogea anga la Iran ni kama vile unapiga kwa kutokujiamini unaogopa ogopa lakini mwisho wa siku si umeona icho walichorusha kimepanguliwa, hakuna madhara aibu tupu waliopata hao mazayuni
Chanzo chako cha habari? TBC ya Iran, right?
 
Juzi USA katoa onyo kwa Iran kwamba asijaribu kwa kulipiza shambulio vinginevyo atahadhibiwa.

Vinginevyo hata USA anahitaji vita sababu siraha zake nyingi mpya hajazijaribu ili kuona matokeo.

Kuna sisi ambao tunatamani kuona zikipigwa pande zote as upande wa NATO na ule wa BRICKS, kitu kibaya sisi sisimizi ndiyo tutaumia sana.
Usa yupo nato hapo kwa nini asiwagawie ukrain ili azijaribu kwa rusia
 
Ndege zilikuwa nje ya Iran zilikuwa kwenye anga la Iraq waliogopa ata kusogea anga la Iran ni kama vile unapiga kwa kutokujiamini unaogopa ogopa lakini mwisho wa siku si umeona icho walichorusha kimepanguliwa, hakuna madhara aibu tupu waliopata hao mazayuni
Tuendelee kusubiri mkuu; muda ni mwalimu mzuri. Hakuna sababu ya mimi na wewe kutofautiana kwasababu ya Israel na Waarabu; BTW wale ni ndugu, mimi na wewe ni Watanzania ambao we have a lot in common than those brethren. Hofu yangu ni mafuta kupanda bei, basi mengine hayanihusu mimi Mmwera
 
Bado mnasema Israel ndo Taifa Lenye Nguvu...
Anakupiga Mtu halafu onyo anatoa Mwingine Ole wako umrudishie 🤣🤣..
Ina maana anajua Ukimrudishia Watu watajua kuwa hana Nguvu 🤣🤣 kama anavyosifiwa
Tumia maarifa Silaha pesapanga mzigo Israel ameshik
 
Isaya 60:9-10
[9]Hakika yake visiwa vitaningojea,
Na merikebu za Tarshishi kwanza,
Ili kuleta wana wako kutoka mbali,
Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao,
Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako,
Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli,
Kwa kuwa amekutukuza wewe.
[10]Na wageni watajenga kuta zako,
Na wafalme wao watakuhudumu;
Maana katika ghadhabu yangu nalikupiga,
Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu.

Hao USA wanajipendekeza kama Neno la Mungu linavyosema
 
Israel ndio Boss !
anatuma Mbeya tu ,ila wewe hutaki unanuna ,Urusi kapeleka Manati huko Iraq zimepigwa kibiriti mbona hatujalalamika sisi Wayahudi wa Buza ?
 
Aisee lilikuwa suala la muda kwa Iran, now picha inasafishwa negative soon tutaiona printed 😀!.
Aah yaani usa nae haogopi fatah zile zama za aircraft carrier sijui B2 nyokonyoko zimepita ule upuuzi wa unique capabilitiey tupilia huko sasa hivi drones zimeweka uwanja sawasawa hata super power anachapika wamemshindwa myemen pale red sea wtaweza huku akipelekewa swamp ya air na sea drones wanafumua hayo maaircraft carrier na kupata uwendawazimu haya yetu macho wazichape tuendelee kuenjoy movie na mabisi yetu.
 
Back
Top Bottom