Huenda uko sahihi kwa kusema kuwa "wangetaka kutuua wangesha tumaliza kwa HIV/UKIMWI". Hata hivyo, unatakiwa uelewe kwamba lengo la hayo magonjwa kuenea si kuua maskini wa Afrika! Hapa ndo watu wengi wanashindwa kuelewa. Hawana mpango wa kuwaua waafrika na hawatakuwa nao hata siku moja kwasababu wananufaika kwa uwepo wao.
Hata hivyo, hii haizuii kuleta matatizo Afrika kwa makusudi na yakaleta madhara makubwa tu ili baadae waje na suruhisho. Hili lipo na lazima tulielewe hivyo
Toka enzi za mapinduzi ya viwanda ya kwanza karne ya 18 huko, malengo ya nchi za magharibi kwa Afrika yamebaki kuwa ni yale yale hadi leo:-
1. Afrika kubaki mzalishaji wa mali ghafi wanazohitaji wao kwenye viwanda vyao (Source of raw materials)
2. Afrika kuendelea kubaki eneo lao la uwekezaji lakini lisifaidike na uwekezaji huo (Area to invest theie surplus capital)
3. Afrika kuendelea kubaki soko la bidhaa kutoka kwenye viwanda vyao (Source of market for their manufactured goods)
Haya malengo hayajawahi kubadilika ila kinachobadilika ni namna (means) ya kuyafikia hayo malengo yao
Wakati wa ukoloni walitaka kufikia malengo hayo kwa nguvu na utawala wa wazi, lakini kadiri ya mabadiliko ya dunia na uelewa wa waafrika hupelekea nao kubadili mbinu na kuzifanya kuwa za kisasa zaidi.
Kwa mfano, wewe unasema ARV zinaokoa maisha ya wengi, ni sahihi kabisa na kwao katika hili wamefanikiwa kwasababu ili wakupe hizo ARV lazima ukubali kuunda nao "urafiki" utakaopelekea wao kutekeleza malengo yao niliyoandika hapo juu
Asilimia kubwa ya dawa za hospitali, chanjo, vifaa tiba na miradi ya utafiti katika sekta ya afya vinakuja kama msaada kwa "kivuli" cha kusaidia afya za waafrika lakini kimsingi wanatoa misaada hiyo wakishajihakikishia kupata fursa ya kutekeleza malengo yao
Hawawezi kuwaacha waafrika wateketee kwa HIV, cancer, kisukari, TB, na magonjwa mengine kwasababu watapoteza soko lao la ARV, madawa ya cancer, chanjo mbalimbali, nk. Watamuuzia nani? Uwekezaji wao katika tafiti za madawa, nk watamfanyia nani sasa?
Lazima kuwepo na wagonjwa ili soko la dawa liwepo.
Lazima kuwepo na magonjwa ili soko la chanjo liwepo
Lazima kuwepo na magonjwa mapya ili miradi ya tafiti za kisayansi ziendelee na watu wapate pesa
Ni lazima haya mambo tuyaangalie kwa mlengo huu, tuepuke kushabikia kila kinachokuja tukidhani kinakuja bila malengo mahususi
Point taken.
Muktadha unazingatiwa.
Niongeze tu another viewpoint.
ARV's zinahusiana moja kwa moja na afya ya Umma na Ustawi wa Jamii. ARV's ni muhimu katika kudhibiti VVU na kuboresha ubora wa maisha wa wahanga./waathirika
Misosi hii tuanayoletewa vs Afya: Mchele ,na hizo soy beans na mafuta ya kupikiwa Vimechakatawa, ikiwa na maana vimeongezwa hivo virutubisho(fortified), but they don't immediately treat life threatening conditions kamavile ARV's zinavyofanya.
Masuala ya afya ya mtu yanachukua uzito, kabla ya lishe.
Watoa misaada wanapaswa kutambua hilo, wananchi nao watambue hilo. it is not an Either or situation, hatahivyo nyanja zote ni muhimu.
Utu vs Uhuru, Nchi zinazotoa misaada ni lazima wazingatie utu, pamoja na kwamba wanatoa kwa uhuru na utu wao, ni lazima wakaheshimu utu na uhuru wetu-Aliyoyasema Mh. Bashe yalilenga Kuheshimu Utu na Uhuru wetu.
Ni lazima wajali utu wetu, kwani kila taifa bila ya kujali hali yake ya kiuchumi, linastahili heshima na uhuru. Umasikini wetu haumaanishi tupuuze heshima yetu au uhuru wetu, kinyume na hilo ni kupuuzia utu wetu na haki zetu-hatuwezi kuendelea hivyo.
it is just not sustainable,.
Ni muhimu vilevile kuwa misaada hiyo haipuuzi haki ya nchi kufanya maamuzi sahihi kuhusu misaada.
Tanzania ni taifa huru, na tuna haki ya kuamua kuhusu sera zetu wenyewe, ikiwa pamoja na kukataa msaada, bahati mbaya wengi wanao dai haki hizi huwa wanamalizwa mapema, hususani wa bara letu la Afrika, itoshe sisi tuna haki ya kukubali au kukataa msaada huo, saa nyingine kusema "No thank you" ni haki inayostahili kuzingatiwa na kuheshimiwa especially inapotoka kwa mtu/nchi unayetaka kumsaidia. Heko tena Mh. Bashe...
Kupokea misaada inayoendana na mahitaji ya ndani na vipaumbele ni muhimu zaidi kuliko kupokea misaada ambayo inaweza kuwa haifai.
Msaada huu wa Mchele ulio na virutubisho, hauendani na mahitaji, sio kipaumbele na haufai kwa mabinti wetu/watoto zetu.
Tuache ushabiki wa kukuza ukuu wa "Wazungu" kwa hoja hafifu kama "mbona hatukatai ARV's" ama mbona tunatumia kila kitu kutoka kwao.
Kweli ni hizo ni kebehi. Napinga msaada huu.