Wazo Muflisi: Alijaribu Kujitenga lakini Anarudi Bila Tenga...

IO...heshima yako
 

Huyu jamaa alishindwa je huyu ataweza...ngoja tuone
 
Siku hizi sisikii neno la wewe ni Sukuma gang 😆😁😁😂wote Sasahivi tunaimba wimbo mmoja, Samia shikilia hapo hapo mpaka 2025😂😂😁.
 
Kutoleana Macho na Kupigana Mikwara! Alijaribu kujitenga na habari za Bw. Yule; lakini sasa karudi tena karudi na naona na tenga analipiga mkwara. Tunakoelekea jina la Bw. Yule litaanza kuimbwa mbele zake kama alama za kumuunga mkono.
Ninyanyue tu sampuli ya kipande hiki kuwasilisha andiko zima na kusema: Sikubaliani/Nakubaliana.

Samia hata siku moja hawezi; hata kwa kuigiza kama anavyojaribu sasa kuwa kama Magufuli kwa njia yoyote ile.
Hili ni kosa moja la mada nzima.

Samia, toka aingie madarakani, hajui afanye nini. Hana msimamo madhubuti anao uamini yeye kama yeye; matokeo yake ndiko huko kuyumbayumba unako kuona, hasa kupitia katika utenguzi na uteuzi wa karibu kila wiki

Samia, hakuna chochote kinacho mpa msukumo kuwaongoza waTanzania, mbali ya kudondokewa na tunda la mwembe chini ya mti wa mchongoma. Kitu pekee kinacho mpendezesha ni kuwa na hayo madaraka makubwa ambayo hakuyategemea. Kwa bahati mbaya sana, kadakwa na genge, hasa huko huko ndani ya CCM, linalo tumia nafasi yake hiyo sasa kufanya uchafu wanaotaka.

Samia sasa kaja kugundua kuwa nafasi yake ipo mashakani, kwa sababu kule kujipendesheza kwa wananchi uliko kuelezea kwa ukweli, kumeshindikana. Kwa hiyo nafasi kwake kwa kushinda uchaguzi kwa kura hakupo; kwa hiyo njia pekee iliyo baki ni kuhakikisha anarudi madarakani kwa nguvu.
Katunga sheria ya kuwapoteza na kuwaua watu ili uoga baina ya watu ienee. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sasa ni Tamisemi ndio watahakikisha watu wao ndio watakao hakikisha huko mitaani kura za bandia za Samia zinapatikana
Hata katika haya, hakuna mfanano wowote na Magufuli

Yapo mengi, ya kumtofautisha Samia na Magufuli lakini ngoja niachie hapa.
 
Naam! Mwanzo alitaka ushauri wa JK, lakini baadaye akawatosa watu wa JK na kuanza kufuata ushauri wa Chawa
 
Huyu wako hata ungemfunga mgongoni kwako uwe unampa maelekezo unayodhani ni mazuri kwenu, bado nyote mtaanguka tu; kwa sababu akili zenu haziko 'tuned' kuwa viongozi.
Sasa anagalia kwa mfano haya uliyo andika hapa, na wewe mwenyewe umetoa hoja iliyo nyooka. Hata hujui 'ujamaa' ni nini, wala ubepari nao hujui unahusu nini!
Unaloweza kufanya ni kutapika tu uliyo jifunza vitabuni miaka kadhaa iliyopita wakati vita baridi ingali inaendelea!
 
Duh,
Nimeipenda hii staili ya uwasilishaji.

Pongezi kwako.
 
mafirauni ni mafirauni tu hawabebeki...sasa ngoja wapelekwe kama walivyozoea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…