Na hapo ndo tatizo lilipo, ni ugonjwa mkubwa ambao umetuathiri sana, kwamba unapozungumzia kazi basi lazima mtu aajiriwe akae kwenye ofisi ya serikali. Ofisi ziko ngapi?! Wasomi mlivyo wengi ivyo mtaenea?! Mkuu maisha yetu ya kila siku duniani kote yanategemea uzalishaji wa viwandani na kilimo. Imarisha viwanda na kilimo, zalisha bidhaa bora utauza duniani kote. Aridhi nzuri na kubwa tu kwa ajili ya kilimo tunayo, maji tunayo...rasilimali viwanda tunazo kila mahala...kwanini hatuwekezi huko ili tutoe ajira kwa wahitimu wetu?! Fungua viwanda vingi, imarisha sekta ya kilimo, tutapunguza hili tatizo badala ya kusubiriana tustaafu ili ofisi wakalie wengine. Mtu anaajiriwa leo ili astaafu atafanya kazi miaka 30+, inamana wewe utamsubiri huyu astaafu ili uchukue nafasi yake so utakua ushazeeka na wewe?! Ukiuelewa huo mstari wangu wa mwisho sidhani kama utatilia tena maanani mambo ya ajira. The government employment circle is very complicated kwa sasa.