WAZO: kwanini serikali isipunguze muda wa kustaafu kwa watumishi wa umma

kama viongozi wa serikali wangelikua wanapitia hoja na maoni ya watu kwenye mitandao ya kijamii hakika tanzania tungelikua mbali sana . tukisema katiba mpya tunaambiwa mchakato unahitaji fedha nyingi ila pesa ya kuwapa viongoz wa dini zawad goli la mama zipo khaa! qumamakee
 
hata hao wazee nao walikia vijana kama ni experience waliipata kazini mbele ya safari
 
Pia uongozi wa muda mfupi mfupi, unaweza usilete tija, kwa sababu unakuwa unajua leo upo kesho haupo; inakuwa ni vigumu kutimiza yale malengo ya muda mrefu.​
 
well said
 
Serikalini hakuna hiyo mishahara labda uwe mbunge , nchi hii kwa mwendo wa demokrasia haiwezi kuendelea hata siku moja.
 
1. Miaka unatosuggest mtu ndo ana uzoefu na ni highly productive
2. Hao walioajiriwa wenyewe hata hawatoshi. Kuna sehemu mtu anafanya majukumu ya watu wengine hata wawili watatu , nikimaanisha, serikali haijawahi kujaza nafasi zinazohitajika.
 
Hii inaweza saidia kupunguza tatizo la ajira nchini ikibidi kutoka miaka 60 mpka 45 au 50 ili vijana nao wapate nafasi kwani hii itatoa nafasi nyingi katika kada mbalimbali .
Utukome.... Hivi hayo mashirika ya pensheni yatamudu kuwahudumia? Tetesi ni kwamba umri wa lazima kustaafu soon itakuwa 65
 
Hii inaweza saidia kupunguza tatizo la ajira nchini ikibidi kutoka miaka 60 mpka 45 au 50 ili vijana nao wapate nafasi kwani hii itatoa nafasi nyingi katika kada mbalimbali .
Acha roho ya kichawi wewe, nenda VETA kajifunze hata kufuga nyuki ili ujiajiri kuliko kuwachawia wenzio.

Ebu nipe mfano hata wa nchi 1 , baada ya ugumu wa ajira, umri wa kustaff ukashushwa then likaondoa tatizo la ajira. Au kama ili ni gumu sana, nipe mfano wa nchi hata 1 ambayo umri wa kustaff ni miaka 45.

Serikali inatoa 10% tu ya ajira zote za nchi hii, 90% yote ipo sector Binafsi, kama umeshindwa kupata kazi sector Binafsi na kuna 90% ya kazi huko, mimi naamini hata umri wakustaff ukipunguzwa BADO UTAKOSA KAZI TU. Nenda VETA.
 
Ukiona wanataka kuongeza majimbo ya Ubunge ujue watakuja kuongeza umri wa kustaafu ikiwezekana wafie kazini ili vijana wakose ajira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…