Wazo Muflisi: Alijaribu Kujitenga lakini Anarudi Bila Tenga...

Tatizo siyo bwana yule na wala siyo bibi huyu, bali tatizo ni kwamba Katiba tuliyonayo ni mbovu na Sheria zilizopo ni kandamizi, hazifai.
 
Tofauti yake na Nchimbi ni hii;
1/.Dr.Nchimbi ni kiongozi [by nature]
2/Dr.Nchimbi ameelimika.
3/.Dr.Nchimbi haandaliwi hotuba,hutoa kichwani mwake
4/.Dr.Nchimbi husoma hali ya uwanja kabla hajaongea,kisha huongea kwa kuzingatia hali ya uwanja, HAKURUPUKI.
5/. HEKIMA imo ndani yake,huzingatia UZITO na UNYETI wa jambo analozungumzia.
 
Mtu mweusi huwa hapewi uhuru hata siku moja
Ni kweli… kama hii nchi hatukutakiwa kupewa uhuru kabisa, tulitakiwa tuendelee kutawaliwa na wakoloni.

How about this? au haufahamu mipaka ya kauli yako? 🚮
 
Hilo lako kweli ni wazo muflis, kabisa tena.

Kazi ya Mungu haina makosa.
Kazi ya Mungu ata Hangaya ndiyo anaandaliwa hivyo asiposhituka na kujiuzuru.
Unabadirisha Wakurugenzi wa TISS kama Wakuu wa Wilaya!🤣🤣🤣.
Ile hotuba ya juzi ni michezo anayochezewa;na atachezeshwa lege mpaka afurahi yaani.
Mwambieni vyombo vya usalama na ulinzi vina taratibu zake haviingiliwi,ameyatimba, mwambieni akae pembeni kwa usalama wake!!
 
= Unabadilisha.
Mchezo wa tarehe 23 umepigwa marufuku.
 
Wazo lako lingekuwa na maana kama ungesema serikali ifute mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Vinginevyo, ni ujinga mkubwa kusema arudishe siasa za kuwashughulikia wapinzani. Kama hawatakiwi, kwa nini mruhusu wawepo kisheria, in the first place?

Sikuelewa Magufuli alipoweka lengo la “kumaliza” upinzani kufikia 2020. Kama ilikuwa ni kwa kubadili sheria na katiba au kuondoa mawazo ya upinzani vichwani mwa watanzania wote!? Mawazo ya ajabu sana haya.

Halafu ni vigezo vipi vinavyopima wanasiasa uchwara na vibaraka? Na ni nani huyo mwenye mamlaka ya kupima na kuamua mambo hayo (regulator)?

Nijuavyo nchi inatakiwa kuendeshwa kwa AKILI na MAARIFA kwa sheria, kanuni na taratibu na si kwa HISIA za misimu.
 
Samia si tatizo letu.

Samia ni dalili tu ya tatizo letu.

Na kila tunavyo focus kwenye dalili ya tatizo na kuacha kuangalia tatizo lenyewe, tunazidisha tatizo.
Hakika ...hata kwenye andiko la MM kwa jicho la Tatu ...la sisi wachache unaliona tatizo!
 
Halafu MM anatushawishi tumkumbuke😭 labda tulinganishe!
 
Huna akili wewe.
 
Tanzania hakuna siasa za Vyama vingi ni maigizo.
 
Sifa za kuwa Kiongozi ni zipi huko kwenu ambazo ziko tuned?

Kwamba sijui ujamaa vs unepari si upinge hoja yangu Kwa hoja badala ya kujiswmesha kwa majigambo kama mabondia wanaojiandaa Kwa pambano.

Nasisitiza hakuna kuingiza ujamaa kwenye uchumi,hizo ziishie kwenye siasa za majukwaani na leadership style,mifano nimeshaiweka.
 
Hayo yote yalikuwa yanatabirika kirahisi sana na baadhi yetu tuliyatabiri kwa namna tofauti tofauti.

Ila, tulipojaribu kuwaambia, tukaishia kuchekwa na kuitwa ‘Sukuma Gang’ na majina mengineyo.

Wengine walitubeza kwamba hatuamini kilichotokea na wala hatuamini kinachoendelea na kwamba tuko kwenye ‘denial’ flani hivi.

Wengine wakawa hawachoki na hawaachi kutukumbusha kwamba Ngosha keshakufa na harudi tena.

Wapo baadhi yao, wachache kwa idadi, walioenda mbali zaidi na kusema kwamba tayari Ngosha huko aliko keshaoza na kuoza.

Dah! Basi tena….tukawa hatuna la kusema zaidi tu ya kuwakumbusha kwamba ni muda tu ndo utaoongea.

Wanasemaga hayawi hayawi na yame……

Sasa sijui imekuwaje tena maana vilio vimeongezeka na Ngosha hayupo na wala hatorudi tena.

Ushauri mdogo tu….maishani mtu ukitumia tajiriba [experience], busara za kawaida [common sense], kuyaangalia na kuyatathmini mambo kwa kutumia akili na uhalisia na si hisia, kwa kiasi kikubwa utajikuta unafanya maamuzi mengi yaliyo sahihi kuliko yale yasiyo sahihi.
 
Reactions: Cyb
Huyu amekuja na mpya ya kuteka WATU kwenye mabasi, nataka kusafir cjui nitumie usafiri gani.
 
alisema mtanikumbuka wao wakakazana kufanya asikumbukwe kwa kuonyesha mabaya yake na sasa sio muda mrefu watamkumbuka kwa mazuri
 
Tatizo karibu wote tunamuangalia rais kama ugonjwa, wakati rais ni dalili ya ugonjwa tu.

Ugonjwa upo katika jamii yote.

Mtoto anavyolelewa tu ni tatizo, sasa unategemea huyu mtoto akija kuwa rais ataongoza nchi vizuri?

Ndio maana Kuna wakati unawaza mambo yasiwezekana mfano Bora nchi wakabidhiwe consultants waendeshe. Tuwe na Rais kama mfalme Kwa maana ya Alana tu ya mamlaka ya taifa.

Hao jamaa wakamate Kila kitu. Kuanzia kukusanya Kodi, kusimamia uendeshaji wa miradi na mambo yote Kwa mujibu wa dira na malengo ya taifa.

Kurekebisha hili tatizo kwenye jamii itatuchukua muda sana, na hasa Kwa vile hatuanfalii chanzo Cha tatizo, tutaangalia matokeo ya tatizo.
 
Tatizo karibu wote tunamuangalia rais kama ugonjwa, wakati rais ni dalili ya ugonjwa tu.

Ugonjwa upo katika jamii yote.

Mtoto anavyolelewa tu ni tatizo, sasa unategemea huyu mtoto akija kuwa rais ataongoza nchi vizuri?
Umemsikiliza Jenerali Ulimwengu?
Rais anapokosea kosa lake ni kubwa kwa sababu ya nafasi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…